Anatafutwa: Ted Kennedy wa Tanzania!

Anatafutwa: Ted Kennedy wa Tanzania!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
4,526
Reaction score
1,540
Wasifu mkubwa wa Ted Kennedy ni Utungaji sheria, kupigania maslahi ya walalahoi, na kubwa ni kitendo chake cha kugombea kuchaguliwa kuwa mgombea wa Uraisi akiwakilishe chama cha Democrats akipingana na aliyekuwa Rais wa Marekani Jimmy Carter ambaye alikuwa naye ni Democrat.

Je tunaweza kuona kitu kama hichi ndani ya CCM?

Je kitendo cha Zitto kugombea uenyekiti kupingana na Mwenyekiti wake tutakiweka sawa na cha Kennedy kupingana na Carter?
 
Sijui kama atapatikana hivi karibuni, ingawa naweza kusema walikuwapo zamani, nao hawakuishi maisha marefu. Tatizo la kwetu wanasiasa wengi wanaingia kwenye siasa wakiwa na nia ya kuwa matajiri, na "celebrities", na sio kwa dhumuni hasa la kutetea maslahi ya mnyoge, mwanakijiji ambaye hana mtu wakumsemea. Watu kama Kennedy, waliingia kwenye siasa kama wito na sio utajiri maana tayari familia yao ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha, hilo la kwanza.

Pili, wapo wanaojaribu kugombea nafasi hizi za juu, kama ambavyo tumeona, lakini wanashawishiwa kutoa majina yao kwenye list ya candidates. Lazima pia tutambue kwamba utamaduni wetu ni tofauti na wawazungu na kwa maoni yangu, kwa sababu ya hili (utamaduni) haliweza kutokea mara kwa mara. Kama watu wanasikilizana na kuamua kutogombea nafasi za juu kwa hiari yao ni vema sana. Mambo yalitokea Chicago kwenye hio democrat convention mwaka 1980 yalikuwa na athari kubwa sana kwa chama cha Democrat na nchi nzima, hata uhasama ambao uliendelea kichinichini kati ya mzee Carter na marehemu Ted, mpaka leo hii (mzee Carter akiri mwenyewe, juzi alipohojiwa na CNN).

Kwa kifupi, akijatokea mwanasiasa mtanzania atakaye simamia haki ya wananchi wanyonge, ambaye hana hidden agenda, ila hii moja tu, ya kusaidia watanzania, itakuwa siku ya kumshukuru Mungu sana.
 
Yah ryt Bro! Tanzania will tek long tym 4 tht to happen...
 
Rev. Kishoka,

Na wewe ni matheory tu ya Wamarekani kila siku huku nyumbani watu hata kula kunawashinda.

Vijana wenzenu wakitokea kugombea mnawapiga vita; sasa mnafikiri huyo mtu atatoka wapi?

Kennedy hakuwa clean kwa matendo yake kama kijana lakini moyoni alikuwa mtu mzuri na alipopata nafasi akabadilika na kuwa mzuri katika matendo mpaka hapo alipofikia.

Njooni nyumbani muje muanze na A, B, C badala ya kuhubiri mambo ya Marekani tu ambayo kwa kweli kwa huku nyumbani ni ndoto tu.

Kinachonisikitisha nyie wasomi wetu na mlio kaa majuu ni WIVU wa KIKE ambao wengi wenu mnao. Mkiona mwenzenu mmoja anataka kufanya la maana mnaanza kuleta mambo ambayo hayana maana kabisa. Sababu kubwa inakuwa wivu; kama jambo huwezi kufanya wewe, akifanya mwingine ni WIVU tu.

Wivu ndio unatufanya vijana hata tushindwe kusaidiana na kuaminiana na matokeo yake wote tunaganga njaa pale pale tu.

Samahani kama nimetumia lugha mbaya lakini mambo mengine yanaudhi. Leo hii tunajadili mambo ya Zitto, wale mabingwa wa theories za demokrasia mko wapi? Mnaanza kuhalalisha au kukaa kimya. Kwenye suala la Mwakalinga nyie wenyewe ndio mlikuwa vinara wa kumchafua huku mnajua kabisa he is a good man. Wengine wakakaa kimya kama hawaoni. Jamaa yangu mmoja akasema hao wangependa hayo anayofanya Mwakalinga kwao wao ndio wangefanya, hapo ungewaona vichwa juu juu.

Inabidi kuwaunga mkono watu kama akina Zitto; ndio kuna wakati watafanya makosa mengi maana hakuna asiyefanya makosa. Lakini angalia dhamira ya Zitto ni nzuri na ameonyesha mfano. Sisi tunakuja kumchafua hapa JF bila sababu za msingi kabisa.

Mnataka hao wa kuibadili CCM au Tanzania watoke wapi?
 
Sijui kama tunahitaji supporter wa abortion clinics kwa kisingizio cha rights of women to choose and same sex marriage Tanzania - simply ni abomination
 
Sijui kama tunahitaji supporter wa abortion clinics kwa kisingizio cha rights of women choose and same sex marriage Tanzania - simply ni abomination

Tanzania tunahitaji transformational figure kama Ronald Reagan....siyo maliberali kama huyo Kennedy
 
Rev.Kishoka,

..familia ya kina Kennedy walikuwa wanapenda sana madaraka.

..kwa maoni yangu walihusika kuwahujumu Lyndon Johnson na Jimmy Carter kwa mambo ya kibinafsi na kupenda madaraka.

..Ted Kennedy alikuwa anajua kabisa kwamba alikuwa hawezi kumtoa Jimmy Carter who was a sitting President, lakini akalazimisha kugombea na kukihujumu chama.

..Jimmy Carter alishindwa uchaguzi na Ronald Reagan, ambaye alikuwa mkatili sana kwa nchi za Kiafrika haswa zilizofuata siasa za Ujamaa kama Msumbiji na Angola. pia Reagan ndiyo aliyewafadhili Mujahedeen[wasoviet walikuwa wawamalize hawa] ambao baadaye wakahitimu na kuwa Taliban na Al-Qaeda.

NB:

..zile hotuba zake moto-moto zilikuwa zinatayarishwa na jamaa anaitwa Bob Shrum "the word smith of the kennedy's family."

..pia nimeona TED KENNEDY naye alikuwa akitumia TELEPROMPTER. kumbe teknolojia hiyo imekuwepo tangu miaka ya 1980.
 
Last edited:
..pia nimeona TED KENNEDY naye alikuwa akitumia TELEPROMPTER. kumbe teknolojia hiyo imekuwepo tangu miaka ya 1980.

Joka na wewe bana...yaani ulikuwa hujui kuwa prompter ziko mrefu? Wewe ulidhani Obama ndio kazivumbua nini? Aahahahahaha...wewe utakuwa umenyweshwa kool-aid ya Obama wewe
 
Nyani Ngabu,

..unajua nimekutana na watu wenye elimu na madaraka makubwa serikalini na wanaamini kwamba Obama zile hotuba zote zinamtoka kichwani.

..sasa tangu hapo nikaanza kuwa makini sana. kila nikiangalia speech natafuta teleprompter iko wapi.

..sasa kwenye ile hotuba "the dream shall never die" ya Ted Kennedy inabidi uwe makini kidogo kugundua kuwa kulikuwa na telepromter pale.

NB:

..pamoja na hayo lazima ujue kuitumia teleprompter na jinsi ya ku-pose.

..ukiwa hujui kusoma vizuri kama Sarah Palin teleprompter haiwezi kukusaidia sana.
 
Nyani Ngabu,

..unajua nimekutana na watu wenye elimu na madaraka makubwa serikalini na wanaamini kwamba Obama zile hotuba zote zinamtoka kichwani.

..sasa tangu hapo nikaanza kuwa makini sana. kila nikiangalia speech natafuta teleprompter iko wapi.

..sasa kwenye ile hotuba "the dream shall never die" ya Ted Kennedy inabidi uwe makini kidogo kugundua kuwa kulikuwa na telepromter pale.

NB:

..pamoja na hayo lazima ujue kuitumia teleprompter na jinsi ya ku-pose.

..ukiwa hujui kusoma vizuri kama Sarah Palin teleprompter haiwezi kukusaidia sana.

Wow! Just wow! Lakini unachosema ni kweli. Kwa viongozi wetu hasa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, sishangai hata kidogo kama wakidhania Obama huwaga anatema off the top of the dome.

Mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kutema ni MLK bana. Jamaa alikuwa ni kichwa kwelikweli. I really admire him.
 
Nyani Ngabu,

..unajua nimekutana na watu wenye elimu na madaraka makubwa serikalini na wanaamini kwamba Obama zile hotuba zote zinamtoka kichwani.

..sasa tangu hapo nikaanza kuwa makini sana. kila nikiangalia speech natafuta teleprompter iko wapi.

..sasa kwenye ile hotuba "the dream shall never die" ya Ted Kennedy inabidi uwe makini kidogo kugundua kuwa kulikuwa na telepromter pale.

NB:

..pamoja na hayo lazima ujue kuitumia teleprompter na jinsi ya ku-pose.

..ukiwa hujui kusoma vizuri kama Sarah Palin teleprompter haiwezi kukusaidia sana.

bahati yako hajui kiswahili!
 
Rev. Kishoka,

Na wewe ni matheory tu ya Wamarekani kila siku huku nyumbani watu hata kula kunawashinda.

Vijana wenzenu wakitokea kugombea mnawapiga vita; sasa mnafikiri huyo mtu atatoka wapi?

Kennedy hakuwa clean kwa matendo yake kama kijana lakini moyoni alikuwa mtu mzuri na alipopata nafasi akabadilika na kuwa mzuri katika matendo mpaka hapo alipofikia.

Njooni nyumbani muje muanze na A, B, C badala ya kuhubiri mambo ya Marekani tu ambayo kwa kweli kwa huku nyumbani ni ndoto tu.

Kinachonisikitisha nyie wasomi wetu na mlio kaa majuu ni WIVU wa KIKE ambao wengi wenu mnao. Mkiona mwenzenu mmoja anataka kufanya la maana mnaanza kuleta mambo ambayo hayana maana kabisa. Sababu kubwa inakuwa wivu; kama jambo huwezi kufanya wewe, akifanya mwingine ni WIVU tu.

Wivu ndio unatufanya vijana hata tushindwe kusaidiana na kuaminiana na matokeo yake wote tunaganga njaa pale pale tu.

Samahani kama nimetumia lugha mbaya lakini mambo mengine yanaudhi. Leo hii tunajadili mambo ya Zitto, wale mabingwa wa theories za demokrasia mko wapi? Mnaanza kuhalalisha au kukaa kimya. Kwenye suala la Mwakalinga nyie wenyewe ndio mlikuwa vinara wa kumchafua huku mnajua kabisa he is a good man. Wengine wakakaa kimya kama hawaoni. Jamaa yangu mmoja akasema hao wangependa hayo anayofanya Mwakalinga kwao wao ndio wangefanya, hapo ungewaona vichwa juu juu.

Inabidi kuwaunga mkono watu kama akina Zitto; ndio kuna wakati watafanya makosa mengi maana hakuna asiyefanya makosa. Lakini angalia dhamira ya Zitto ni nzuri na ameonyesha mfano. Sisi tunakuja kumchafua hapa JF bila sababu za msingi kabisa.

Mnataka hao wa kuibadili CCM au Tanzania watoke wapi?

Bambumbile,

Sikumleta Ted Kennedy ili tuchangue Ujana wake wala matendo yake akiwa kijana. Kila binaadamu, kadri anavyokuwa ndivyo anavyozidi kupevuka.

Ila kuna tofauti sana ya wale ambao hupatiwa ushauri nao wakaukataa, na wale wanakaa chini na kutafakari ushauri waliopewa, kisha kuufanyia kazi.

Umekuja kwa ghadhabu nyingi sana na ukali na hata umekosa mwelekeo wa kujenga hoja yako.

Kwanza unanishambulia kwa kuwa nina theory za Wamarekani na watu Tanznaia wanashindwa kula. Je Tanzania haikujengwa kwa theory?

Je tulipoachwa na Mkoloni si tayari Demokrasia iliyoko Marekani na Uingereza leo hii, ilikuwepo Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Japani na nchi zote zilizoendelea na zenye Uchumi imara na Demokrasia? Kilitushinda nini kujenga mfumo mzuri wa Kisiasa na Kiungozi ili badala ya kurudi nyuma, tungeendelea kupiga hatua mbele na kurekebisha makovu ya Ukoloni?

Je Vyama vya Siasa na Uchaguzi wa wakilishi tulivitoa wapi? kama hazikuwa theory za Marekani na Uingereza au Wagiriki ambazo zilishakuwa practical kwa miaka zaidi ya 150 siku tulipopata Uhuru? Kwa nini basi alikuwepo Mtemvu na Chama chake tulikimbilia kumtwez na kumfananisha na Mkoloni kaa si Msaliti kwa kuwa yeye hakuwa TAA/TANU?

Je tulipokumbatia theory za Mashariki, UChina, Urusi na mkorogo kati ya Ukomunisti na Ujamaa, mbona hukupiga kelele kulalamika bali uliandamana kuunga mkono Azimio la Arusha?

Kama watu hawana uwezo wa Kula na wanakufa njaa, linahusianaje na Mchungaji au kumtafuta Maverick kama Kenndy au McCain Tanzania?

Ukosefu wa Chakula ni kutokana na sababu mbili kubwa, ya kwanza ni ya binafsi ya anayeshinda njaa ambayo inatokana na Uvivu, Uzembe, Utegemezi na Ujuvi. Sababu ya pili ambayo ndiyo wengi wanaikimbilia kuhalalisha umasikini na njaa Tanzania ni Serikali, Mvua, Soko, Ajira na Kipato.

Sasa kama Mnyaturu na ardhi yote aliyonayo, yeye kazi yake ni kutega panzi na kulima hataki wakati kuna mvua, kinapokuja kiangazi ile robo heka yake ya mtama ikanyauka, kwa nini ilaumiwe Serikali au Mchungaji Kishoka?

Sina Wivu wa Kike, wala wa Kiume. Wivu ni wivu na sina wivu na mtu yeyote kwa sababu yeyote kwa kwa lolote. Simuonei gere mtu yeyote awe kaufuma, kapata au hanazo, wote ni sawa kwandu. Simtegemei mtu aninunulie Bofulo na yule anayekula chapati maji kila siku asubuhi na mayai ya kukaanga hiyo ni staha yake na sioni wivu kwa maana mimi mhogo wa kukaanga ndiyo chapati maji yangu.

Zitto kugombea Uwenyekiti, Mwakalinga kugombea Ubunge viweje viwe ni vitendo vinavyonikera? Si uamuzi wao binafsi na kwa manufaa yao na mtazamo wao, au kinacho kutatiza na hata kudai tuna Wivu wa Kike ni kile cha kawaida kumhoji mtu nia yake ya kuwa mwakilishi? Mbona Kikwete, Lipumba, Nape, Lowassa nao waliulizwa kwa nini wanataka uongozi?

Nikianza na Mwakalinga, ni wapi nilipomkashifu au kumbeza Mwakalinga? Kibinafsi nilimuuliza Mwakalinga masuali yafuatayo ninayo yanukuu hapa
What is your vision for Kyela and how will you bring change
and development in Kyela in contrast to Kasyupa to even Latter Day "Chief" Mwakyembe?

On your plan, what part will Kyela play to rebuild our nations economic, political and social development?

Kisha kabla ya CHADEMA kuboronga na kuonyesha hawafai kutuongoza nikamuuliza kwa nini aliamua kwenda CCM na si TLP, CUF au chama chochote cha Upinzani na si CCM

Bwana Ambwene wa Mwakalinga,

Kama Spika ambaye ni mhimili mmoja mkuu wa Serikali anadhalilishwa namna hii kuhusu kutumia kanuni za Kibunge ambazo ndio zanazotumika kuongoza Bunge na si katiba ya CCM, tukuelewe vipi unapong'ang'ania kusema utaweza kuwatumikia Wanakyela vema ikiwa CCM inashurtisha watu walinde maslahi ya Chama na si maslahi ya Taifa?

Huoni kama umefanya kosa kuingia chama kisichokuwa na nidhamu kwa Katiba ya Tanzania?

Mwakalinga akanijibu
Rev,

Kuchapa kazi na malumbano ya kisiasa ni vitu viwili tofauti. Sisemi CCM ni safi, lakini je alternative yake ni nini? Wengine tumesubiri kuwa na wagombea huru bila mafanikio.

Binafsi nina malengo yangu ambayo ndiyo yananipeleka kwenye siasa na ninaamini ninaweza kuyatimiza mengi kwa faida ya wana Kyela hata nikiwa ndani ya CCM hiyo hiyo. In fact kuna mengine tumekuwa tukifanya hata sasa bila kuingiliwa na wanasiasa. Changes zozote za maana zinaanzia chini na ndizo hudumu vinginevyo inabidi kufanya mapinduzi.

Pia Sitta na kundi lake walishindwa vita pale walipoamua kutumia vita dhidi ya ufisadi kama mtaji wa kisiasa. Katika mapambano yoyote fairness ni kitu muhimu mno. Lakini ukishindwa kuwa fair kwa watu wanaokupinga juwa na wenyewe hawatakuwa fair ukiwekwa kwenye kikaango. Wao waliamua kwa makusudi mazima kwamba kila anayewapinga kisiasa lazima wamlink na mafisadi na wamefanikiwa sana kwa hilo.

Wengine tumeonja makali ya hilo kundi la Sitta, tuna hata video ya baadhi ya hotuba zao. Inasikitisha tena sio kidogo. Inanikumbusha mwanzo wa mauaji ya Rwanda ni wanasiasa kueneza uwongo ambao si ajabu hata wenyewe wanajua ni uwongo. Kule Northern Ireland, watu walizua tu kwamba kuna msichana kawa raped; watu wakauana. Inapotokea wasomi wanatumia hizo tactics inakuwa hata ni hatari zaidi.


Hii dhana ya you are either with us or with the terrorists ilimshinda hata Bush ndio wawe akina Sitta?

Dunia hii wengine tunakuwa washangiliaji wa mpambano mpaka tunapogundua mpambano wenyewe umefika milangoni kwetu. Unapoona mtu anapohutubia watu tena bila woga hata kidogo, bila ushahidi hata chembe moja, akikutuhumu kupewa milioni 400 na mafisadi; hapo ndio unajua mpambano umefika nyumbani kwako. Unaanza kujiuliza, kama wanaweza kuwa very wrong kwa tuhuma dhidi yako, je vipi hao wengine wanaowatuhumu?

Binafsi naamini hapo ndipo walipopotoka; kuanza kumwita kila mtu ambaye hakubaliani nao kwamba ni fisadi, anatumiwa na akina Lowassa nk. Ndio maana hii vita na mafisadi itakuwa ngumu kuishinda maana askari wanaoongoza vita wanarusha risasi kila upande na kuua mbu na inzi badala ya nduli.

GAM

Nami nikamjibu

GAM,

Nashukuru sana kwa neno kubwa uliloliweka hapa ambalo nanukuu 'Wengine tumesubiri kuwa na wagombea huru bila mafanikio.

This answers alot of thousand questions kwa nini ulijiunga CCM.

Lakini hata hivyo, kwani CUF na CHADEMA vina ubaya gani? Mbona Zitto, Hamad, Slaa na hata Mzee Mapesa wako upinzani na wamo Bungeni?

Je sauti ya nyikani ya Mwakalinga kama ingetokea CHADEMA, CUF au hata UDP zje isingesikika kwa Wanakyela?

Je ni CCM pekee ndiyo yenye uwezo wa kukufikisha "Darini" uanze kuwatumikia WanaKyela?

Je WanaKyela wamekula yamini ya CCM kupita kiasi kuwa wanafumbia macho uozo wa CCM na kushindwa kuchagua chama kingine? Maana kama wameshindwa kumwajibisha Mwakyembe kwa kudai maendeleo ya kweli na si porojo zake za kila siku za kutafuta umaarufu, mtu aliye na utashi mkubwa na mvuto kitaifa, watawezaje basi kudai maendeleo kutoka kwa mtu mwingine kupitia cham kile kile cha Kasyupa na Mwakyembe?

Sikudhamiria kuhoji suala la kukimbilia majukwaa na kutoa hotuba, baali ni ukweli kuwa ndani ya CCM, maslahi ya Chama ni ya kwanza na si Maendeleo ya Taifa.

Kama CCM ingekuwa na mtazamo na kuwa na mkazo wa kulijenga Taifa na kuwaachia Wabunge wake wafanye kazi za kujenga majimbo yao kimaendeleo na si kueneza imani na enzi ya chama, wala nisingelifikiria mara mbili kwa nini GAM kaenda CCM.

Sikujihusisha na upuuzi uliokuwa humu ndani JF kuhusiana na Mwakalinga na Mwakyembe kwa kuwa tayari mjadala ulishakosa mwelekeo. Wengiwa wana JF wana imani na "Pimbi" Mwakyembe kuwa ni shujaa kutokana na kitu kimoja tu, Richmond, lakini ilipojulikana kuwa Mwakyembe naye ana kampuni yake ya kufua umeme na huku ni Mwanakamati ya Nishati ya BUnge tukasema kakosea kufanya hilo, ndipo sura ya JF ilipoonekana kuwa wamekula kiapo kwa Mtu na si kumpima matendo yake.

La Zitto, nitalipambanua kwa namna mbili. Kwanza, Zitto alikuwa anataka kugombea Uenyekiti, lakini hajawahi kusema ni vipi alipingana na Mwenyekiti wake na ni vipi ataleta mageuzi Chadema tofauti na Mbowe. Binafsi nilichopigia kelele na kutahamaki ni mchakato mzima wa yeye kutangaza kugombea na hata kuamua kujitoa na nilisema kuwa amefanya kitendo cha Kitoto.

Najinukuu
Nasikitika kusema kuwa kilichotokea ni utoto wa hali ya juu na kukosekana kwa busara kutoka kwa Wazee wa Chadema, Freeman na Zitto mwenyewe.

Kwanza sielewi na hakuleti maana kusikia kuwa Zitto alichukua fomu na kutangaza nia yake ya kugombea Uenyekiti akiwa njiani kwenda Ujerumani. Kama hiki kitendo ni cha kweli, basi kilikuwa cha Kitoto sana na cha kipuuzi ambacho kinaonyesha woga.

Ama baada ya nia yake ya kugombea kujulikana na mkutano mkuu kuanza, kitendo cha yeye kukubali kuwekwa kikaoni na kukimbilia kutoa masharti ambayo tunayasoma humu kama ndio nji pekee ya yeye kusimama mguu pande ni kweli, basi Zitto na Chadema hawafai kupewa dhamana ya kuliongoza Taifa letu.

Mbowe ilisadikika kuwa hatarejea kwenye Uenyekiti, ni kwa nini basi aliamua kubadilisha mawazo na kugombea?

Kilichotokea CHADEMA ni kunyongwa kwa Demokrasia na udhaifu wa kuelewa njia bora ya kujenga chama cha kisiasa.

Chadema na Zitto wamejidhihirisha kwa Watanzania kuwa bado ni watoto sana katika masuala ya siasa na wamejiunga na kundi la TLP, NCCR na vyama vingine ambavyo vimekuwa na migogoro ya kiuongozi na ubinafsi.

Kama kulikuwa na mtu anayetegemea kuwa CHADEMA ni chama madhubuti cha Upinzani, naomba urudie makala zangu za CHADEMA must Reform na Focus 2010!

Zitto alijua wazi tangu mwanzo kuwa kitendo cha yeye kugombea kingeleta vurugu na kukosesha amani chama.

Wazee wa CHadema na Freeman, nao waliposikia hili, kwa nini hawakumpisha Zitto awe mwenyekiti wa Chama kwa kuwa Freeman Mbowe ilishasikika kuwa atastaafu?

Mambo yaliyotokea CHADEMA katika siku hizi 5 zilizopita, yanayapa nguvu yale maneno ya mtaani yanayodai kuwa kuna watu waliotaka kuingia CHADEMA kutoka CCM ambao si safi na walitaka mtu kama Zitto ambaye ni mwepesi wa ku-compromise, awe Mwenyekiti ili yanayosemwa mtaani kuhusu hawa jamaa, yaishe kimya kimya.

Si mara ya kwanza kwa Zitto kutuhumiwa kuwa anatumiwa na kikundi fulani ndani ya CCM.

Yalianza na kamati ya madini, ikaja suala la Dowans, na kila panapokuwa na tuhuma za Zitto kutumiwa kama kibaraka wa CCM na ajenda zake, si Zitto au CHADEMA ambao wamesimaam kidete na kuondoa huo utata, kitu kinachoonekana wazi kuwa tuhuma hizo ama zina ukweli au basi kuna vurugu ndani ya Chama kama vile Chacha Wangwe alivyodai kuwa Zitto adandie basi la CCM aachane na la Chadema!

Kura na heshima yangu mmeipoteza, nyote CHADEMA na Zitto sawa na vile CCM ilivyojiharibia machoni pangu.

Sasa kama kuhoji mtu ni Wivu wa Kike, basi tukubali kutokukubaliana.

Nimeleta mfano wa Kenndy nikiwa nimekilenga Chama cha Mapinduzi na zaidi nikiwa nimelenga hili kundi linalojiita la Wapiganaji ndani ya CCM.

Uchaguzi Mkuu unakuja mwakani na CCM inatafuta mgombea URais, kama kina Mwakyembe, Seleli, Kimaro, Kilango wanaona kuwa Uzalendo wao unavunjwa nguvu kutokana na Rais kutokuwa Imara, kwa nini basi nao wasiwe kama Kennedy na kugombea ndani ya CCM ili wachaguliwe kuwa Mgombea Urais kupitia CCM?

Na wao wakichukua fomu, nitawauliza Maswali yale yale niliomuliza Mwakalinga na wakilazimishwa wajitoe ili Kikwete awe mtu pekee CCM, nami nitawakung'uta kwa nilichosema kuhusu Zitto na Chadema.

Tanzania itajengwa na wote, walioko ndani ya nchi na walioko nje ya nchi. Si lazima wote tuwe Dar Es Salaam, Dodoma au Unguja. Tunaweza kuwa kila kona ya nchi hii.

Si lazima wote tuwe Wanasiasa, Wabunge au Rais ili kuleta maendeleo, tunaweza kuwa Waalimu, Wakulima, Wavuvi, Wahasibu, Machinga, tukiwa kila kona ya Dunia.
 
Inawezekana akapatikana kabisa na pia kuna makosa mengi kama vile binadamu wakawaida kufany kwa wanasiasa kama wakina Zitto lakini wana nafasi kubwa sana katika kufanya na kuweka historia. Kwa CCM labda wote watoke ndani ya CCM ndio wanaweza kusimamia ukweli kwa uhuru wote bila ya kuficha
 
Back
Top Bottom