Anaweza kuzaa na mwanamume mmoja tu hapa duniani!!!

hahahahaaaaaaaa

nimefurahi sana kwa mcango huu.

ni moja ya kanuni muhimu sana, palilia sifa zako hadi mwisho.

kuna watu wanabadilika mfano baada ya kuolewa au kuoa wanaonyesha tabia nyingine kwa wenzi wao na hawaonyeshi kunyenyekea tena kama mwanzo. matokeo yake ndoa zinaanza kuchacha, muhimu sana tusikunjue makucha baada ya mambo kutuendea vizuri.

unawza kurejea kisa cha nani wa kwanza kujulishwa mtoto anapozaliwa uona mojawapo ya matokeo ya kurefusha makucha ndani ya ndoa

Tatizo unafurahiiiiiiiiii, afu unacheeeeeeeeka matokeo yake unasahau kale kabatani ka SENKSI! Afu unategemea kura yangu ili upate ubunge....... Hahaha! Hujachelewa kagonge basi!

nikuhakikishie mzee PJ wote ni waafrika. wanishi dar mmoja kinondoni na mwingine kijitonyama

katika mazungumzo yetu na wote wawili niligundua mengi sana katika maisha yao wote wawili yaliyoathiri saikolojia zao. huko kuwachukia wanaume kulitokana na sababu nyingine nje ya mapepo kama walivyochangia wengine hapa jamvini. moja ya sbabu ilitokana na kuwa alianza mapenzi katika umri mdogo sana, misukosuko aliyoipata ndani na nje ya familia yake ilipelekea kuamua "kustaafu" masuala ya mapenzi alipofikisha umri wa miaka 23 tu!

hadi anakutana na huyo mpenzi wake alikuwa na umri wa miaka 32 (mpenzi wake akiwa na miaka 33) yaani takribani miaka 9 ma maisha ya ustaafu, tena bila penseni!

Nimeshangaa maana nilidhani huyo mdada ana miaka 50!
Sasa huyo kaka anajibaraguza nini kama mdada anampenda kiasi hiki?...Atakuja kujuta zama hizi za usanii wa mapenzi.

ni hivi muu, wakati wanakutana kwa mara ya kwanza mwanume alikuwa 33 mwanke 32, hadi wananiletea kisa hiki ni miaka takriban mitano wako katika uhusiano kwa hiyo mwanaume alikuwa 38, mwanamke 37.

nafikiri sasa nimeeleweka vizuri

asante kwa ufafanuzi..bado hoja yangu iko palepale!
Mwambie huyo kaka aache kujivunga..atakuja kujuta when it is too late.

ni hivi muu, wakati wanakutana kwa mara ya kwanza mwanume alikuwa 33 mwanke 32, hadi wananiletea kisa hiki ni miaka takriban mitano wako katika uhusiano kwa hiyo mwanaume alikuwa 38, mwanamke 37.

nafikiri sasa nimeeleweka vizuri

Mkuu hii ni hadithi nzuri na kuna mambo mengi ya kujifunza. Wanawake wanaelewa vizuri mambo ya maisha kuliko wanaume linapokuja suala la kuzaa watoto. Ndiyo maana ni kawaida sana kusikia mwanamke analaani kwamba kachezewa (endapo uhusiano aliokuwa nao hakuenda kama alivyotarajia).

Hawa wote wana matatizo. Mwanamke ana matatizo ya kisaikolojia ambayo yanatokana na historia yake ya nyuma. Kwa hiyo itakuwa vizuri akapata msaada zaidi toka kwa watalaamu. Vinginevyo atakuja kuwa kichaa kama huyu mwanamume wa sasa atamfanyia kitu ambacho hakukitarajia wakati wanaendelea na uhusiano wao.

Huyo mwanamume pia ana matatizo. Kama alihitaji kuoa mwanamke mwingine, kwa nini alikaa na huyu muda wote huo? Na hadi anakutana na huyu (akiwa na miaka 33) hakuwa ameshaamua ni mwanamke wa aina gani anamtaka? Mshauri akubali alichokipata badala ya kuhangaika kutafuta anachokitamani wakati hata hajui kama atakipata.

alipenda mwenyewe, shida ila wenzie walikuwa wamemzidi umri na wazoefu zaidi
kwa huyu wa sasa ndio mapenzi ya dhati au ndo anakimbizana na muda maana age haimsuburi, age nzuri ya kuzaa ni under 35!

sifikiri kama anakimbizana na age, kamaingekuwa hivyo si angezaa na mwingine yoyote, kwani lazima amlilie huyu kama yeye hamtaki?

nafikiri ametokea kupenda tu kutokana na kuvutiwa na lifestyle yake, kumbuka wana miaka takriban mitano kwenye mapenzi na wote wanakiri mapenzi yamekuwa mazuri sana kwa muda wote huo

Hawa wote wana matatizo. Mwanamke ana matatizo ya kisaikolojia ambayo yanatokana na historia yake ya nyuma. Kwa hiyo itakuwa vizuri akapata msaada zaidi toka kwa watalaamu. Vinginevyo atakuja kuwa kichaa kama huyu mwanamume wa sasa atamfanyia kitu ambacho hakukitarajia wakati wanaendelea na uhusiano wao.

Huyo mwanamume pia ana matatizo. Kama alihitaji kuoa mwanamke mwingine, kwa nini alikaa na huyu muda wote huo? Na hadi anakutana na huyu (akiwa na miaka 33) hakuwa ameshaamua ni mwanamke wa aina gani anamtaka? Mshauri akubali alichokipata badala ya kuhangaika kutafuta anachokitamani wakati hata hajui kama atakipata.

ni kweli, mkuu

wote wawiili wanapata psychological training, na wanaendelea vizuri

Haya wapendwa nawaletea kisa kingine.

Kuna mwanamke mmoja mtu mzima, alinifuata nimsaidie kumshauri mpenzi wake aliyenaye angalau akubali kuzaa nae hasa baada ya kukataa kumwoa! Alisema kwa uchungu huku machozi yakimtoka.

Katika mazungumzo yetu, ilibainika kuwa yule mwanamke anawachukia wanaume wote hapa duniani isipokuwa huyo mmoja tu! Na hadi anakutana nae huyo pekee anayempenda alikuwa alikuwa kishakaa karibu muongo mzima bila mwanume na alishaamini kuwa hatahitaji mwanaume hadi mwiso wa maisha yake.

Kuhusu alivyotokea kupendana na huyu mwanaaume, alisema alimsikia siku moja akiongelea vizuri masuala ya malezi ya watoto, akampenda hadi leo! Hana sababu nyingine.

Alimshauri amuoe akakataa, alimshauri wazae mtoto, akakataa. Akaona kila dalili za kurudia maisha yale ya upweke ziko wazi, akajaribu kuzizuia zisifike,

alikuja kwangu nimsaidie, nashukuru, sasa ana ujauzito wa huyo bwana na ana furaha sana, na mpenzi wake ana furaha na amani.

tabia ya huyu dada nimeipenda, amenikumbusha kisa cha Abigail na mumewe Nabali!

Mungu ni mkuu sana

Mbunge wa CCM kwanza naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Mimi nadhani huyu mwanamama anatafuta mtambo wa kumzalishia watoto na kulea tu basi. Sidhani kama kuna mapenzi hapa.

Haya wapendwa nawaletea kisa kingine.

Kuna mwanamke mmoja mtu mzima, alinifuata nimsaidie kumshauri mpenzi wake aliyenaye angalau akubali kuzaa nae hasa baada ya kukataa kumwoa! Alisema kwa uchungu huku machozi yakimtoka.

Katika mazungumzo yetu, ilibainika kuwa yule mwanamke anawachukia wanaume wote hapa duniani isipokuwa huyo mmoja tu! Na hadi anakutana nae huyo pekee anayempenda alikuwa alikuwa kishakaa karibu muongo mzima bila mwanume na alishaamini kuwa hatahitaji mwanaume hadi mwiso wa maisha yake.

Kuhusu alivyotokea kupendana na huyu mwanaaume, alisema alimsikia siku moja akiongelea vizuri masuala ya malezi ya watoto, akampenda hadi leo! Hana sababu nyingine.

Alimshauri amuoe akakataa, alimshauri wazae mtoto, akakataa. Akaona kila dalili za kurudia maisha yale ya upweke ziko wazi, akajaribu kuzizuia zisifike,

alikuja kwangu nimsaidie, nashukuru, sasa ana ujauzito wa huyo bwana na ana furaha sana, na mpenzi wake ana furaha na amani.

adsisi inayokujja ni ya sungulla sikia, adsisi uliyongoja leo tumekuletea. Nimeandsika ki dsarasa la tatu B ili kuongewza mashiko

najionea sinema ya kihindi tu hapa. huwezi funga milango kwa kuwa umefungiwa mlango sehemu fulani...hiyo nayo ni abuse ya maumbile yako. tumeambiwa tuhangaike kutafuta maisha. kama maisha ulipotarajia hayakubali, kwa nini usijaribu kwingineko? labda kama una matumaini yenye ishara ya mafanikio

Back
Top Bottom