Anaweza akalipwa fidia?

Anaweza akalipwa fidia?

MOSHIFST

Senior Member
Joined
Jun 4, 2014
Posts
136
Reaction score
262
Habari Wakuu
Kuna binti mmoja alipewa ujauzito na kijana,huyo binti alikua anamalizia masomo yake ya form four mwaka 2011 (yaani alipata ujauzito wakati ndo anafanya mtihani na bahati mbaya alitoka na BRN yanii 33).Bahati mbaya yule kijana aliyempa mimba hakua anakaa kwa wazazi wake coz alikua anasoma chuo kikuu flani hapa Tanzania,kwa hiyo ilitokea tu akampa ujauzito msichana wa watu then jamaa akatimuka.Kuona hivyo (kwa mujibu ya maelezo ya binti,mlalamikaji) yule binti aliamua kwenda kuishi kwa wazazi wa kijana (mlalamikiwa) mpaka alipojifungua mwezi wa nne 2012,kwa muda wote wa ujauzito jamaa hakuhudumia ila wazazi wa jamaa walimhudumia kila kitu mpaka alipojifungua (coz alikua anaishi kwao na jamaa).
Baada ya kuona hivyo,binti alivumilia lakini jamaa akarudi nyumbani kwao baada ya miaka miwili na kumkuta huyo binti jamaa alitimuka tena mpaka leo hajarudi (miaka miwili imepita).Lakini wakati huohuo wazazi wa pande mbili(but upande wa mpigwa mimba walikuja juu) walikubaliana kupeana mahari lakini bila idhini ya muoaji japo muolewaji hakuwa na kipingamizi,basi bana huyu binti amekaa mpka akachoka maana alikua hana mawasiliano na jamaa hata mahusiano hayakua mazuri coz inavyooneka jamaa hampendi mdada! mambo yameenda mdada naye akaanza visa akiwa anakaa hapo hapo nyumbani kwao na jamaa,ikaanza migongano ya hapa na pale mpaka yule binti akaja akatoroka na kwenda kusikojurukana pamoja na mtoto wake,basi jamaa kujilishwa kua mkeo katoroka...jamaa hakufatilia wala kufanya juhudi yoyote akidai kuwa yeye hana mke na hajaoa,huyo mdada kazaa naye tu na hana uhusiano wowote na yeye(but mahitaji ya mtoto anatoa ila kupitia kwa wazazi wake jamaa).Mdada naye aliopotoroka alienda yakamshinda tena alikoenda ikabaidi arudi tena kwa wazazi wa jamaa hukuu mtoto akiwa mgonjwa!
Aliporudi wazazi wa jamaa (yaani mpiga mimba) walimkataa binti wakidai kuwa hawamtambui tena maana katoroka na hawakujua alikua wapi na wakampeleka kwa baraza la wazee la kitongoji na kumfukuza wakimwambia aende kwao au kwa mme wake (yaani mme wake yule mpiga mimba),mpiga mimba naye yuko moto hamtaki kabisa.Basi bana,binti hakua na jinsi ikabidi arudi kwao alikotoka ila alimkataa mtoto na kumwacha kwao na jamaa,wazazi wa jamaa (mpiga mimba) walimkubali mtoto na wanamhudumia kila kitu wala (mtoto walimuuguza mpaka akapona mpaka sasa dogo yuko fiti anadunda tu na bibi pamoja na babu yake,yaani dogo hata mama hajawahi kumwota) kwa hiyo wazazi wa jamaa hawana habari na wazazi wa mtoto wao wanajari mjukuu tu!
Kasheshe imekuja sasa baada ya kupita hizo kukurukakara,jamaa kamaliza chuo na akapata kazi kwenye shirika flani hivi hapa nchini,jamaa ameamua kuoa rasm mke mwingne huku akiwa na madai ya kwamba yule dada aliyempa ujauzito ilikua bahati mbaya ila pia alipokwenda kukaa nyumbani kwao alimwacha maana angeteseka sana wakati akiwa mjauzito,ila tatizo la binti ana kiburi na kujifanya much know pia wazazi wa binti ni wakorofi sana ndo maana kaamua kumwacha na pia hana ndoa yoyote naye,hajakaa naye wala kulala na toka apate ujauzito na kujifungua mpaka leo yaani kutoka 2011 mpka 2015.
Kuskia kuwa jamaa anataka kuoa binti naye kaja juu anataka sijui madai au fidia akidai kuwa eti kamharibia maisha na kamtelekeza,na binti anadai talaka pia.
Huyu jamaa ni rafiki yangu na binti pia ni ndugu yangu,je kwa macho ya sheria huyu dada ana haki ya kumzuia kuoa huyu rafiki yangu au ana haki ya kumshitaki kwa kutomuoa? ukiangalia hawajakaa pamoja toka mimba itungwe mpaka leo? Binti ni ndugu yangu ila pia kichwa maji sana,wazazi wake naye binti nao ni hovyo maana wamejenga visasi sana kwa jamaa eti wanataka kumfilisi ila jamaa naye ni wale wale,akitishia kidogo tu anawajibu naye hovyo hovyo tu kuwa hampendi binti yao hata akimwoa hawatadumu ila tu anaweza akamsaidia kwa njia nyingne tu km akihitaji msaada km mzazi mwenzake na si km mke! na amewaambiwa bora aolewe na wanaume wengine tu maana hawezi kuoa kwa kutishiwa au kulazimishwa na akawaambia pia km wanaona anamkaosa waende tu mahakamani wamshitaki basi na si vinginevyo.Nawasilisha kwenu wajuzi wa sheria na wanajukwaa kwa ujumla,je huyu dada ana haki kisheria kumshataki huyu jamaa?
NB:katika mgogoro huu nami nahusishwa na wazazi wa binti(ndugu zangu) wananilalamikia rafiki yangu kamharibia maisha mwanao
 
Mkuu mi sijui sheria ngoja waje ila naona kma hkuna kesi hapo
 
Mkuu mi sijui sheria ngoja waje ila naona kma hkuna kesi hapo
Nawasubiri kwa hamu mkuu,maana kuna mambo mengine unaweza ukaona usumbufu kumbe wanasheria wanaona sivyo kwa jicho lao la kisheria
 
Huyu binti ana umri gani sasa?
Baba wa mtoto atalazimika kutoa matunzo ya mtoto lakini swala la ndoa ni makubaliano baina ya muoaji na muolewaji, hakuna shurutisho.
 
Huyu binti ana umri gani sasa?
Baba wa mtoto atalazimika kutoa matunzo ya mtoto lakini swala la ndoa ni makubaliano baina ya muoaji na muolewaji, hakuna shurutisho.
Binti ana miaka 26 mkuu,na mtoto ana miaka mitatu ila anatunzwa na wazazi wa baba wa mtoto,binti sasa hivi naye yuko kwa wazazi wake yaelekea mwaka sasa mkuu namless girl
 
malalamiko ya wazazi wake hayatakiwi kukuumiza, we hukuwepo wkt wanafanya mambo yao..watu wazima toka then hadi now...sema unamtafutia ndugu yako a solution
 
Back
Top Bottom