HOJA Anayedai kudhumiliwa Dola 200,000 amlilia Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba

HOJA Anayedai kudhumiliwa Dola 200,000 amlilia Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Denice Deusdedit Nsimeki, kijana wa Kitanzania aliyekwenda kusoma tangu mwaka 2021 amekujikuta akishindwa kuendelea na masomo yake baada ya kujiingiza kwenye biashara ya madini na matokeo yake kutapeliwa Dola 200,000 (sawa na Zaidi ya Sh500 milioni).

Katiba barua aliyomwandikia Waziri Mkuu Januari 30, 2026 pamoja na maelezo mengine aliyoyajua Juni 14, 2026, Nsimeki anaomba asaidiwe kutatuliwa tatizo lake, akidai kuwa fedha hizo alitapeliwa na kampuni ya Chato African Gold inayojihusisha na uuzaji wa dhahabu.

Nsimeki anasema kuanzia mwaka 2025 akiwa nchini India, alijiunga na wafanyabiashara wanaomiliki kampuni ya Inaara Precious Metal F.Z.C Company aliowakaribisha kuja kufanya biashara nchini Tanzania.

“Wafanyabiashara hawa ambao waliniteua mimi kuwa mwakilishi wao kwa nchi za Africa,” anasema.

Anaeleza kuwa, Novemba 25, 2025 akiwa jijini Dar es salaam alikutana na Pius Charles Madabuke anayemiliki kampuni ya Chato African Gold inayojihusisha na uuzaji wa dhahabu ofisi hiyo iko kwenye jengo la soko la madini ghorofa ya 11 mtaa wa Samora Evenue.

Anasema baada ya kukutana na Mabaduke walikubaliana kwamba Mabaduke awauzie dhahabu kilo 12 tu.

“Akatutaka tumpe pesa za kulipia ushuru ambazo ni Dolla 200,000 sawa na Zaidi ya Sh500 Milioni ili kuwezesha kufanya biashara ya madini ya dhahabu yenye uzito wa kilo 12, yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani 1.8 milioni (Sh46.4). Bosi wangu aliondoka kuendelea na majukumu yake, na majukumu yote ya hapa nchini nikaachiwa Mimi mwakilishi wa kampuni.

Nsimeki anasema Bosi wake alilipa fedha hizo (Dola 200,000 kwa njia ya Cryptocurrency.

“Ilipofika Desemba 2, 2025 ndugu Pius Madabuke aliniita niende Kawe kushuhudia uchomaji wa dhahabu mpaka tukaziweka kwenye Jewel Boxes nikazihifadhi kwenye safe box yangu.

“Pius Madabuke alipendekeza nihamie maeneo ya karibu na mjini wakati najiandaa na safari akatafuta nyumba (B&B) Mikocheni akalipa yeye tukahamia hapo mimi pamoja na mdogo wake ndugu Willington Reginald Moshi tukiwa na dhahabu zetu,” anasema.

Anaendelea kueleza kuwa Desemba 4, 2025 alimfahamisha Piuse Madabuke kuwa anakwenda Tegeta kuchukua pasi yake ya kusafiria.

“Pius Madabuke alituletea gari aina ya Benz tukatoka mikocheni mimi pamoja na mdogo wake tukiwa na box zetu za dhahabu kuelekea Tegeta.

“Tulipofika maeneo ya mlalakuwa karibu na makao ya JKT tulisimamishwa na polisi na kabla hajasema chochote ilitokea gari aina ya IST ikiwa na mwendo mkali ikasimama nyuma yetu wakashuka kwa kasi watu wawili wakiwa na radio call pamoja na pingu wakamshusha mwenzangu kwa nguvu ndugu Willington Reginald Moshi aliyekuwa anaendesha gari wakakaa naye pembeni.

“Baadaye wakanishusha na mimi kwa nguvu wakanifunga pingu wakatupakia kwenye gari aina ya IST aliyetusimamisha aliona tukio hilo. Moshi aliwauliza ninyi ni kina nani?

“Watu hao wakamjibu sisi ni wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya TPSIS (Tanzania Private Security lntergratation Services) wakaonyesha vitambulisho vyao. Wakamwambia kwamba sisi tumeiba simu ndio maana wametukamata.

“Askari (traffic) akaamuru watufungue pingu akawafunga wao baada ya tukio hilo mmoja wao alijitambulisha kuwa Katibu wa CCM (W) Kinondoni.

“Traffic aliita wenzake wakatuchukuwa wote mpaka Oysterbay polisi.”

Anasema walipofika kituo cha Polisi Oysterbay walikutana na ofisa mwenye nyota tatu waliyemtambua kwa jina la C.M. Lugaila ambaye aliamuru wafungue masanduku yenye dhahabu.

“Nikafungua akaona dhahabu akaniamuru nifungie tena box wakatuweka mahabusu bila hata ya kuchukuliwa maelezo pale kituoni.

“Kilichonisikitisha mimi wale watu wa kampuni ya TPSIS walikuwa wakitufuatilia na kutaka kututeka waliachiwa kwanza wakitoa sababu kuwa mmoja anaumwa presha na mwingine mke wake ni mjamzito mimi nikabaki na mdogo wake Pius Madabuke kituoni.

“Tukaambiwa tumuite Pius Madabuke alete nyaraka za dhahabu lakini hakutokea. Ilipofika saa 5 usiku alifika Ofisa mmoja (anamtaja) akatuambia tuandike maelezo kuwa wametuachia na dhahabu zetu zikiwa salama baada ya kujiridhisha kuwa sisi sio wahalifu bali ni wafanya biashara halali tulipomaliza kuandika maelezo walinikabidhi jewel box niondoke nazo usiku ule.”

Hata hivyo anasema walipotoka tu kituoni hapo alishangaa kumwona Pius Madabuke akiwa ndani ya uzio wa polisi usiku ule.

“Akaniamuru niweke dhahabu kwenye gari lake tukaondoka hadi ofisini kwake soko la madinini Samora Evenue Floor No 11,” anasema.

Anasema siku iliyofuata Pius Madabuke aliwaeleza kuwa ameitwa polisi Osterbay na RPC hivyo wapumzike akitoka atawajulisha.

“Pius Madabuke alitujilisha kuwa ameachiwa pia Ofisa Madini wa Mkoa wa Dar es salaam (RMO) amekataza biashara isifanyike mpaka zipite siku 21.

“Madabuke alitukabidhi nyaraka zinazoonyesha amelipa ushuru wa serikali kumbe zote alikuwa ameghushi kwani zinaonyesha malipo yamefanyika mwaka 2023 badala ya mwaka 2025.”

Kutokana na hali hiyo, anasema alikwenda kumwona Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ambaye naye alimrudisha kwa Ofisa Upelelezi wa Wilaya ambaye naye alimpa mpelelezi wa kesi hiyo.

Ili kupata suluhisho la mapema, Nsimeki aliamua kwenda kumwona Ofisa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO) Faustine Mafwele.

Mafwele akanikabidhi kwa mpelelezi (anamtaja), ambaye alimsaidia kufungua jalada la uchunguzi NO. KIN/CIO/PE102/2025.

Tangu wakati huo, Nsimeki anasema kesi yake haikukamilika, badala yake alianza kufuatiliwa na watu wasiojulikana kila alipokuwa akienda.

“Niliamua kurudi nchini India kwa ajili ya usalama wangu, lakini mpaka sasa nimefukuzwa kazi na kampuni iliyoniajiri, huku Pius Madabuke akiendelea kutamba mitaani.

“Waziri Mkuu, ombi langu kwako naomba unisaidie ndugu Pius Madabuke alipe pesa Tshs. Millioni 500,000 za watu pia unilinde kwani ananitumia watu wa kunidhuru nimekuwa naishi kwa mashaka sana kwani nafuatiliwa na watu kila ninapokwenda.

Kwa mujibu wa gazeti la Rada la Aprili 13-19, 2026, Mkurugenzi wa Chato African Gold, Pius Madabuke alikiri kufahamu suala hilo na kusema liko chini ya vyombo vya uchungunzi lakini akasema biashara hiyo ilighubikwa na utapeli mkubwa

"Mchakato wa biashara hiyo ulijaa utapeli mpaka baadhi ya wafanyakazi wangu na ofisi wamehusishwa na wamehojiwa na mamlaka serikali,” alisema Pius za Madabuke.

"Wewe angalia nyaraka zote, ni wapi kampuni yango imelipwa fedha hizo. Sijawahi kupokea fedha yoyote. Pia biashara ya dhahabu haifanyiki namna hiyo. Huyo amepigwa wahuni alisema.”

Kigogo amiliki mtandao hatari

Waziri katika serikali ya awamu ya nne (jina linahifadhiwa) ametuhumiwa kuwalinda kwa kutumia cheo chake vibaya wahalifu waliohusika kumteka na kumtapeli kijana wa kitanzania Denis Nsimike mbele ya askari wa usalama barabarani maeneo ya Mlalakuwa Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa gazeti la Rada la Aprili 20- 26, 2026, inadaiwa kwamba wakati tukio hilo linatokea, mfanyabiashara huyo Denis Nsimeki alikuwa na dhahabu kwenye gari zilizokuwa na thamani ya shilingi bilioni 46 za Kitanzania alizokuwa amekadhiwa na kampuni ya madini ya Chato African Gold ndipo alipokutana na mkasa huo wa hatari.

Kigogo huyo mstaafu kutoka wizara inayosimamia Jeshi la Polisi nchini alifanikiwa kuwasaidia watuhumiwa kuwatoa kwenye mikono ya polisi oysterbay muda mchache baada ya kung'ang'aniwa.

Kwa upande mwingine, kigogo huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria amenukuliwa sehemu mbalimbali katika ofisi za serikali anapoitwa mfanyabiashara mkubwa wa madini nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chato African Gold Charles Pius Madabuke akidai kwamba yeye ndio msemaji anayemtetea mteja wake popote anapoitwa na mtu au taasisi za serikali.

Katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Nsimeki amesema kwamba mkasa huo wa kunusurika kutekwa ulitokea maeneo ya Mlalakuwa baada ya kusimamishwa na askari wa usalama barabani ndipo walipotokea 'watekaji' waliokuwa na gari ndogo wakiwa na silaha zikiwemo pingu.

Kijana huyo anaelezea kuwa kilichomuokoa kutoka mikononi mwa watekaji ni baada ya askari trafiki kuingilia kati na kuwataka wahalifu hao pamoja na mhanga wote waende ende Kituo cha Polisi Oysterbay Dar es salaam kwa mahojiano zaidi.

Nsimeki ni Mtanzania ambaye ni mwakilishi wa Kampuni moja ya kigeni inayojihusisha na biashara ya dhahabu nchini India kwa Ukanda wa Afrika ikiwemo Tanzania (jina linahifadhiwa)
 
Dah!! Hapa ndipo unapotamani uchawi mmae..
Nchi imeoza hii, haki hakuna kabisa.
 
Mambo ya cryptocurrency kwa bongo n rahis kutapeliwa

Pesa za mtandaon kwa bongo bado sana
 
Back
Top Bottom