Mkuu wetu haheshimu katiba, haheshimu uhuru wa bunge, mahakama hata taasisi za serikali yake mwenyewe. Yeye huingilia na kuamrisha watu/taasisi zifanye mambo kwa utashi wake yeye na sio kwa weledi na taaluma zao.
Mifano:
1. Ni mchumi gani, aliyesoma chuo gani ambaye kamshauri mkuu kuwa pesa inatakiwa “irudi serikalini”, kuwa serikali itumie pesa zake kwenye makampuni yake yenyewe wakati tuko kwenye uchumi huria na sio ule wa kijamaa uliotushinda? Kuna mtu anaweza sema mchumi mshauri wa jambo hilo yupo?
2. Wote mnakumbuka watendaji wake mbalimbali walivyokuwa wanahaha kuelezea uhalali na sababu za kukataza bunge live, lakini majuzi hapa (sijui aliteleza?) akathibitisha kuwa actually yale yalikuwa maamuzi yake yeye na sio wao kwa sababu zingine tofauti kabisa na zile tulizopewa
3. Mara kwa mara anatembelea mahala na kuahidi kuwa ataleta pesa, wakati pesa hizo haziko kwenye bajeti! Maana yake ni kuwa huko atakakozichomoa kuna mtu atalazimishwa aende kinyume na bajeti iliyopitishwa na bunge! Kuna manunuzi kama ya ndege n.k ambazo hatujui zilipitishwa na kikao kipi cha bunge. Na hata maamuzi kama ya kuhamia Dodoma serikali ilipanga mpaka tarehe za kuhamia wakati suala lenyewe hata bungeni halikuwa limefika. Obviously walikuwa na uhakika kuwa bunge linge rubber stamp tu na hakutakuwa na mjadala.
4. Polisi wanazo taratibu zao za kupandishana vyeo, sidhani kama kutukanana na mke wa waziri ni ushujaa unaotosheleza askari kupandishwa cheo, lakini mkuu kaingilia hapo na kuamuru mtu huyo apandishwe cheo kwa kuwa tu yeye kafurahi. Ieleweke kuwa kupandishwa cheo jeshini huwa actually ni jambo la wanajeshi wenyewe baada ya kukidhi vigezo vyao vya kijeshi, na rais hupelekewa tu majina, kama ambavyo misamaha ya rais haimaanishi ni rais huwa anachagua nani wa kumsamehe personally, ila analetewa majina na jeshi la magereza yeye apige saini. Huku ni kuingilia taasisi. Hii haina tofauti na madikteta waliokuwa wanagawa vyeo kwa watoto wao, hali iliyolazimu wanajeshi professionals wampigie saluti mtoto wa miaka kumi aliyewazidi cheo!
5. TRA ndio wanaohusika na kodi, wamekamata makontena ya Azam kwa sababu zao za kitaalamu, Azam hawakupinga na hata jamii hatukujua kwa kuwa ni michakato ya kawaida tu ya kodi. Lakini mkuu wakati anazindua kiwanda cha Azam katoa agizo kuwa makontena yaachiwe! Nani ajuaye ni makontena mangapi yanaachiwa kwa amri/memo zake? Kontena zinaachiwa kwa kuwa TRA wamelipwa au zinaachiwa rais akiagiza ziachiwe kwa kuwa siku hiyo kaamka vizuri?
6. Polisi ndio wenye dhamana kikatiba ya kulinda amani nchini. Polisi kwa taaluma na weledi wao hawakuona hatari yoyote, hawakuona uchochezi wowote kwa wanayanga kusafisha gari la Manji wala kwa wafuasi wa Gwajima kuimba mapambio. Lakini yeye kwa kuwa kaudhika alitaka polisi wakamate wote mpaka gari liende ndani! Kwa sheria ipi ambayo ilivunjwa, anajua yeye! Wote tukasikia kesho yake polisi wakapiga marufuku ya mikusanyiko vituoni! Ni wazi kuwa matamko/maagizo haya si kutokana na polisi kudhani kuwa kutakuwa na uvunjifu wa amani au uchochezi nk, bali tu ni kwa sababu mkuu hataki! Kama kungekuwa na hatari yoyote ile, hilo lingetakiwa kusemwa na polisi na sio yeye mwanasiasa hata kama ni bosi wao. Hivi ni nani mwenye akili timamu anayeweza kudai kuwa mkuu ana utaalamu wowote ule wa kuona uvunjifu wa amani kumzidi kamanda sirro!?
7. Miradi inatolewa kwa contract, contract inaainisha wajibu wa kila upande, lakini mtu anavamia eneo la mradi na kuutangazia umma kuwa “tumepigwa”, kwa utaalamu upi? Hivi ni kweli ukiwa waziri wa ujenzi unakuwa mtaalamu kiasi cha kupima thamani na ubora wa mradi mkubwa kama airport terminal kwa kupiga hatua kama unapima shamba la mihogo? Kwa nini ushahidi usipelekwe kwenye bodi iliyotoa tenda, na kwenye taasisi inayoshughulikia masuala ya tenda za serikali? Ili pamoja na yote sheria ichukue mkondo wake?
Mifano hiyo michache ni ile ambayo Mungu ametupa neema ya kujua kuwa ni mwenyekiti ndio aliyeamua iwe hivyo na sio wateule wake. Kwa mifano hii tunapata mwanga wa hii “roho ya wendawazimu” ambao imegubika watendaji. Wengi tulikuwa tunashangaa watu wenye taaluma zao awamu hii wote wameingiwa na “wehu”, wanakuwa na maamuzi ya ajabu ajabu ambayo hayaendani na wao wenyewe. ("people at the top aren't thinking rationally anymore" - Lissu). Hivi mtu mwenye Phd ya sheria (tena ya katiba) ni mtu wa kulumbana naye juu ya haki ya vyama vya siasa kufanya siasa? Hivi polisi anayesimamia sheria ni mtu wa kupiga watu virungu kwa kumsalimia Lowassa? Sheria juu ya kukataza umiliki wa .com yametokana na wahandisi wa TEHAMA kweli? Uweledi kuhusu ofisi ya mwanasheria mkuu juu ya kesi za ajabu ajabu kwa wapinzani? Majibu ya maswali yote haya ni kuwa hawa watu wanaendeshwa kutoka juu kama kwenye hiyo mifano yangu.
Hivyo katika hili la cloudsgate, mimi nadhani tuangalie upande mwingine. Bashite ni tatizo lakini sio tatizo kuu. Nashawishika kuamini kuwa cloudsgate imefanyika with full blessings kutoka kwa mkuu. Mkuu alikuwa anajua, na ni mkuu ndio alietoa go ahead. Siku chache tu zilizopita mkuu katangaza mapenzi yake juu ya kipindi kilichovamiwa, watanzania lazima watakuwa na hamu ya kukiona kipindi anachopenda mkuu kinafananaje. Kama mkuu alitamani hata awe IGP ili tu awasweke ndani waimba kwaya wa Gwajima unadhani hawezi ku –okay mteule wake yule yule adui wa Gwajima achukue wanajeshi waende clouds ili wakamchafue Gwajima kwa kutumia kipindi kile ambacho kina presidential status? Mkuu wa mkoa anapata wapi kikatiba madaraka juu ya wanajeshi? Hayo madaraka juu ya jeshi la sirro tu ni ya kulazimisha sana, kikatiba hayapo!
Mpaka sasa kuna ushahidi wa kutosha at least kumuweka pembeni Bashite kutokana na masuala ya forgery ya vyeti, conflict of interest kwenye masuala ya madawa ya kulevya na utata wa mali zake. Lakini mpaka sasa hamna kitu. Kelele juu ya forgery za Bashite zilikuwa zinaishia hewani baada ya kufanya sherehe ya kujipongeza mchana kweupe!
· Ukitazama footage na maelezo ya kilichotokea utaona jinsi Bashite anavyojiamini. Kujiamini kwake kumepitiliza kujiamini kwa kawaida kwa mvunjaji sheria. Huku ni kujiamini ambako kunatokana na uhakika fulani kuwa hakuna shida yoyote kutokana na yanayofanyika. Isingekuwa CCTV footage , hii kashfa nzito ingeishia kuwa another rumour humu JF. Na maneno ya wahanga wote yangepuuzwa tu. Na hii ndio sababu naona tayari upepo umeshabadilika, waziri kafuta akaunti yake nzima ya twitter ili kujidistance na tweet aliyotoa kwa sababu ameshaona uwezekano wa Bashite kuwa na baraka za mkuu katika jambo lile. Mtu aliyevamiwa hawezi yeye ndio apelekwe vituo mbali mbali vya polisi kuhojiwa wakati aliyemvamia ni mapolisi hao hao! Huyo mhanga kaitwa kuwekwa sawa ili asije “kuichafua” serikali na labda ajieleze ni kwa nini wamerusha CCTV footage inayomuonyesha RC “kinyume na sheria” au “kiuchochezi” kwa mujibu wa sheria ya mitandao???
Kwa vile CCTV footage imeharibu mambo, Bashite will have to take one for the team. Lakini tusahau kuhusu makosa ya jinai ya kufoji vyeti, makosa ya jinai kuhusu rushwa na matumizi mabaya ya madaraka (the so called vita ya madawa ya kulevya), uchunguzi juu ya mali zake n.k, most likely ataambiwa ajiuzulu au atawajibishwa kwa maadili ya utumishi au any other “slap on the wrist”, halafu maisha yataendelea. Bashite hajafanya lolote kubwa zaidi ya wakuu wa wilaya waliosweka ndani waandishi wa habari na madaktari na hakuna lolote lililofanyika. Tofauti hapa ni hii CCTV footage. Hata Bashite akiondoka, tunabaki na tatizo kubwa zaidi ambalo ni mkuu.