Anaweza kusoma kozi gani huyu

Chilangachiba

Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
26
Reaction score
2
Ndugu zangu wana jamvi. Nina ndugu yangu ambaye ni muhanga wa matokeo ya Kidato cha nne ya mwaka huu ambayo yameundiwa tume na Mheshimiwa Pinda ili kuwapa watu ulaji. Ndugu yangu huyu amepata D mbili tu yaani ana division IV ya 33 (amepata D ya kiswahili na Kiingereza). Zamani zilizopita mwaka 2008 alisoma certificate ya Nursery Teaching, kwa kweli amerudia mitihani hii ya O-level mara mbili sasa bila mafanikio na kwa kweli amekata tamaa ya ku-reset tena. Je anaweza kusoma kozi gani kwa hizi qualifications alizonazo. Nisaidieni wana jamvi maana mtu ananitegemea. Nategemea kupata majibu. Thanks
 
Ajifunze ukalimani, kiingereza, kiswahili, na lugha nyingine. inaonyesha ana afadhali kwenye lugha
 
duh, hapa inatakiwa uwe na upako ndo utoe ushauri... Mm simo...
 
kuna hivi vyuo vinavyo tangazwa kila siku kwenye media (sitaki kuvitaja, bila shaka mnavijua) wao wanapokea kuanzia darasa la saba. kwa yeye na pass zake 2 atapokelewa bila wasi.wana kozi za utalii,computer, secretary,upishi,hotel, ualim wa nursery n.k .
 

amuulize NAPE..alifanyaje
 
nenda veta kaulizie kozi gani....anaweza kujifunza ufundi stadi mambo ya katering ujenzi food processing design nk akajiajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…