Anataka nimdhamini au wakala wa Bank, je, kuna tatizo?

Anataka nimdhamini au wakala wa Bank, je, kuna tatizo?

Mzee wa old school

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
873
Reaction score
1,405
Habarini,

Naomba kuuliza kwa wajuvi wa mambo ya uwakala wa Bank mfano kama CRDB, NMB n.k,

Kuna jamaa namfahamu anajishughulisha na Tigo Pesa na M-Pesa, akajiongeza na kwenda kuomba kuwa wakala wa Bank, akapewa fomu na baadhi sehemu zinahitaji udhamini hivyo akaomba nimdhamini kwaa ajili ya hiyo.

Hivyo nina wasiwasi juu ya hilo, naomba mnipe elimu kidogo juu ya hilo.

Naamini nitafahamishwa vyema.

Nawasilisha.
 
Heading sikuielewa Ila mada nimeielewa, mdhamini tu haina shida yoyote, au nenda benki husika kawaulize majanga anayoweza kukutana nayo mdhamini
 
Udhamini ni kwasababu ya zile mashine tu hakuna cha ziada kwasababu bank hawampatii fedha bali wanampatia mashine tu.
Tena mashine zenyewe hapati bure, mfano crdb ni jiwe3 non refundable hata wakija kupora mashine yao
 
Mdhamini tu haina shida kabisa, hata me nilidhaminiwa na mtu ambaye tumejuana kwenye biashara, alikuwa mteja wangu tu.

Mpaka Leo napiga kazi kama kawaida .
 
Back
Top Bottom