Naomba nikiri mimi ni Mwanachama wa Simba na nilishwahi kufanya kazi kwenye moja ya makampuni ya huyu anayejiita YOUNG BILLIONAIRE (si lolote si chochote).
Niliwahi fanya kwenye kampuni ya 21st CENTURY ,kisha mkataba wangu ukaamishiwa kampuni la EAST COAST akaniamishia tena mkataba wangu kwenye kampuni ya ROYAL DETERGENTS kote huko lengo ni kupunja maslahi yangu ajira ya mwanzoni
Kwa msiomjua Mo -Dewji na hujawahi kufanya kazi kwenye makampuni yake au kwenye taasisi zake unaweza kumlaumu Mzungu na unaweza kupuuza yale malalamiko ya Haji Manara wakati alipolalamika alivyofanya kazi na Bw.Mo
Kwa kifupi Mo-Dewji ni mnyanyasaji mkubwa wa wafanyakazi wake na mtu asiyefuata sheria za mikataba ya kazi.
Kwa makampuni ya Mo uwa hafukuzi wafanyakazi pale anapokuchoka anatumia watendaji wake kuanzisha hila na chokochoko ili uondoke mwenyewe na aminye haki zako za msingi.!
Limenitokea mimi, limemtokea Haji Manara na linamtokea mzungu.
Kwanza siku Manara aliposema alikuwa analipwa 700k nilishangaa sana mimi kumzidi mshahara, nilikuwa nalipwa 800k Kwa,Mwezi.
Yaani mimi wa kumzidi Manara mshahara wakati,Manara alifanya kazi Closed na Bwana Mo-Dewji.
Mshahara wangu ulishuka kutoka 1.5m mpaka 750k,kila nilipoamishiwa kampuni na kuanza upya mkataba wa ajira,nilishtuka nikaondoka kwa style ya MZUNGU.
KUHUSU KUCHANJWA MZUNGU.
Sina hakika kama ameongea hivyo.KAMA NI KWELI alisema hayo,sishangai,kwani hata mimi wakati nafanya kwa Bw.Mo ,ilikuwa ni kawaida kuvunjwa nazi viwandani zenye maandishi ya kiarabu na tulilishwa vipande hivyo vya nazi.
.
Na ilikuwa ni LAZIMA ukikataa huna kazi au alichinjwa Mwanakondoo kwenye geti kuu la viwanda na nyama tuligawiwa.!
Kwa hiyo yote kwa yote yanawezekana.