Amemaliza 4m4 hakuchagua kwenda advave bali chuo so bado anasubiri selection
1.Kwa kozi atakayochaguliwa ajitahidi awe mzuri sana sio kwenye mitihani tu lakini tu hata kiutendaji mfano kupresent kazi za darasani na kama kozi zina practical awe mzuri zaidi na huko.
2.Awe mwepesi kushirikiana na wengine academically,kwa anachojua awe mwepesi kuwashirikisha wenzake na kuwasaidia wenye uwezo mdogo darasani.
3.Awe mwepesi wa kujichanganya,na kuongea na watu,group discussion,vyama vya kidini,events za chuo...uchangamfu,ucheshi,utani na furaha ndivyo huunganisha watu kwa urahisi sana.Bila kusahau michezo.
3.Ukaribu atakaoupata na watu autumie kuwajua watu zaidi,asilazimishe,awe yeye lakini apate kuwajua watu,walikotokea,stori zao za maisha,kwa nini wapo hapo,matamanio yao.Awe mzuri wa kuuliza maswali kwa wote wakubwa wake,walimu wake na wale wa rika lake.Awe mzuri sana wa kusikiliza.
4.Muda wa likizo asiutumie kurudi nyumbani,kuna sehemu potential ambazo wanaweza kuhitaji mtu mwenye ujuzi kama wake...makampuni,mashirika n.k aombe akajifunze kwa vitendo zaidi.Huko ajitume,ajishushe na awe mdadidisi wa kutaka kujua na kujifunza zaidi.
5.Si kila mtu ambaye atafahamiana nae atakuwa na msaada sana kwake,kwa wale watakaonesha kuwa karibu na kuvutiwa na namna alivyo awaweke karibu zaidi,ni rahisi kupata msaada wa mawazo au chochote huko.
6.Ajifunze kukipenda zaidi kile atakachoenda kusomea,aenjoy maisha ya chuo,aheshimu wakubwa zake na wadogo,ajitenge na makundi yanayoweza kumuhuharibia ndoto zake,awe na karibu na watu wenye ndoto kama yeye na wale wanaofanya kile anachokisomea.
Naamini anaweza kupata mwanzo mzuri wa kile anachokipagania.
Kila la heri kwake.