Anatoka na harufu pamoja ute mzito kama makamasi ukeni. Je anasumbuliwa na nini?

Anatoka na harufu pamoja ute mzito kama makamasi ukeni. Je anasumbuliwa na nini?

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2016
Posts
2,228
Reaction score
2,064
Habari zenu wana jf kuna mtu wa karibu yangu anapatwa na tatizo kwa siku kama mbili.

Anasumbuliwa na muwasho ukeni pamoja na harufu kali pia wakati wa kukojoa mkojo unakuwa wa njano sana alafu kunatoa ute mzito kama mafuwa hivi.

Msaada wenu tafadhali, je atakuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani na unatibika je dawa gani anaweza kutumia ili kuondoa tatizo hilo.

Natanguliza shukrani za dhati kwenu
 
Acheni kutumia madawa ya uzazi wa mpango oooh..
 
Kama sio Syphilis hiyo ni Gono akapimwe aanze sindano mapema, pia asisahau kupima Ukimwi huwa vinaenda pamoja hivyo.
 
Hilo ni gono kama njia ya mkojo pia imeathirika na nitatizo la mda mrefu si chini ya miezi 7 linatibika wahi hospitali
 
Uwezekano yaweza kuwa ni fungus za ukeni ( candidiasis vaginalis ) mara nyingi mchanganyiko wa mambukizi ( mixed infection ) kama fungus, trichomoniasis, gonorrhea na trachomatis.Akienda hospitali madaktari watajua tatizo lake vizuri na kuhudumiwa ipasavyo.
 
Kiongozi hapo juu, nakazia hapo kwenye Madawa ya Uzazi wa mpango.

Hayo Madawa ya Uzazi wa mpango sio Mazuri hata kidogo.

Yaani unakuta Mashine inatoa Maji mengi sana, kiasi kwamba hutotaka tena kukutana na Mashine ya hivyo.

Kwa kweli hayo Madawa/Sindano ya/za Uzazi wa mpango hayafai/hazifai hata chembe
 
Kumbe we wa kiume...

Na huyu ni mtu wako wa karibu...

Msisahau kuongozana pamoja!

Upo ndugu yangu? Huo ni ushauri wa busara, anaweza kuwa anatumia dawa haponi kumbe wanatibu tatizo upande mmoja. Vile vile wanashauriwa wasitumie sabuni kali sana zinaua bacteria wanaohitajika kuweka ulinzi huko. Wengi wanafikiri manukato na sabuni kali zinaleta harufu nzuri kumbe ndio wanaharibu.
 
afike hospitali huo ute upimwe, kutumia dawa mtaani ni hatari
 
Back
Top Bottom