Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.

Hivi unaposema " Hatujui" ni wewe na nani? Nani kakutuma umsemee?!!! Au ndiyo kutaka kujifanya mko kundi au kikundi chenye mawazo kama yako?!!! Semea nafsi yako... Kama mpaka sasa huelewi nini anafanya Rais JPM ... Basi tulia fanya shughuli zako za halali lipa kodi stahiki hayo mengine watafanya wanao husika na wewe utaona tu matokeo .....
 
Kujitegemea sio jambo la mzaha .
Kinachofanyika ni kurejesha Maadili na nidhamu ya Taifa Tuweze Kujitegemea.
 
Kama wewe hujachanganyikiwa umechelewa. Ukiwa unachanganyikiwa labda mimi ntakuwa naanza kuelewa tunapoelekea
 
Jamani au mimi ndo sielewi mnieleweshe?? Maana niliyotegemea kutoka kwa Magufuli ni tofauti na ninayoyaona

Nilichokitegemea ni uchapakazi uliopitiliza na mkazo mkubwa katika ukusanyaji wa kodi kutoka katika makampuni makubwa na migodi ambayo ilikuwa ikilipa kodi ndogo na mingine ikiwa hailipi kabisa

Kwa sababu alitwambia tanzania ni tajiri sana na atatumia utajiri wetu kututoa katika umaskin

Utajiri huo ni kama migodi,gesi,maji,mbuga nk

Sasa mbona hatutolei umaskin kutoka kwenye huo utajiri tulionao zaidi ya kuendelea kutukamua sisi maskini?

Kodi kwetu zimekuwa nyingi mpaka kero

Mfano mtu anamiliki mpesa:- analipia reseni tra na pia katika halimashaur husika analipa kodi,kwenye miamala serikali inakata kodi,kwenye malipo anayopata kutoka kwa kampuni anakatwa kodi,hela aliyolipwa akitaka kuitoa kwenye simu anakatwa kodi na sasa akitaka kumtumia mtu itabid akatwe kodi

Huyo mtu mmoja anakatwa kodi tano heeeee!!

Nahisi tutaisoma namba
 
Na mvimbe mpasuke, mtajijua wenyewe, mliipenda wenyewe mkadai kuwa nichaguo lenu milele, acha tuisome namba
 
Ni kweli, wengi mlidhani CCM ni ile ile...mlitegemea atakuwa upandewenu...kamwe haitakuwa hivyo
 
Ujinga ni mzigo kweli; gumia la misumari.
 
Hizo hela wanazohangaika kuandaa maandamano, kufungua kesi ,sisi wanachadema tunapendekeza wajenge ofisi za chama.

Ofisi ya chadema pale ufipa inatia kinyaa
 
Kiukweli,tukubali au tukatae,Nchi haina mwelekeo,hakuna anayejua kesho kuna nini wala hakuna mwenye dira ya kwamba tunaelekea wapi ni mizuka tu ya papo kwa hapo alafu inazima nziiiiiii!!

.....kweliiiii
 
Sukari vepee?
 

Hilo ndio tatzo la watanzania, wao wanataka kila kitu wafanyiwe, hawajui wao ndio wa kufanya, wao ndio wa kubuni cha kufanya. Back in time pale raisi wa marekani alipo waambia wananchi Wake USIULIZE NCHI IKUFANYIE NINI, WEWE NDIO UJIULIZE UTAIFANYIA NINI NCHI YAKO.
My fellow Americans, ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country.
 
Alivyosema zungusha zaidi hamkumwelewa kuwa mtazungushwa mpaka mpate kizungu zungu ccm mlisema mbele kwa mbele sasa ndio mlio kwenye masaburi mnaisoma no.
 
CCM imepoteza DIRA By Horace Kolimba(R.I.P.)
 
Watanzania jana walishuhudia kusomwa kwa bajeti ya kwanza ya awamu ya tano. Kwa vipindi tofauti Rais amekuwa akiomba aombewe kwa mwenyezi Mungu ili atende haki.

Kwa bajeti iliyosomwa jana, naamini kuna haja ya kuendelea KUMUOMBEA ILI ASITUPELEKE KWA NAMNA AMBAVYO BAJETI IMEWATENDA WANANCHI HASA WANYONGE.

1. TUMUOMBEE AACHE KUWAGANDAMIZA WANANCHI WANYONGE.
2. TUMUOMBEE AACHE KUGANDAMIZA DEMOKIRASIA YA USAWA WA SIASA HURU.
3. TUMUOMBEE AACHE KUJIONE YEYE NI FIKRA PEKEE HAPA NCHI NA HAKUNA WENYE MAWAZO MBADALA.


TUMUUOMBEE AWAOGOPE NA ASIWADANGANYE WANANCHI KWA MWAMVULI WA HAKI.
 
Waisalamu watatumia mwezi mtukufu huu kwa kufanya sala kwa ajili yake, wAkristo tusubir kwa rezma tutaomba, walokole waitishe Maombi ya dharula kwa kufunga wiki mojA, kwa ajili ya mh
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…