Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Lusubilo Mwakabibi aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, alitimuliwa kwenye kazi hiyo na kushitakiwa Mahakamani kwa Uhujumu uchumi, ambako aliachiwa kwa dhamana huku kesi yake ikipangiwa tarehe nyingine.
Tangu hapo hatujawahi kusikia tena kama kesi hiyo iliendelea popote , Je na yeye kapata nafasi kwenye Plea bargain?
Kwa wasahaulifu na wale wageni hapa jf ni vema tukawakumbusha kidogo, Lusubilo Mwakabibi ambaye ni mzaliwa wa Mwakaleli huko Rungwe , alikuwa DED wa Kakonko, na baada ya kupora uchaguzi wa marudio wa ubunge kwa kumdhulumu mgombea wa Chadema na kumtangaza Mgombea wa ccm chini ya kikosi cha askari 400 wa Polisi, Usiku huo huo 'akapandishwa cheo' na Rais Magufuli na kuhamishiwa Dar es Salaam, manispaa ya Temeke.
Ni mmojawapo wa wale Wakurugenzi waliojinunulia yale Ma V8 ya bei mbaya nje ya bajeti halali , hata hivyo aliachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote, lakini baada ya Magufuli kuondoka akatumbuliwa.
Kwa kufupisha stori hii tunaomba yeyote mwenye taarifa za kesi ya mtu huyu iliyofunguliwa na Jamhuri ikihusisha ufisadi wa ujenzi wa barabara huko Kijichi kwa kuongeza sifuri kadhaa kwenye hela iliyopangwa basi atuwekee hapa ili nasi tufahamu ilipofikia.
Natanguliza Shukrani.