Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Sijui ni kwa nini haturidhiki na kidogo ambacho tulichonacho na hata kudiriki kukikashifu kuwa hakina umaana wowote ule wakati tunacho. Sasa unapokuwa umenyang'anywa ndipo unatambua kuwa kumbe khali yako ilikuwa ni bukheri sana bila ya wewe kujitambua.........na kukumbuka neema nyingi ambazo Mwenyezi Mungu alikushushia lakini wewe hukuona na hivyo kudharau.
Tujifunze kuthamini kidogo tulichonacho kwa sababu kuna sababu ambazo Mwenyezi Mungu ameona ndicho kinachotutosha ili tuishi kwa amani na furaha humu duniani. Utakapoanza kufukuzia makubwa ndipo utakapoweka rehani afya yako, usalama wako, utu wako na hata mengineyo ambayo........kwa hiyo mihangaiko, tunakuwa sawa na mtoto ambaye analilia wembe na Mwenyezi Mungu kwa majonzi na masikitiko makubwa huamuru malaika zake tupewe huku akijua ya kuwa hicho kiu cha makubwa kitakuletea kiama chako.
Soma Jeremiah 45:5 kwa elimu ya ziada............." And do you seek great things for yourself? Do no seek them; for behold, I will bring adversity on all flesh," Says the LORD, "But I will give your life to you as prize in all places, wherever you go."
Pamoja na Mathew 4:4 " Man shall not leave by bread alone but by every word that proceeds out of the mouth of God."
Kwa hiyo tutafute mkate kwa jitihada zote lakini tujiwekee mipaka ya kuwa furaha na afya zetu haziwezi kuwekwa rehani kwa ajili ya kuukwaa mkate tu.....................ujumbe huu ni kumbukumbu ya simanzi ya wote wale ambao maisha yao yalikatishwa kabla ya muda wake uliopangwa kwa sababu ya kuijali hii dunia na maruerue yake yote........kupita kiasi.......Let us all be Blessed in the name of the LORD...........