Anapolilia wembe umpe au umtahadharishe?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Sijui ni kwa nini haturidhiki na kidogo ambacho tulichonacho na hata kudiriki kukikashifu kuwa hakina umaana wowote ule wakati tunacho. Sasa unapokuwa umenyang'anywa ndipo unatambua kuwa kumbe khali yako ilikuwa ni bukheri sana bila ya wewe kujitambua.........na kukumbuka neema nyingi ambazo Mwenyezi Mungu alikushushia lakini wewe hukuona na hivyo kudharau.

Tujifunze kuthamini kidogo tulichonacho kwa sababu kuna sababu ambazo Mwenyezi Mungu ameona ndicho kinachotutosha ili tuishi kwa amani na furaha humu duniani. Utakapoanza kufukuzia makubwa ndipo utakapoweka rehani afya yako, usalama wako, utu wako na hata mengineyo ambayo........kwa hiyo mihangaiko, tunakuwa sawa na mtoto ambaye analilia wembe na Mwenyezi Mungu kwa majonzi na masikitiko makubwa huamuru malaika zake tupewe huku akijua ya kuwa hicho kiu cha makubwa kitakuletea kiama chako.

Soma Jeremiah 45:5 kwa elimu ya ziada............." And do you seek great things for yourself? Do no seek them; for behold, I will bring adversity on all flesh," Says the LORD, "But I will give your life to you as prize in all places, wherever you go."

Pamoja na Mathew 4:4 " Man shall not leave by bread alone but by every word that proceeds out of the mouth of God."


Kwa hiyo tutafute mkate kwa jitihada zote lakini tujiwekee mipaka ya kuwa furaha na afya zetu haziwezi kuwekwa rehani kwa ajili ya kuukwaa mkate tu.....................ujumbe huu ni kumbukumbu ya simanzi ya wote wale ambao maisha yao yalikatishwa kabla ya muda wake uliopangwa kwa sababu ya kuijali hii dunia na maruerue yake yote........kupita kiasi.......Let us all be Blessed in the name of the LORD...........
 
Thanks, kama niko kanisani vile!

yaani wacha tu......................niko kwenye simanzi kubwa...................an old flame -that flickered out longtime ago- has passed away tonight..............she dedicated her life on seeking for greater earthly things for herself....................she got them in many ways.........she was an envy of many too, but today I am looking for her and she is nowhere to be seen for GOD has took her away because of her recklessness.......
 
Ubarikiwe kaka kwa maneno haya yenye hekima na yanayofikirisha............... .....

Tukiishi kwa kipimo tutafaidi hii dunia...............lakini tukiwa walafi tutachongewa majeneza kabla ya muda wetu.....................it is a pity with this reckless generation how it is squandering it all for a day of sipping honey and milk...........which 2morrow is not there for a toilet has taken it away.........
 

Ubarikiwe kwa ushauri na kwa NENO.
 
Ubarikiwe kwa ushauri na kwa NENO.

Mkate hatukatai ni mtamu sana lakini afya zetu, furaha yetu na utu wetu kamwe hakuna wa kutupatia..........hivyo tusiwapatie wengine nafasi ya kutudhulumu hizi bidhaa adimu........lol
 
Ruta una busara sana.

Oh Husniyo..........you are killing me softly....................thanks a lot..............just stating facts of life which we often overlook at our own peril..................
 
So be it...thank you and be blessed too!
 
Mungu akubariki kwa ujumbe wako, umenibariki sana, endelea kutupa neno, kwani neno ni chakula cha uzima.
 
Mungu akubariki kwa ujumbe wako, umenibariki sana, endelea kutupa neno, kwani neno ni chakula cha uzima.

busara ni kutambua mipaka ya kila kitu kuwa kuna hasi na chanya zake.................ukizikodolea chanya tu na kusahau hasi ujue umekwisha ingawaje unatembea...................1 TIMOTHY 5:6 But she who lives in pleasure is dead while she lives.............................scary message don't you think so?
 
Ubarikiwe kaka kwa maneno haya yenye hekima na yanayofikirisha............... .....

wakati mwingine tunahitaji chemsha bongo kuchangamka..........
 
asante sana kaka education is anywhere, anytime!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…