Anayejihusisha na hisa tubadilishane mawazo

mr_stev001

Senior Member
Joined
Feb 4, 2023
Posts
159
Reaction score
220
Habari ndugu zanguni,

Mimi najihusisha na DSE naomba kama kuna anayejihusisha pia na hisa, tujuane tuweze kubadilishana mawili matatu.
 
Natafuta ABC za DSE ili ninunue hisa
Hebu share uzoefu wako hapa
Kampuni zilizooridheshwa, zinazotoa gawio nono, madalali/brokers na ishu zingine
 
Natafuta ABC za DSE ili ninunue hisa
Hebu share uzoefu wako hapa
Kampuni zilizooridheshwa, zinazotoa gawio nono, madalali/brokers na ishu zingine
1. Kwenye soko la hisa huwezi nunua hisa direct, lazima utumie hao madalali mf. Solomon stockbroker ltd, core securities ltd nk
2. Utawasiliana na dalali, utafunguliwa account maalaum ikiwa ni pamoja na kujaza fomu na kulipia hisa unazotaka kwenye kampuni ambazo ziko listed dse mf. Crdb, dse, jatu, nmb, tbl nk
3. Dalali ataweka hela kwenye account maalum ya benk kwa ajili ya kununua na kuuza hisa
4. Dalali ataweka oda yako kwenye mfumo ya kununua hisa kwenye soko la hisa
5. Bei unayotaka kununulia hisa zikifanana na ambaye anauza atakuwa amekukunulia hisa hizo.
6. Baada ya kufanya mabadilishano hayo katika mfumo utapewa cheti cha kusibitisha kuwa wewe ni mwekezaji wa kampuni hiyo

7. Ukita kuuza utawasiliana na dalali, kisha process nyingine zitafata
NB. Ukinunua hisa utakuwa unapata gawio na faida nyinginezo kulingana na idadi ya hisa ulizonazo
 
nadhan inawezekana kwakuwa ile nibiashara so unaweza kununua nakuuza hisa zako ukapata faida
 
HApa naweka kambi.
Natamani kujua kama tz pia kuna zile pools ambazo zinakua na hisa from kampuni mbalimbali na pia kuhusu gawio.
It might be a good investment kama kuna legitimacy na good returns.
 
Mfano :-
Nikiweka million 100,kwa mwaka naweza kuambulia kiasi gani? (highest pay company)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…