Mkuu unakaa wapi!? Mbona hiyo bei yako ya sukari kubwa sana!? Na unga umeshaanza kushuka bei..Sukari imefika 3200 na unga wa mahindi 2200, where are we going????? Masikini wanaendelea kuwa masikini zaidi, na washangiliaji nao wanajitahidi kumshangilia kwa kila jambo.
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.
Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.
Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu
Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?
Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.
Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Ha ha ha ha sasa ulitaka iende mbele?Mimi niko ndani ya Lori la mkuu nashangaa miti inavyorudi nyuma....
Ongezeni kumwombeaAmefeli nje ya uwanja
Mbona siona hoja hapa ktk andiko lako . . ?!Rais anatupeleka tunakopaswa kwenda, na anachojaribu kufanya ni kujenga msingi wa kitu kinaitwa the Development State Model. Kwa sasa anajaribu kusahihisha makosa tuliyoyafanya huko nyuma ili kujenga msingi imara. Hata mataifa yaliyoendelea yaliendelea kwa sababu yalithubutu kurekebisha makosa yao na kusonga mbele. Kila anachofanya rais ni katika kuhakikisha kuwa tunaweka mambo sawa ili tuwe na msingi wa maendeleo. Kwa mtu yeyote mwenye uelewa ataelewa ninachojaribu kusema. Na kama rais atapata ushirikiano wa kutosha nchi itasonga mbele. Tatizo la walio wengi tunapinga kila kitu kwa kujua au kutokujua.
Mbona siona hoja hapa ktk andiko lako . . ?!
Kujenga DEVELOPMENT STATE MODEL ndio kudhibiti uhuru wa vyama vingine vya siasa ?! Au ni kudhibiti Uhuru wa habari na vyombo vya habari . . ?!
Hebu toa definition ya hii DSM uliyotaja . .
Hii ni dharau au kejeliTeh..teh...Maimamu wa karibu misikiti yote Dar es salaam baada ya kupewa "FUTARI" na Bashite mawaidha yao mengi ni kumuunga mkono Magu na utawala wake.Inakumbushia zile milioni kumi kumi waluzopewa wabunge wa CCM.Maimamu wa Dar bei rahisi sana
Nasubiri siku Bashite awaite Pengo,Malasusa,Shoo,Gwajima,Kakobe Lusekelo nk..awagaie mchele na sukari ..
Hii ni dharau au kejeli