Anayejua ilipofikia kesi ya Uhujumu Uchumi iliyomkabili Mwakabibi aliyekuwa DED wa Temeke atuambie

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Lusubilo Mwakabibi aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, alitimuliwa kwenye kazi hiyo na kushitakiwa Mahakamani kwa Uhujumu uchumi, ambako aliachiwa kwa dhamana huku kesi yake ikipangiwa tarehe nyingine.

Tangu hapo hatujawahi kusikia tena kama kesi hiyo iliendelea popote , Je na yeye kapata nafasi kwenye Plea bargain?

Kwa wasahaulifu na wale wageni hapa jf ni vema tukawakumbusha kidogo, Lusubilo Mwakabibi ambaye ni mzaliwa wa Mwakaleli huko Rungwe , alikuwa DED wa Kakonko, na baada ya kupora uchaguzi wa marudio wa ubunge kwa kumdhulumu mgombea wa Chadema na kumtangaza Mgombea wa ccm chini ya kikosi cha askari 400 wa Polisi, Usiku huo huo 'akapandishwa cheo' na Rais Magufuli na kuhamishiwa Dar es Salaam, manispaa ya Temeke.

Ni mmojawapo wa wale Wakurugenzi waliojinunulia yale Ma V8 ya bei mbaya nje ya bajeti halali , hata hivyo aliachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote, lakini baada ya Magufuli kuondoka akatumbuliwa.

Kwa kufupisha stori hii tunaomba yeyote mwenye taarifa za kesi ya mtu huyu iliyofunguliwa na Jamhuri ikihusisha ufisadi wa ujenzi wa barabara huko Kijichi kwa kuongeza sifuri kadhaa kwenye hela iliyopangwa basi atuwekee hapa ili nasi tufahamu ilipofikia.

Natanguliza Shukrani.

 
Lusubilo mwakabibi alipita kibondo kakonko then Temeke km DED nadhan plea bargain ishafanya kazi yake na kwa sheria hiyo ilivyo ni kapuku tu atakayefungwa (nje ya mada Mwakabibi alifanya kazi nzuri kutokumtangaza Elia michael maana tungepeleka kituko bungeni kwa sasa pamoja na kuwa katibu tarafa amekuwa kituko cha karne huko kakonko
 
Sasa Plea bargain ishaanza kuwa siri tena ?
 
Tusubiri waje ila kesi ni safari ndefu yahitaji ushahidi makini ....tusubiri
 
😂😄😁😆😅😆😁😁😄Kapuku Na Sakara Ndiyo Watapata Tabu Mno
 
Alikutwa hana kosa yeye ni tofauti na yule konyagi boy aka makengeza aliyenyoosha mikono juu na kuomba msamaha

USSR
 
Mwakibibi ni ndugu yako, nyinyi wote ni vijana wa Kyela. Muache tu aendelee na maisha.
 
Babu ana Sachi atakuja na mrejesho hivi punde🤔
 
DPP ANASEMAJE KUHUSU PLEA BARGAINING MZEE HAJAANDIKA BARUA MAANA DPP ANATAKIWA NAE AKUSANYE MAPATO SAFARI HATA MAFISADI WATAACHILIWA WOTE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…