Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Dah! Nimekoshwa na hivyo vina ambavyo kiuhalisia ni majanga! Ghafla nimepitiwa na kivuli cha utambulisho wa msanii wa bongo fleva ajulikanaye kama Dizasta Vina. Siujui muziki wake bali jina linaakisi majanga ndani ya vina vya shairi hili maridhawa.Nimejiridhisha na sasa nawafahamisha. Namzungumzia kiongozi wetu hapa nchini, kiongozi mkubwa lakini kwa kubebwa bila kukabwa wala ubwabwa. Kiongozi kutokea jimboni hadi Bungeni na Serikalini. Watu wa mfumo wanamuita 'Dogo Janja'.
Ameshakuwa mzoefu na maarufu. Amekwepa mishale mingi na vigingi na sasa Watanzania hawampingi. wanamkubali kwa kila hali. Anakagua, anahutubia, anaagiza, anaonya, anahutubu bila kutubu, anatekeleza maagizo na maigizo, anaweza.
Amini nawaambia, popote mnapomuona anakagua, anapokea, anatoa, anahutubia, anafikisha salamu, au hata anauzungumzia mradi wowote wa kinchi au kiserikali au kichama, jueni kwamba mradi huo una ujanjaujanja. Una mashaka yenye uhakika, mashaka yenye mashiko kuliko mwiko.
Wenzangu wa kule nilikostaafia watakuwa wameshamjua. Wanatamani kumtaja kwa jina na kumzungumzia kwa kina lakini hawawezi. Hawathubutu. hawajaribu kwakuwa wataharibu. Dogo Janja anajipanga ingawa hapangiki bila mikikimikiki. Hapangiki kwakuwa haitajiki wala hatajiki.
Dogo Janja wa Kusini anashaini, anasavaivu kiushupavu bila uvivu ila wivu. Shaka inamvuata kila aingiapo. Shaka haimuachi bila kumsachi. Inaenda na yeye popote. Inatembea naye. Anapenda kuaminika na kukubalika bila mashaka. Ni mjanjamjanja. Lakini kiranja kwenye uwanja.
Mama Samia, nasi tuanze kampeni kama ufanyavyo?
Mzee Tupatupa (kwasasa Kilosa, Morogoro).
Lakini mhusika ni dogo wa ukweli au kubwa jinga mwingine anayejizuga?