Shida yangu ni hali mbaya ya wengi wetu kiafya, kielimu, kijamii na yote haya yanasababishwa na uchumi wetu kuwa mbaya ilhali tuna utitiri wa mali ghafi, tuseme ukweli, nchi imezungukwa na maziwa na mito, lakini bado kuna sehemu hakuna huduma ya maji safi na salama, ardhi kubwa tuliyojaaliwa bado kuna sehemu hazina chakula cha kutosha, elimu yenye manufaa haitolewi badala yake tunakaririshwa mambo ambayo mtu anamaliza chuo anazurura na makaratasi kazi hakuna na hawezi kujiajiri, tuna mifugo ya kutosha leo mtu kula nyama ni anasa, bahari na maziwa tuliyo jaaliwa tunashindwa hata kula samaki. Kuna mtu analipwa 20,000,000/- kwa mwezi na kuna mwingine analipwa 100,000/- kwa mwezi, huoni tunashindwa hata kujipangia vipato vyetu na ndiyo maana ruhswa inaongezeka, uminywaji wa haki unaongezeka, hali ya usalama siyo nzuri sana kwani bado watu wanaibiana vitu vidogovidogo.
Mandeleo ya mtu mmoja mmoja ukiyaangalia nyuma ya pazia utakuta kuna uvunjifu wa sheria mpaka mtu ndiyo aweze kutoboa, lakini kihalali tusidanganyane huwezi kutoboa kama si mwizi au ukashirikiana na wezi. Nchi kama Kenya imejitengeneza kimaendeleo katika miundo mbinu na kibiashara lakini sasa iangalie hao wanasiasa wanavyoifikisha Kenya yao.