ufumawicha
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 504
- 209
Ni miezi mitatu nimehamia kikazi hapa jijini Mbeya.Tatizo ninasumbuliwa na tumbo linaniuma sana.Huwezi amini maumivu yamefika kiunoni na mgongo wote hadi shingoni.Nimeenda pale rufaa wamenifukuza eti sina barua ya rufaa wakadai niende mkoani nako sikupata huduma yoyote.Naomba mwenye kujua hospitali yoyote anijuze hata kama ni ya private.Nimeshajaribu na dawa za fadhaget zile za tiba lishe ajabu ndiyo zimeongeza tatizo.Nisaidieni wadau!