Anayebambuliwa ana haki ya kushtaki?

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Hii kitu inaitwa kubambua. Ipo sana huku Kilimanjaro, sijui mikoa mingine kama ipo. Ni hivi: Kwa mfano kamati ya shule ya msingi imeamua kila mtoto alete shuleni mahindi debe moja na maharage sado mbili. Halafu wanatangaza kwamba mzazi atakayeshindwa kuleta vitu hivyo, atabambuliwa yaani mali zake za nyumbani zitakamatwa.


Hii ilimtokea dada yangu mapema mwezi huu wa kwanza. Mtoto wake anayesoma shule ya msingi aliagizwa apeleke mahindi debe mbili, maharage sado tatu na mzigo wa kuni. Mzazi wa mtoto hakuzingatia sana jambo hili ila alistukia siku moja kikundi cha watu wanakuja nyumbani kwake na mmoja wao anaingia sitting room na kuanza kuzoa makochi. Dada alipouliza kisa na mkasa akaambiwa anabambuliwa kwa sababu hajatoa mahindi, maharage na mzigo wa kuni. Ilibidi aombe sana wasichukue makochi yake ila walikubali atoe pesa badala ya nafaka na mzigo wa kuni. Dada akatema sh. 44,500/-wakaachana naye.

Wanasheria naomba mnisaidie. Je kama asingekuwa na hizo fedha na makochi yakachukuliwa angekuwa na haki ya kwenda kushtaki popote? Au kwa maneno mengine: Hii kitu ya kubambua watu ina nafasi gani katika sheria zetu?
 
Hao ni wezi kama wezi wengine tu. yeye apige yowe na wao wabambuliwe vichwa kwa sababu mahakamani watapelekwa jela na kutuongezea mzigo walipa kodi huru.
 
Kubambua? Duh hiikali ili neno nalipeleka jukwa la lugha nikapate ufafanuzi kamili
 
Kubambua? Duh hiikali ili neno nalipeleka jukwa la lugha nikapate ufafanuzi kamili

Kwa uzoefu wangu, kubambua ni kama kutaifisha mali ya mtu aliyeshindwa kulipa mchango fulani ilivoelezwa na mtoa mada, au huwa kama adhabu kwa mtu aliyeacha kutoa nguvu kazi bila sababu za msingi.
Ninavyoajua, aina hii ya utaifishaji inakuwa imepewa baraka kupitia mkutano wa wanakijiji, ikihusisha vitu vitakavyobambuliwa; ili kuhakikisha lengo fulai (kama kujenga shule linatimia). Kwa kawaida ubambuzi unaogozwa na M/kiti wa Kitongoji akishirikiana na migambo wa Kata. Hivyo basi, siamini kama ni kosa kubambua.
Ahsante sana mtoa mda, umenikumbusha mbali sana, nawatakia michango mwema ili kuhakikisha watoto wanakula mchana wakiwa shuleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…