Nani saa hizi anawaza nini kinachoendelea kuhusu uhaba wa chakula na mifugo inayokufa?
Nani saa hizi anawaza kuna wahitimu wa vyuo vikuu wa mwaka 2015/2016 wamenyimwa vyeti kutokana na bodi ya mikopo kutolipa ada?
Nani saa hizi anakumbuka kuna vijana wamekosa mikopo na saa hizi wanasota mitaani?
Nani saa hizi anawaza kuna vijana wamemaliza vyuo na wamekosa ajira?
Nani saa hizi anawaza kuna watumishi hawajaongezewa mishahara?
Nani saa hizi anawaza kuna watumishi hawajapandishwa vyeo?
Nani saa hizi anakumbuka kauli kuwa serikali haina shamba?
Nani saa hizi anakumbuka kuna wanafunzi walisitishiwa ufadhili wa masomo nje ya nchi?
Nani saa hizi anawaza wanafunzi wa kidato cha kwanza wanatakiwa kufanya mtihani wa mchujo kuchagua wanaotakiwa kuendelea na masomo na watakaofeli imekula kwao?
Nani saa hizi anawaza kuhusu matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne kwa mkoa wa Dar-es-salaam?
Nani saa hizi anawaza nini kinaendelea huko Chato?
Nani saa hizi anawaza kuhusu biashara zinazofungwa?
Nani saa hizi anaongelea tena habari za uchumi kuyumba?
Nani saa hizi anaongelea swala la bei ya unga?
Swala la shisha limeishia wapi?
Kampeni ya usafi nchi nzima imeishia wapi?
Ni lini tumewahi kuwa na live coverage kujadili au kuongelea maswala kama ya kupanda bei za vyakula,biashara kufungwa,mizigo kupungua bandarini, upungufu wa chakula,n.k.
Ni kweli tatizo la madawa ya kulevya ndio tatizo kubwa kuliko mengine yote?
Nguvu hii ya kupambana na madawa ya kulevya mbona hatuioni katika kuwatafuta wanaotuhumiwa kuochota mabilioni ya Escrow kupitia benki ya Stanbic?
Mbona CCM mkoa wa Dar-es-salaam hawakujitokeza kwenye vyombo vya habari kuongelea swala matokeo mabaya ya mkoa Dar-es-salaam kama walivyofana leo?
Kama hii ndio ilikuwa agenda,mbona kamishina wa Tume ya kudhibiti madawa ya kulevya alikuwa hajateuliwa siku zote hizo?
Tume hii imetengewa fedha kiasi gani katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 ili kupambana na biashara hii?
Likiisha hili tusbiri tukio lingine.