SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Hii kitu inaitwa kubambua. Ipo sana huku Kilimanjaro, sijui mikoa mingine kama ipo. Ni hivi: Kwa mfano kamati ya shule ya msingi imeamua kila mtoto alete shuleni mahindi debe moja na maharage sado mbili. Halafu wanatangaza kwamba mzazi atakayeshindwa kuleta vitu hivyo, atabambuliwa yaani mali zake za nyumbani zitakamatwa.
Hii ilimtokea dada yangu mapema mwezi huu wa kwanza. Mtoto wake anayesoma shule ya msingi aliagizwa apeleke mahindi debe mbili, maharage sado tatu na mzigo wa kuni. Mzazi wa mtoto hakuzingatia sana jambo hili ila alistukia siku moja kikundi cha watu wanakuja nyumbani kwake na mmoja wao anaingia sitting room na kuanza kuzoa makochi. Dada alipouliza kisa na mkasa akaambiwa anabambuliwa kwa sababu hajatoa mahindi, maharage na mzigo wa kuni. Ilibidi aombe sana wasichukue makochi yake ila walikubali atoe pesa badala ya nafaka na mzigo wa kuni. Dada akatema sh. 44,500/-wakaachana naye.
Wanasheria naomba mnisaidie. Je kama asingekuwa na hizo fedha na makochi yakachukuliwa angekuwa na haki ya kwenda kushtaki popote? Au kwa maneno mengine: Hii kitu ya kubambua watu ina nafasi gani katika sheria zetu?