Anataka kunua gari lakini Chassis Number yake haionekani

upeo

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2013
Posts
369
Reaction score
218
Wakuu naomba msaada kuna rafiki yangu anataka kununua gari, bahati mbaya hiyo gari chasiis yake hajaonekana, kwa kile kibati kinachoonesha kila kitu kinachokaa pembezoni mwa mlango wa dereva kimefutika chote, hata kwenye mkanda wa dereva hakuna.

Swali langu je ni sehemu gani nyengine kwenye basi hilo la mistubish rosa itaonekana hizo number chassis?

Nitashukuru sana wakuu mkinipa msaada huo kwani jamaa kesha toa pesa nusu, chaka ipo hapo asanteni.
 
Kwenye Card ya Gari TRA kwa kuangalia namba ya gari na information zake. Nenda TRA peleka namba ya gari hilo watakupa chassis namba.
 
Wao waliposajili wali verify vipi kuwa hiyo ndo chassis number? Tumia tu kigezo hicho.kuwa kama mpaka walisajili basi hilo gari walithibitisha ndo lenyewe.

But again nenda katoe taarifa polisi kuwa unataka kununua gari xxx lenye usajili huo na chassis namba inayosoma hiyo halafu wakushauri.na unaponunua fuata taratibu zote za kuuziana kitu na mtu.

Wakishakupa utaverify vipi kuwa chassis number hiyo ndo gari hilo?
 
Mkuu huyu jamaa mpaka kajakupost huku tayari atakua anawasiwasi kuwa namba iliopo kwenye kadi sio namba ya gari hilo lililoletwa, kwa hiyo anataka kutafuta hiyo namba physically ili awe na amani.

Ushauri wako wa kwenda polisi unaweza ukawa sahihi zaidi, maana unaweza kukuta hilo gari ni la wizi na wameisugua hiyo vin makusudi.
Ingekua gari dogo nimemwambia afungue mbele chini ya kioo kwenye njia ya maji ya mvua kuna sehemu akitoa angeiona.
Ila kwa gari lake hilo sidhani kama ipo hapo pia
 
Naam sawa sawa unavyosema nina waswas na hili gari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…