Mmenielewa? maana naona toka aanze kuchaji hainyeshi kupata hata kijiwe kimoja.
Jamani, katumbua majipu hatujaona usaha, sijui unabaki ndani?
Wafanyakazi Hewa kaokoa Shilingi ngapi, hajasema,
Wanafunzi Hewa kaokoa Shilingi ngapi hajasema,
Kazuia Siasa za upinzani, CCM wanafanya Siasa kasaidia kiasi gani CCM kupendwa hajasema,
Sijawahi kusikia toka nianze kujua tunaendeshwa kwa Bajeti kwamba bajeti imeferi kutekelezwa, sio kutekelezwa tu, kutokutekelezwa kwa asilimia 50. yaani 50% sijawahi.
CCM mwambieni awaamini watendaji wa Serikali, awaachie watumie akili zao, awatengenezee sheria za kuwabana sio kuwabana kwa mabavu.
Mwambieni msimwogope Simu bila Betri ni Sawa na kujipulizia Pafyumu bila kuoga.