ANAYEHITAJI KUWEKEZA WKENYE MICROFINANCE AWASILIANE

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Wana JF secta hii ya Microcredit ni nzuri sana, kuna fursa kwa anayehitaji kuwekeza kwa masharti ya kwamba

1. awe na mtaji wa sh 400,000 - 1,000,000, kila sh 100,000 atapata faida ya sh 5,000 kwa mwezi 1 na nusu,
2. kuwekeza kuwe kwa mwezi 1 na nusu tu kama jaribio la kuona kama ataweza kuendelea au kuacha,
3. akubaliane na masharti ya taasisi husika kwa kipindi cha mwezi 1 na nusu kwanza.
4. yeyote anaruhusiwa kuwekeza kwa mwezi 1 na nusu kwa kiasi hicho kwa mkataba na bima.

Taasisi imesajiliwa na inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, wateja wamekuwa wengi kiasi kwamba wanahitaji wawekezaji, unahakikishiwa kuhusu uwekezaji na ulinzi wa mali kwa kipindi hicho. kiwango hicho ni kuwawezesha watu wa chini na wa kati ambao hawawezi kuwekeza kwa mambo makubwa.
Asiye na uwezo wa kuwekeza na asiyehusika asi comment kisicho mhusu. Njoo PM kwa majibu ya maswali zaidi na maoni pia yatapokelewa.

Mod One Mod Anthony Mod Two Moderator msaada badilisheni title isomeke:
ANAYEHITAJI KUWEKEZA KWENYE MICROCREDIT AWASILIANE NASI
 
mkuu nakushauri ungefanya kuuza hisa hio ndo mm naiona n nzuri tofauti na hii unaonekana ka tapeli flan iv
sidhani kama umeelewa kivile, habari ya kuuza hisa ni kitu kingine, hii inakuwa kama vile wananikopesha mimi kwa dhamana flan halafu nawalipa si vinginevyo.
 
sidhani kama umeelewa kivile, habari ya kuuza hisa ni kitu kingine, hii inakuwa kama vile wananikopesha mimi kwa dhamana flan halafu nawalipa si vinginevyo.
Yuko sahihi sana wewe ndio hujamwelewa, pili nadhani leseni yako ya Microfinance kama umepewa kibali cha Bank kuu haikuruhusu wewe kukopa tena kwa watu ili tena uwakopeshe wateja wako (sina hakika), ushauri wa De Play Boy ni mojawapo sahihi ya wewe kupata fedha kwa kuuza hisa au hati fungani(Bond)
 
ukiwa tayari kuuza hisa naomba ni pm ndugu yngu
 
kwa staili yako hii hupati mtaji, weka mambo wazi, mwaga hisa
 
Unawekezaje kwa kukukopesha wewe? Ni vzr kwamba umetaka kuondoa risk kwa huyo atayekuja kushirikiana nawe lakini kwa msingi huo huo sio uwekezaji! Uza vipande vya mtaji kama unataka watu wawekeze au ukachukue mkopo bank
 
kumbe unataka kukopeshwa
bas nenda benki kakope tu ndugu yangu
 
kumbe unataka kukopeshwa
bas nenda benki kakope tu ndugu yangu
Si hitaji kukopeshwa, micro credit ina mtaji mkubwa nlichotaka ni kuwaunga wengine kwenye biashara si vinginevyo
 
kwa staili yako hii hupati mtaji, weka mambo wazi, mwaga hisa
sihitaji mtaji, hatuna lesseni ya Benki kuu tuna lesseni ya mamlaka zingine sisi sio benki, Benki kuu pekee ndio inatoa leseni kwa mabenki, tulielekezwa kupata lesesni sehem husika na benki kuu
 
Duh..Aisee hivi hujui mpaka mabenki yanakopa?.... Mfano CRDB bank wanakopa AfDB.....
 
Nimeipenda hiyo, ila hebu ngoja nione maoni zaidi humu ya Wadau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…