Anavuma sana kwenye magazeti ya udaku udaku,na kununua tuzo lakini live jukwaani ni 0%

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
2,567
Reaction score
416
Nimejiuliza sana mpaka nimehamua kulimwaga hapa jamvini, hivi inakuaje msanii anawika na kupambwa sana katika vyombo vya habari hasa magazeti ya udaku udaku udaku, pia hata tuzo anazopata zinaleta maswali na walakini pasipo majibu na cha ajabu zaidi msanii huyu huyu akipanda jukwaani apige live show ni 0%. hata nyimbo zinazompatia huo umaarufu na tuzo pia ni.0.00%.

Wajameni kwa ujanja ujanja huu kweli mziki wa bongo utakua?
 
Swali langu kwako ni moja tu! Hivi unajisikiaje kila siku lazima uandike thread kwa ajili ya mtu huyo huyo? Hivi hujisikii aibu hasa nikizingatia uandishi wako unaonekana ni mwanaume na kila siku kazi yako ni kumwandika mwanaume mwenzako!!

Pole sana, utaishia kujidhalilisha hivyo hivyo kila siku ukidhani kuwa na posts nyingi JF ni ujiko!
 

mkuu nimeuliza swali na sijasema namuongelea nani hapa ndo maana sijataja jina la mtu hapa
 
Ao unaowata wanaoimba live 100% mchangowao kwenye muziki wa Tz ni 0.0002 ila huyo ambae haimbi live mchango wake 68% bora yupi?

bora hao kwani perfomance yao inaonekana na kukubalika
 
mkuu nimeuliza swali na sijasema namuongelea nani hapa ndo maana sijataja jina la mtu hapa
Trust me, una matatizo ndugu yangu na siku utakapokuja kurejewa na ufahamu wako, utajisikia aibu sana unless kama hauna mshipa wa aibu! Sina la zaidi mbali na kuendelea kukupa pole coz' ikiwa una access na internet namna hii, niambie nikupe hata links za free online education kutoka taasisi zinazoheshimika kabisa duniani kuliko kila siku kupoteza muda kuandika mambo ambayo wala hayana faida kwako! Ni ushauri tu, you can take it or leave!
 

Dd azat tree aaao azizah e
 
ivi mtu ananunua tunzo na zile likes kule youtube ananunua pia?
Jana Diamond amenitumia M-Pesa sh. 20,000/= kwa ajili ya kugonga LIKES kwenye page yake ikimuonesha anapiga stori na Youssou N'dour mwaka 2010!!! Yaani jamaa unaambiwa ana pesa wewe... manake anazomwaga kwenye kununua LIKES tu za kutosha hapo hujataja anazonunua kupata views nyingi Youtube, anazonunua tuzo za nje ingawaje pesa ya kununua tuzo za ndani hana; anazowanunua watu kama akina Swizz ili mwanae a-dance Nana... we acha bhana!
 
Please Go STRAIGHT! hilo ni dongo la Mondi si ndio?
 

We kajamaa bwana cjui una shida gani, kwanini usitafute shughuli ya kufanya kuliko kushindq humu ukileta utumbo wako?😱
 
Katika miaka yote hakika mwaka 2015 umekuwa wa mafanikio sana kwa Diamond Platnumz kikazi na maisha binafsi.

(1) Princess Tiffah
: Hii ni furaha ya Diamond kwa sasa, kwa muda mrefu amekuwa akihangaikia suala la kupata mtoto lakini, mwaka huu baada ya kumpata Zari (the boss lady) ndio akafanikiwa. Hata hivyo mtoto kaja na nyota kama ya wazazi wake, kwa siku ya kwanza tu akapata mkataba wa milioni 50, na endorsement ya shopping milioni moja kila mwezi kwa mwaka mmoja jumla mil 62.. Tena baada ya siku arobaini kwenye kuonyesha sura yake akaend3lea kukusanya pesa kutoka kwa NMB, na kupitia tv rights za kipindi kilichoonyeshwa live Clouds tv..

(2) Tuzo na nominations:
Kwa mwaka huu diamond ameendeleza rekodi zake kwenye tuzo mbali mbali kwani mpaka sasa amepata tuzo 9 (6 zikiwa za kimataifa) kwa 2015;

- Hipipo (Uganda 1)
- Ktma (Tz 2)
- Archievers by UDSM (Tz 1)
- African archievers (South Africa 1)
- MTV MAMA (South Africa 1)
- Africa Nafca (USA 2)
- UEA (Uganda 1)

Na hapo bado kuna Tuzo 7 zinazosubiriwa kutolewa zenye jumla ya nominations zaidi ya 17..

(3) Hit songs na Collaborations: Kwa mwaka 2015 Diamond ametoa nyimbo mbili tu! Nasema nawe na Nana.. hizi zote zimefanya vizuri na zinaendelea kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania, Charts kwenye vituo vikubwa, views Youtube, nominations kwenye tuzo, hadi mitaani mpaka wilfred bony aliopo uingereza ikamfikia Nasema nawe akapost instagram account yake akiyarudi mauno. Na ameshirikishwa na Iyanya, K cee, Donald, Ney wa mitego na Linex...

Hata hivyo ngoma zinazosubiriwa;
- Za kwake (Ft. Neyo, Psquare, na nyingine hazijawekwa wazi)
- Za kushirikishwa (Fally ipupa, AKA, Flavour, Toofan na nyingine hazijawekwa wazi)

Vitu vingi sana vikubwa ikiwemo kutajwa kama NEMBO YA TAIFA LA TANZANIA (SHUJAA), kafanya shows zilizompa mkwanja mrefu sana, show za bila kukata tokea tar 1 (Huku akiendelea kuwa mwanamuziki ghali Afrika mashariki), kuumaliza mjengo wake STATE HOUSE unaowatoa mate kila siku wasanii wenzake.

Kuzidi kuongeza mashabiki kila kukicha MITAANI NA MITANDAONI mfano tu instagram mwaka unaanza hakuwa hata na followers laki tatu ila ndani ya miezi tisa kafika milioni, Kufungua studio yake binafsi ya WCB RECORDS ambayo mpaka sasa imemsaini msanii mmoja Harmonize, na ngoma kibao za wasanii zimerekodiwa tayari.

WANAMUZIKI WA BONGO FLAVOUR WANA VINGI SANA VYA KUJIFUNZA HAPO KUTOKA KWA KING OF AFROPOP HIFADHI YA TAIFA.

PRESIDENT DIAMOND PLATNUMZ OF WCB..

Tukiwa tunasubiria kwa hamu kubwa ile collabo bora ya kimataifa kati ya Diamond Platinumz na Neyo, mtoto wa Alicia Keys akiwa ndani ya gari la baba yake ameshindwa kuvumilia na kujikuta akisankoroka vilivyo. Baba yake bila kusita ikabidi arushe kwenye mtandao maarufu kabisa wa instagram ili kuionyesha dunia namna gani Nana ilivyompa homa mwanae.

Hizi dalili njema kwamba mziki wetu umeshatoboa tobo USA kiasi kwamba producer maarufu kama huyu mume wa Alicia Keys anasikiliza muziki wetu tena ndani ya gari yake mwenyewe. Rai yangu kwa wasanii wa Tanzania ni kuwa acheni chuki na wivu wa kijinga kwa Diamond, bali angalieni kafanyaje hadi kaweza kufanikiwa kiasi hicho ili nanyi muweze kufikia kiwango hicho na pengine kuzidi. Tunapofanikiwa si sifa kwenu binafsi bali ni sifa kwa taifa nzima.

Hongera sana Diamond na uongozi mzima wa Wasafi kwa kazi nzuri mnayoifanya.

Post ya mume wake na Alicia Keys huko instagram



Post ya Diamond Platinumz kuhusu collabo yake na Neyo

Attachment ya tatu ni video ya mtoto wa Alicia Keys akisankoroka.

.......................................................................
UPDATES>>

Baada mashabiki wa Diamond Platinumz kuvamia post ya Swiz Beats ikimuonesha binti yake anavyosankoroka na Nana fever, jamaa kapost clip nyingine ikionesha binti yake akimfundisha namna ya kucheza wimbo wa Nataka kulewa wa Diamond Platinumz. Bonyeza hapa kupakua clip hiyo.


View attachment 291906View attachment 291917
 

Acha wivu wa malaya,get a life.
 
Na mbaya zaidi baada ya kujitutumua na dongo lako kama hili jamaa ashuki ndo kwanza anazidi kupanda na wewe unamsaidia kumpromoti bila kulipwa.
 

Hahahahaaa umenichekesha!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…