Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Anayefahamu kanisa zuri lenye sifa zifuatazo, anijulishe nijiunge tafadhali

Man kuna ukweli. Kuna moja lipo mitaa ya Kibangu kanisa la Mabati Mabati, sitataja exactly location.

Bwana nikaanza kwenda, sio kanisa langu ila kwakua lipo karibu na nilipokua nimehamia. Mi naendaga kanisa la jirani lolote.

Day one nimeenda attention ndogo wakasema tu wageni wajitambulishe nikajitambulisha. Basi ikaisha. Wanasisitiza tutoe sadaka kuanzia buku 5 kwenda mbele.

Next Sunday kukawa na mvua, nikaondoka home na gari, sasa ubaya unavopaki pale kila mtu anakuona. Parking ipo mbele ya kanisa, hafu ni la mabati na nyavu so kuanzia mchungaji anakuona.

Tunavotoka wanasema vijana wabaki. Mi uwa sijishirikishi hayo mambo, nataka kusepa jamaa akanifuata akasema vijana tunabaki. Aisee nilipewa cheo sijui kamati ya nm ya vijana. Na ndio ikawa Jumapili yangu ya mwisho hapo.
Mmmh siku hizi kuna ministry nyingi na kila MTU anajiita yeye ni assemblies o Pentecostal..so watu wanapiga pesa kupitiaa tiketi ya ulokole but for me TAG is the best one[emoji5][emoji5]
 
1. liwe kanisa la kikristu (hapo unaonekana mkatoliki, kanisa lililokufa limebaki mifupa tu,okokeni mmwone Mungu maishani mwenu).

2. Mfumo wa kitaasisi (hiyo sio garantii kwamba ni kanisa sahihi).

3. kila mkoa/wilaya (hiyo sio garantii kwamba ni kanisa sahihi).

4. teamwork na kusaidiana/kubaguana etc (hakuna kanisa kama hilo siku hizi, popote utakapoenda treatment ya watu inatofautiana na kipato chako, elimu, michango kwa church, wadhifa n.k. hii ni kwasababu, kikawaida mtu anayestahili heshima, mpe heshima yake hata atakapokuja church. hatutegemei Mkuu wa Jeshi Mabeyo aje church halafu tumkalishe au tumchukulie kikawaida kama tunavyokuchukulia wewe, ana hadhi yake hata kama pale church sote tupo sawa. usipompa heshima yake nalo ni kosa. sisemi kuwa ni kosa na sisemi uwa ni sahihi.

5. kutegemea uwepo wa mchungaji (najua hapa unamsema kakobe, au wengine. kila kanisa linategemeana na nani amelianzisha na aliyeanzisha ametoka vipi na Mungu, sio kila jumuiya ya kikanisa itakusaidia umwone Mungu, wengine hata kama unawaona wakuda na hauwaelewi Mungu anawatumia na wangeweza kukusaidia).

6. kanisa lenye ratiba maalumu (hapo utayapata makanisa ya shetani au ya mafarisayo tu ambayo yanampangia Mungu ratiba. kanisa halisi ni Mali ya Roho Mtakatifu ndio analiongoza, kama Roho Mtakatifu atataka muendelee na ibada masaa sita au kumi, mtaendelea, kama atataka muendelee lisaa limoja mtamsikiliza. huwezi kumpangia Mungu masaa. ni sawa na mtu aliyeenda kuchimba dhahabu akakuta dhahabu inatema mno, lakini akajiwekea masharti kuwa hata kama dhahabu inapatikana ikifika saa fulani naondoka. unajuaje muda ule unapoondoka ndio kisima cha baraka/mafuta ya Mungu kitatibuka? naongea na watu wanaomjua Mungu tu hapa, wengine hamtanielewa. makanisa yote yenye ratiba za kumpangia Mungu, ni ya kifarisayo na kidini, na hayamsaidii muumini kumjua au kumwona Mungu katika maisha yake.

7. kanisa linalojali malezi ya watoto (hapo nakubaliana na wewe, ndio kazi mojawapo ya kanisa hiyo).

8. kanisa la watu wenye akili timamu (hapo hujui unaongea nini, hao unaowadharau na kuwaona hawana akili timamu yawezekana ndio waliokuzidi hata wewe akili. siku ya pentecost watu wengi walishangaa mitume wanaponena kwa lugha, wengine wakasema wamechanganyikiwa, wengine wakasema wamelewa, hadi Petro aliposimama na kuwaelewesha. ndivyo mlivyo mafarisayo wa siku hizi, watu wanapobubujika na kukutana na Mungu, mnasema hawana akili timamu, kumbe hamjijui kuwa ninyi ndio msio na akili. Yesu aliwaita watu kama ninyi kuwa ni makaburi yaliyopakwa rangi kwa nje ila ndani yamejaa mifupa mitupu tena inayonuka (emphasis added).

9. kanisa linalopenda haki na usawa. sijui una maanisha nini kwa kusema hivyo. kanisani tunaenda kumwabudu Mungu, ni haki gani unaenda kutafuta kanisani? au katiba mpya?

10. namba kumi nakubaliana na wewe.
Asante
 
Kuna siku walikua wanachangisha michango wajenge kanisa...bas ikaandaliwa sherehe na mm siku hiyi nikaalikwa nikaenda...yaan siwez sema ni ushamba ila michqngo inachangishwa kwa njia chafu balaa..
Anachaguliwa mwanamke mwenye msambwanda...iwe ameolewa au hajaolewa poa tu....anawekewa mziki....anaanza kata mauno..kwahy men anayetaka kumshika kiuno lazima atoe hela ndefu...imagine...au anachukuliwa mke wa mtu na mume wa mtu anasema leo wangari hatarudi hom kwa mumewe had nipewe laki 5..bas hapo zitachangwa laki 5 ! Mie sion upako kabisa jamani...aibu mno...wanaume wanabambia tu wanawake kisa eti wamelewa...niliudhika
Hivi ulishaacha kusali kwa D. Maboya!!???
 
Kusali ni muhimu, lakini baadhi ya tabia na sheria za baadhi ya makanisa yanachangia sana kuvunja moyo watu kuabudu.

Naomba mwenye kujua kanisa lolote lenye sifa zifuatazo ili nijiunge;
  1. Liwe ni kanisa la kikristu
  2. Liwe na mfumo wa kitaasisi (yaani management iwe kimfumo wa kitaasisi)
  3. Liwe linapatikana angalau kila wilaya/mkoa
  4. Misingi ya waumini wake iwe ni ile ya teamwork (umoja bila kubagua masikini au tajiri hususani wakati wa matatizo ya mmoja mmoja)
  5. Liwe ni kanisa lisilotegemea uwepo wa mchungaji/kiongozi mmoja
  6. Liwe ni kanisa lenye ratiba maalum ya kuzingatiwa (standards)
  7. Liwe ni kanisa linalojali malezi ya watoto kiroho
  8. Liwe ni kanisa la watu wenye akili timamu.
  9. Liwe ni kanisa lenye kupenda haki, usawa na uwazi
  10. Liwe ni kanisa linaloponya, kukuza na kujenga imani kwa waumini wachanga n.k
Yoyote anayefahamu kanisa lenye hizo sifa anifahamishe!! Natafuta kanisa la kujiunga!
Mkuu; Kwa nini unahangaika? Mbona Hilo kanisa unalo tayari na liko hapo nyumbani kwako unapoishi?. i.e FAMILIA YAKO ndo kanisa la msingi (Baba, Mama na Watoto). Nje ya hapo mjomba utakutana na makwazo mengi e.g. Fungu la kumi, Malimbuko, Toa ndugu, Bahasha ya Maendeleo n.k. n.k.
Kanisa Hili ni Kanisa ambalo Makanisa yote unayoyajua na usiyoyajua yanatokea hapo. Ni Kanisa linalonyumbulika(Flexible). Kumbuka Hata Mitume wote maarufu (Yesu Kristo, Mohamad S.a.W n.k.) walitokea katika kanisa hilo. Taasisi hiyo ni ww tu ndo utakayeifanya iwe kama utakavyo. Nje ya hapo Taasisi yako hiyo ina uhuru wa kupokea au kukataa(Kutupilia mbali) ushauri na maoni au mapendekezo kutoka Taasisi/Makanisa mengine wakiwemo na watu Ndg, Jamaa, Marafiki n.k.- Full Stop. Zingatia kwamba hii ndo Taasisi ya Ki-Msingi aliyoiunda Muumba wetu(Mola wetu) kwa maana ya Adam,Eva/Hawa na Watoto wao Kaini na Habili.
Nakubali/Nakaribisha kusahihishwa au kukosolewa.
 
Asante kwa mawazo chanya
 
Kanisa la nini? Tumia akili yako katika imani. Imani yako ipo moyoni mwako, mtafute Mungu wa kweli, dini ni magumashi tu! Basi nenda ukatoe sehemu ya kumi ukashibishe matumbo ya wajanja.
 
Kusali ni muhimu, lakini baadhi ya tabia na sheria za baadhi ya makanisa yanachangia sana kuvunja moyo watu kuabudu.

Naomba mwenye kujua kanisa lolote lenye sifa zifuatazo ili nijiunge;
  1. Liwe ni kanisa la kikristu
  2. Liwe na mfumo wa kitaasisi (yaani management iwe kimfumo wa kitaasisi)
  3. Liwe linapatikana angalau kila wilaya/mkoa
  4. Misingi ya waumini wake iwe ni ile ya teamwork (umoja bila kubagua masikini au tajiri hususani wakati wa matatizo ya mmoja mmoja)
  5. Liwe ni kanisa lisilotegemea uwepo wa mchungaji/kiongozi mmoja
  6. Liwe ni kanisa lenye ratiba maalum ya kuzingatiwa (standards)
  7. Liwe ni kanisa linalojali malezi ya watoto kiroho
  8. Liwe ni kanisa la watu wenye akili timamu.
  9. Liwe ni kanisa lenye kupenda haki, usawa na uwazi
  10. Liwe ni kanisa linaloponya, kukuza na kujenga imani kwa waumini wachanga n.k
Yoyote anayefahamu kanisa lenye hizo sifa anifahamishe!! Natafuta kanisa la kujiunga!
Kwani wataka kulinunua? Si uanzishe lako tu Mkuu?
 
Kipindi nipo advance kuna haya makanisa mawili niliyaelewa vyema (kwa upande wangu )maana waumini wake nilivyokuwa nawaona wapo vyema sana

1. Reformers SDA
2. Full gospel🙂
Hata hawa wako poa sema mafundsho yao meng muda mwingi ni ya ku-critisice dini wengne badala ya kufundshana neno la Mungu binafsi
 
Mkuu karibu sana pale Jesus derivarance church linapatikana mabibo mwisho liko nyuma ya reli inayoelekea tabata ya train za mwakyembe, jaribu kuhudhuria ibada mojawapo jumapili moja, utakuja kunipa mrejesho
hamna kitu huko..huko hamna tofaut na kwa Gwaj
Wanadai wanafufua watu huku kaahndwa kumfufua pot mwenzake
 
Back
Top Bottom