Anayefahamu Simba imechukua kombe gani mpaka sasa anisaidie

John Gregory

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2019
Posts
1,137
Reaction score
2,147
Habari wakuu.

Huwa ninasikia tu hii kilabu inasajili wachezaji, inashiriki michuano na ligi mbali mbali lakini mbona sijawahi kusikia imeshinda taji/kombe lolote? Ina maana wamekuwa washiriki na wasindikizaji tu?

Si Ligi kuu, Si FA, Si Ngao ya jamii, CAFCL,CAFCCL wala mapinduzi. Nini kifanyike ili kilabu hii iweze kupata walau taji/kombe moja japo Ndondo cup?
 
Kombe kubwa walilolichukua simba ni kumtandika horoya miko saba bin sufri ile ya daima nyuma kutoka utopoloni
 
Hata lile 1 tulilokuwa nalo la Mapinduzi tulilipoteza kule Zanzibar
 
Umezaliwa lini?

Je wajua?

Simba ndio klabu yenye makombe mengi ya jumla kuliko klabu yoyote Afrika Mashariki, ikiwa na vikombe rasmi vya kimashindano 58. Hakuna klabu yoyote zaidi yetu yenye mataji rasmi 58 kwenye nchi za Afrika Mashariki. Pichani baadhi ya makombe
 
Ebu tutajie hayo Makombe!

Utasikia alikuwa Bingwa wa kombe la Hedex,
Kombe la Panadol, Kombe la MO, Kombe la miaka 10 ya CCM, kombe la miaka 30 ya Uhuru wa Tanganyika, nk.
 
Ni kombe gn kati ya hayo uliyoorodhesha hapo juu mnyama mkali hajawahi kulichukua kibsbe?
 
Hata lile la mtani jembe halijui masikini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…