Chilangachiba
Member
- Oct 2, 2012
- 26
- 2
Ndugu zangu wana jamvi. Nina ndugu yangu ambaye ni muhanga wa matokeo ya Kidato cha nne ya mwaka huu ambayo yameundiwa tume na Mheshimiwa Pinda ili kuwapa watu ulaji. Ndugu yangu huyu amepata D mbili tu yaani ana division IV ya 33 (amepata D ya kiswahili na Kiingereza). Zamani zilizopita mwaka 2008 alisoma certificate ya Nursery Teaching, kwa kweli amerudia mitihani hii ya O-level mara mbili sasa bila mafanikio na kwa kweli amekata tamaa ya ku-reset tena. Je anaweza kusoma kozi gani kwa hizi qualifications alizonazo. Nisaidieni wana jamvi maana mtu ananitegemea. Nategemea kupata majibu. Thanks