Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Serikali ya awamu ya 5 kwa maono yangu ndio serikali pekee kupingwa si tu na wapinzani, bali hata baadhi ccm wenyewe, imekuwa serikali ya matukio, kila kukicha inacheza na medias, na kila mpingaji anaitwa fisadi, si mzalendo, eti wanaopinga ni wale wazee wa madili, dah, tupo sie ambao toka tumeanza biashara hatujawahi kuacha kulipa kodi kwa wakati,

ila Kiukweli hali ya maisha ni mbaya sana huku, yani mpk wale kuku wa mayai siku hizi hawatagi tena, mashambani ndio kabisa, tuliozoea kuvuna gunia 50 sasa hivi ni gunia 10 tuu, hv huyu aliyeshushwa ni malaika au and vice verse is true?yani hata wale dada poa hapo kabla walijiuza mpk kwa 50k ila walikuwa wapo kibao, siku hizi wameshusha bei mpk 5k ila kuwapata nao ni tabu
 

Haa haaa mfano wako umenichekesha sana.Kuna mtu mmoja (mungu amrehemu) alikataa Mwl.Nyerere kuitwa Baba wa Taifa,akaendelea kusema kumuita Baba wa Taifa eti ina maana mama zetu wote ni wake zake,ametuzaa,Nchii hii ina vituko sana
 
Ok naweza kujiridhisha kuwa amekuwa akirekebisha mifumo , lakini wasiwasi ni kuwa tayari ameyagusa maisha ya wananchi moja kwa moja. wakati anaingia madarakani sukari ilikuwa 1800-2000 , unga kg 1 sh 1000, mafuta ya kupikia lt 5 sh 12000. hvo ni baadhi ya vitu tu.Kwa sasa bei imepanda mara dufu. Kazi ya kiongozi ni kuboresha maisha ya watu. Ila kwa kiongozi tulienae ni kuteaua na kutengua tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa??????????kuwa serious acha upuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilitegemea kuona sehem alipokosea sana hadi ukaamua kuandika uzi huu... Usiwe kama asilimia kubwa ya waandishi wa tanzania kuchukua habari kwenye mitandao na kuandika bila uchunguzi wa kina. Toa ufafanuzi wapi amekosea sana ili ajue ajirekebishe wapi mana kila mtu hukosea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunalipa kodi ni lazima tuone serikali inatumiaje hela zetu.
 


Mfano wako ni irrelevant, sisi ni watu wazima kuna wengine tunamzidi uelewa wa mambo tofauti, wengine wanamzidi hekima na busara, wengine wamesomea masuala ya uongozi na uchumi yeye hajui uchumi nk nk,

Kwa maana hiyo wanaujuzi zaidi yake anahitaji kushirikiana nao, tofauti na mtoto kwa babaye hata hivyo si kila akisemacho mtoto kwa baba hakifai, kuna wakati mtoto anaweza kuwa wa kwanza kumuona nyoka akikuambia ukamdharau shauri yako lakini amesema.
 

Mpiga deal Mkuu ni yeye mwenyewe.Bilion nane za kivuko kibovu leo tunaambiwa hwafukui Makaburi,ila ya walala hoi yanafukuliwa.Nyumba za Kimara leo zote ziko chini.Nasikia anataka kujenga uwanja wa mpira
 

Wananchi tunajituma sana lakini serikali hii imegeuka ya kinyonyaji badala ya kumsaidia mwananchi pamoja na rasilimali zote tulizojaliwa na Mungu .

Wananchi tunalipa kodi zisizo stahili achilia mbali ubireshaji wa huduma zinazotolewa.ukija kwa watumishi ndio kabisa serikali inataka wafe masikini wanakata mshahara wote mtu anabaki kuvumilia tu huu upuuzi unaofanywa na hii serikali ipo dawa yake inakuja. subirini
 
hivi nyie mnaosema vijana wanashinda vijiweni chakula ni serikali inawapa au huwa wanakuja makwenu kuwaomba chakula? niondolee upuuzi hapa
 
Hebu sema mkuu, wewe binafsi JPM kafanya decision gani mbaya ambayo imeletelea kuharibu maisha yako?Kwa upande wangu mimi, mzunguuko mdogo wa fedha umeniathiri,lakini nimefurahishwa sana na uboreshaji wa miundombinu,kudhibiti wizi wa mali zetu za asili;kupiga vita ufisadi,wizi wa mali za uma,matumizi ya vyeti fake,uzembe sehemu za kazi,rushwa,ukwepaji kodi,matumizi na uuzwaji wa madawa ya kulevya na kuongeza uwajibikaji sehemu za kazi.

Hata hivyo harakati hizo ambazo nimezitaja kwa kiasi kikubwa, naamini ndizo zilizofanya mzunguuko wa hela uwe mdogo.Kwa sababu hiyo sichukii, kwa kuwa najua nia ni njema kwetu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.Najua kwamba kila jambo lina "pro and cons."
 


Angalia na upande wa pili!!! Fuatilia hao wanaoshinda vijiweni alaf uje useme ni watu wa aina gani!!! Wengine wanavyeti kabisaa yaani walipoteza mda mwingi wakiwa mafunzoni ukiangalia na elimu yenyewe sio rafiki kwa kujiajiri na utakuta Hata mazingira rafiki ya kujiajiri hakuna !!!! Sasa kwanini wasilaumu serikali!!!!!

Alaf ww umekuja na msemo uleule kwamba watu hawatafuti visenti wanashinda vijiwen!!!! Umekalili!!! Mi sio mtu wa vijiweni nnashughuri zangu lakin usikalili kuponda wenyevijiwe hujui2 pale wengine wakoje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hiyo mifano yako uliyotoa hapo sijaribu kuamini kama umefika hata kidato cha nne na kupata walau divisheni 4 ya 31.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hujui kuwa maamuzi mabovu ya kiongozi,na kutofuata sera pamoja na ukiukwaji wa katiba ndio umaskini wa mtu?
 
Basi ni kweli wewe ni mpiga zumari wa mfalme kama hujui kinacho endelea mitaani, makazini hata vyuoni! Na kwa taarifa yako hata wale wa mabaka mabaka nao wanalalamikia hali mbaya sana hasa baada ya kufutiwa yale maduka yao yenye nafuu

Huyu jamaa anajikaza lakini rohoni anajijua mwenyewe. Je ndugu zake wanajua kutafuta hiyo pesa? Au ndiyo wale ndiyo mzee. Hapo alipo inawezekana yupo hoi lakini ni wale wa kujigamba.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…