Habari ya uzima wenu wapendwa,,namshukuru MUNGU kwa kutulinda na kuwa hai mpaka sasa ni kwa kusudi lake.
Mimi ni kijana nina umri wa miaka 29,ni mlokole nasali kanisa la T.A.G
MAADA:
Kuna changamoto ambayo nimeamua kushare nanyi naamini kuna ushauri ntapata kupitiia ninyi,,
Kuna mabinti kadhaa wamekuja kwa nyakati tofauti wakidai wananipenda ni wa hapo kanisani pia lakini wengi nilipowapima wanataka uasherati baadae ndoa kiukweli nilikuwa nikiwakatali nakuwambia ni dhambi na nilaana kweli walikuwa wakinielewa,,,katika Maombi MUNGU alikuwa anawafunua kuwa njia zao hazipo sawa maana yake hawajajikana na kuubeba msalaba,,
NISIWACHOSHE:
Kuna Mama mmoja ambae ni jirani na nilipo panga,,huyu mama amekuwa akisafiri ananiacha kwa nyumba yake ili nikae pale akiwa kasafiri nimekuwa nikifanya hivyo hadi anapo rudi ,,tunaitana Kaka na Dada hajaenda sana kiumri,
Ilitokea kuniamini saana kutokana na maisha yangu kijamii na kikubwa zaidi ninavyo mtumikia MUNGU kwa bidii,maana amekuwa akirudi anakuta mambo ni Safi+Usalama katika nyumba yake,
POINTI KUU:
Alipata mfanyakazi wa ndani kutoka pande za BK(Mhaya) ana kama miezi 7 hivi kama sikosei yupo pale,,tukazoeana nae kama majirani baadae nikamuulizia mambo ya imani akadai alikuwa akisali E.A.G.T mwanzo alikuwa K.K.K.T baadae nikamwambia tuanze kusali wote asikae bila kusali,,amekuja kama Jumapili 3 hivi akaacha Tena kumfatilia ameenda kusali kanisa jingine E.A.G.T,basi nikamshauri mambo ya kiroho nikamwambia inatakiwa usimame sehemu moja na uwe na Baba mmoja wa kiroho akawa amenielewa baadae nimshawishi akasimama sehemu moja mpaka sasa tunasali nae,,
CHAKUSHANGAZA:
Sikumoja yule Dada wa nyumba ile akaniita niende kwake ilikuwa saa 9 alasiri,nikaenda nikakaribishwa sebleni baada ya kusalimiana na mazungumzo kidogo,,nikaambiwa Y tumekuita hapa kwa jambo zuri tu la KIMUNGU ,nikasema sawa Kaka,,niliyekuwa nazungumza nae ni mme wa yule Dada wa nyumba ,akaniuliza Y unampenda T?! Kiukweli hilo swali skulijibu maana nilishitukizwa sikujua ni nini nimeitiwa nikatafakari bila kujibu,,akaulizwa T,,unampenda Y ?! Akasema ndiyo! Nikawaza moyoni mmh!
Kufupisha story,, Nikitoka pale bila kuwapa jibu nikawaambia wanipe muda.
Baada ya hapo binti amekuwa amekuwa akinganda kwa maswali ya kila aina je,nampenda kweli?,Mara anahisi me simpendi,,Mara Nampa majibu ya mafumbo!
Anasema pale nyumbani wananipenda wanatamani yeye aolewe na Mimi,,maana kwa usminifu wangu ntaishi nae.
Kuanzia hapo binti amekuwa akinitumia jumbe nyingi,,je,nampenda kweli maana anataka me nimuoe,Mara haamini kama nampenda,
Me nimemwambia tuingie kwa Maombi tumuulize MUNGU kama akithibitisha itakuwa,
Wazazi wamekuwa wakimlazimisha aolewe kuwa umri umeenda,hadi wamefikia kumtaftia mwanaume wa kumuoa lakin alikataa,,lakini hayo yote yalitokea kabla ya hili Jambo langu.
MOYO WANGU haujafunguka kabisa juu yake nifanyeje?
Msaada maamzi sahihi yanahitajika maana ndoa ni maisha,,
MUNGU awaongoze vyema.