Anapoingia 'Dogo Janja' kuna ujanjaujanja

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Nimejiridhisha na sasa nawafahamisha. Namzungumzia kiongozi wetu hapa nchini, kiongozi mkubwa lakini kwa kubebwa bila kukabwa wala ubwabwa. Kiongozi kutokea jimboni hadi Bungeni na Serikalini. Watu wa mfumo wanamuita 'Dogo Janja'.

Ameshakuwa mzoefu na maarufu. Amekwepa mishale mingi na vigingi na sasa Watanzania hawampingi. wanamkubali kwa kila hali. Anakagua, anahutubia, anaagiza, anaonya, anahutubu bila kutubu, anatekeleza maagizo na maigizo, anaweza.

Amini nawaambia, popote mnapomuona anakagua, anapokea, anatoa, anahutubia, anafikisha salamu, au hata anauzungumzia mradi wowote wa kinchi au kiserikali au kichama, jueni kwamba mradi huo una ujanjaujanja. Una mashaka yenye uhakika, mashaka yenye mashiko kuliko mwiko.

Wenzangu wa kule nilikostaafia watakuwa wameshamjua. Wanatamani kumtaja kwa jina na kumzungumzia kwa kina lakini hawawezi. Hawathubutu. hawajaribu kwakuwa wataharibu. Dogo Janja anajipanga ingawa hapangiki bila mikikimikiki. Hapangiki kwakuwa haitajiki wala hatajiki.

Dogo Janja wa Kusini anashaini, anasavaivu kiushupavu bila uvivu ila wivu. Shaka inamvuata kila aingiapo. Shaka haimuachi bila kumsachi. Inaenda na yeye popote. Inatembea naye. Anapenda kuaminika na kukubalika bila mashaka. Ni mjanjamjanja. Lakini kiranja kwenye uwanja.

Mama Samia, nasi tuanze kampeni kama ufanyavyo?

Mzee Tupatupa (kwasasa Kilosa, Morogoro).
 
Janjaro yupo vizuri kwa madili...Nakumbuka alishawai kumfilisi shemeji yake wa buzwagi.
 
Nimejiridhisha na sasa nawafahamisha....

Amini nawaambia, popote mnapomuona anakagua, anapokea, anatoa, anahutubia, anafikisha salamu, au hata anauzungumzia mradi wowote wa kinchi au kiserikali au kichama, jueni kwamba mradi huo una ujanjaujanja. Una mashaka yenye uhakika, mashaka yenye mashiko kuliko mwiko....

Mzee Tupatupa (kwasasa Kilosa, Morogoro).
Kwa lile daraja la B7 amakweli ni mjanja mjanja nani anabisha kama ile sio chapati ngozi saba?

Anazingua milango ya buku mbilimbili kwa sababu haijapikwa kwa mafuta ya samli ...

Dogojanja Noma, na mkizidi kubisha mtakoma

Asante Vuta-Nikuvute
 
Tuliosoma Literature and Literature analysis kule Cuba na North Korea tumekuelewa Mzee.🤣🤣🤣
 
Nimejiridhisha na sasa nawafahamisha. Namzungumzia kiongozi wetu hapa nchini, kiongozi mkubwa lakini kwa kubebwa bila kukabwa wala ubwabwa. Kiongozi kutokea jimboni hadi Bungeni na Serikalini. Watu wa mfumo wanamuita 'Dogo Janja'.

Ameshakuwa mzoefu na maarufu. Amekwepa mishale mingi na vigingi na sasa Watanzania hawampingi. wanamkubali kwa kila hali. Anakagua, anahutubia, anaagiza, anaonya, anahutubu bila kutubu, anatekeleza maagizo na maigizo, anaweza.

Amini nawaambia, popote mnapomuona anakagua, anapokea, anatoa, anahutubia, anafikisha salamu, au hata anauzungumzia mradi wowote wa kinchi au kiserikali au kichama, jueni kwamba mradi huo una ujanjaujanja. Una mashaka yenye uhakika, mashaka yenye mashiko kuliko mwiko.

Wenzangu wa kule nilikostaafia watakuwa wameshamjua. Wanatamani kumtaja kwa jina na kumzungumzia kwa kina lakini hawawezi. Hawathubutu. hawajaribu kwakuwa wataharibu. Dogo Janja anajipanga ingawa hapangiki bila mikikimikiki. Hapangiki kwakuwa haitajiki wala hatajiki.

Dogo Janja wa Kusini anashaini, anasavaivu kiushupavu bila uvivu ila wivu. Shaka inamvuata kila aingiapo. Shaka haimuachi bila kumsachi. Inaenda na yeye popote. Inatembea naye. Anapenda kuaminika na kukubalika bila mashaka. Ni mjanjamjanja. Lakini kiranja kwenye uwanja.

Mama Samia, nasi tuanze kampeni kama ufanyavyo?

Mzee Tupatupa (kwasasa Kilosa, Morogoro).
Nishati vs PM.

Kazi ipooo.
 
Madaktari wa Tanzania na hata shirika la WHO lisipochukua hatua dhidi ya ugonjwa wa illusion, sijui niuite ugonjwa wa kuota mchana, au kuwaza mambo ambayo ni ya kufikirika, basi Tanzania itaongoza kwa ugonjwa huu ambao kimsingi, ni ugonjwa wa akili.

Ulishaona kichaa anakimbia lakini hakuna kinachomkimbiza, au anacheka lakini hakuna anayemchekesha, au anaongea mwenyewe tu.

Na inawezekana ugonjwa huu ni wa kuambukiza, mleta mada itakuwa kaambukizwa na Godbless Lemma, huyu ndio anahitaji matibabu ya dharura. Huyu akishavuta madawa ya kulevya, basi huwa anaona vitu vinaelea angani, anamuona Lissu amekaa ikulu, anamuona Mbowe akiongoza vikao vya Bunge kama spika, anamuona fulani anautaka uraisi......,akiamka , anajikuta kituo Cha kuoshea na kulelea wazee anaingia shifti
 
Dogo janja alikuwa kiongozi/mbunge si mkumbuki vizuri. Wakati flani alikuwa na issue ya maumbwa wake kuuliwa na fikiri. Unategemea ulinzi wa maumbwa wakati Neno linasema amelaaniwa amtumainiye mwanadamu. Sijui wa kutumainia mbwa anakuwa wa fungu lipi.
 
Walimu wa kiswahili wasiajiriwe
Wanatuharibia nchi
Mifumbo kama yote
 
Nimejiridhisha na sasa nawafahamisha. Namzungumzia kiongozi wetu hapa nchini, kiongozi mkubwa lakini kwa kubebwa bila kukabwa wala ubwabwa. Kiongozi kutokea jimboni hadi Bungeni na Serikalini. Watu wa mfumo wanamuita 'Dogo Janja'.

Ameshakuwa mzoefu na maarufu. Amekwepa mishale mingi na vigingi na sasa Watanzania hawampingi. wanamkubali kwa kila hali. Anakagua, anahutubia, anaagiza, anaonya, anahutubu bila kutubu, anatekeleza maagizo na maigizo, anaweza.

Amini nawaambia, popote mnapomuona anakagua, anapokea, anatoa, anahutubia, anafikisha salamu, au hata anauzungumzia mradi wowote wa kinchi au kiserikali au kichama, jueni kwamba mradi huo una ujanjaujanja. Una mashaka yenye uhakika, mashaka yenye mashiko kuliko mwiko.

Wenzangu wa kule nilikostaafia watakuwa wameshamjua. Wanatamani kumtaja kwa jina na kumzungumzia kwa kina lakini hawawezi. Hawathubutu. hawajaribu kwakuwa wataharibu. Dogo Janja anajipanga ingawa hapangiki bila mikikimikiki. Hapangiki kwakuwa haitajiki wala hatajiki.

Dogo Janja wa Kusini anashaini, anasavaivu kiushupavu bila uvivu ila wivu. Shaka inamvuata kila aingiapo. Shaka haimuachi bila kumsachi. Inaenda na yeye popote. Inatembea naye. Anapenda kuaminika na kukubalika bila mashaka. Ni mjanjamjanja. Lakini kiranja kwenye uwanja.

Mama Samia, nasi tuanze kampeni kama ufanyavyo?

Mzee Tupatupa (kwasasa Kilosa, Morogoro).
Tulikumiss sana MZEE TUPATUPA WA LUMUMBA MWAGA NONDO
 
Back
Top Bottom