Anataka kukata rufaa

Anataka kukata rufaa

rosita

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2013
Posts
509
Reaction score
469
Habarini wadau wa sheria
Ni kesi ya kiwanja na waliokabidhiana wote ni marehemu...walikabidhiana kwa maandishi miaka ishirini na tano iliyopita but hilo karatasi lilichukuliwa na mke wa marehemu kwa kisingizio cha kumsaidia mama kisheria kubadili jina pale mama alipoanza process za kubadili jina la kiwanja ..na mama yangu alimwamini coz alikiwa ni family frnd na baadae kuja kugeuka kuwa mama yangu ambae alikuwa ni mhasibu wa mume wake aliiba nyaraka za nyumba za mume wake zilipokuwa ofisini na akafungua kesi ya jinai...bahati nzuri kesi ilitupiliwa mbali baada ya kukosa ushahidi wa kutosha kwa upande wa mashtaka na hivyo mama hakuwa na kesi ya kujibu...

Yule mke wa marehemu akafungua kesi ya madai mahakama ya ardhi baada ya kuona kule ameshindwa napo ikatupiliwa mbali since kiwanja kimetolewa miaka 25 iliyopita na alikuwa anaona kilipo jengwa na kuendelezwa na hakuwa na ground za kufungua kesi....hivyo basi kesi ikaisha 2011...

Mwaka jana tunataka kubadili jina na ardhi wakataka kikaza hukumu...wakati zoezi linaendelea huyo mama anarudi na kuomba mahakama kukata rufaa na kuleta medical forms kuwa alikuwa mgonjwa so hakuweza kukata rufaa...miaka mitatu umeshapita tangu kesi iishe na hakukata rufaa na anataka kukata rufaa now baada ya kujua jina linataka kubadilishwa kwa ground hiyo niliyotoa...sasa hapo wadau imekaaje kisheria coz kwa uelewa wangu finyu wa sheria najua haki ya kukata rufaa ina time limit....pls naomba mnisaidie.
 
Sijaelewa kitu, kesi iliisha 2001 sio?
Mama yako ndie alishinda kesi ama mke wa marehemu?
 
Mama ndiye aliyeshinda kesi zote
 
Anapaswa kupeleka kwanza maombi ya kuomba kuwasilisha rufaa yake nje ya muda, rufaa hiyo isikilizwe kwanza kisha ikiwa mahakama itaona sababu zake ni za msingi itamruhusu kuwasilisha rufaa hiyo. Ikiona sababu zake hazijitoshelezi basi itatupilia mbali maombi hayo na hataweza tena kukata rufaa.
 
Back
Top Bottom