Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mkuu huoni mitandao ilivyochafuka mpaka kenya?
Tutajuaje kama hao ni wakenya....labda ni wantanzania wenzetu wanaoitakia mabaya nchi yetu wameamua kutumia mitandao ya kenya! Wewe hushangai...hao 'wakenya' wanavyotiririka kwa kiswahili kisicho na mawaa jambo ambalo si la kawaida?
 
Naona kila kona,kila mitandao wananchi wamechukia na wana hasira sana kiasi ambacho hakijawahi kuonekana tangu Uhuru

Je kiakili wananchi wameasi utawala wao?
kweli mkuu, hadi vijijini yaani.
juzi kati hapa nilikuwa bush huko Katavi na Tabora. wanavijiji (wengi wao wazee) wanadai wazi wazi kabisa eti ni kama tuko chini ya mkoloni!
 
Sio wote, kuna wengi tu ambao bado wanaaminia utawala, inawezekana wakawa wengi kuliko wanaoponda, labda group hili haujakutana nalo tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaachaje kuwa na hasira na utawala huu wakati mlizoea kutumia vyeti feki makazini!?
Mtaachaje kuwa na hasira na chuki wakati mlizoea kukwepa Kodi na kuibia serikali mapato!?
Mtaachaje kuwa na hasira na chuki na wakati mlizoea kupeana ajira kwa undugu na ukabila!?
Mtaachaje kuwa na chuki na hasira na wakati mlizoea kuiba hela ya umma ambayo ilitengwa kwa ajili ya maendeleo ya kila Mtanzania na kujenga mahekalu huko Mbweni n.k!?
Mtaachaje kuwa na chuki na hasira wakati "mabuzi" yenu mengi yanaisoma namba huko segerea na keko!?
Mtaachaje kuwa na chuki na hasira wakati mlizoea kwenda kufanya semina Dubai kwa hela ya serikali!?
Mtaachaje kwa mfano!?
Mjitafakari......
 
Habari huenea kwa kasi sana mkuu,Mimi hii sijawahi kuona tangu nizaliwe,hakika kabisa
Basi wengine tumeona ndugu na sio huko tu, tumemuona alivyokuwa waziri wa ujenzi, waziri wa uvuvi alipunguza sana uvuvi haramu katika maziwa yetu
 
Mtaachaje kuwa na hasira na utawala huu wakati mlizoea kutumia vyeti feki makazini!?
Mtaachaje kuwa na hasira na chuki wakati mlizoea kukwepa Kodi na kuibia serikali mapato!?
Mtaachaje kuwa na hasira na chuki na wakati mlizoea kupeana ajira kwa undugu na ukabila!?
Mtaachaje kuwa na chuki na hasira na wakati mlizoea kuiba hela ya umma ambayo ilitengwa kwa ajili ya maendeleo ya kila Mtanzania na kujenga mahekalu huko Mbweni n.k!?
Mtaachaje kuwa na chuki na hasira wakati "mabuzi" yenu mengi yanaisoma namba huko segerea na keko!?
Mtaachaje kuwa na chuki na hasira wakati mlizoea kwenda kufanya semina Dubai kwa hela ya serikali!?
Mtaachaje kwa mfano!?
Mjitafakari......
Umenena sahihi wengi walio na chuki wauza ngada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Serikali kuingilia na kuchochea mgogoro wa CUF.

2.Wapinzani mwiba kuadhibiwa sana.

3. CCM kuanza kuomba kujadiliwa suala la Rais kuongezewa muda.

4.Katiba ya CCM kubadilishwa kua Mgombea urais kutokua na washindani wengine.

5.Bunge kukosa meno kwa kukosa usimamizi uliojitegemea kujipambanua.

Kwa sababu wabunge wa CCM wanaweza kuamua chochote kwa sababu ya wingi wao na Spika wa bunge kutojua nini anafanya psina shaka muda utanena.

Tu naweza kuelekea kusikojulikana, mark my words.
 
Watz tu wanafiki sana unakuta watu wanaongea mbovu mbovu ila ghafla wakisikia Msafara unapita wanamwagika kama nyuki barabarani huku wakiimba nyimbo za kusifu na kushangilia ila baada ya hapo ghafla wanaanza tena kuponda....
[emoji23][emoji28][emoji23][emoji28][emoji23] hahahahah
 
Watz tu wanafiki sana unakuta watu wanaongea mbovu mbovu ila ghafla wakisikia Msafara unapita wanamwagika kama nyuki barabarani huku wakiimba nyimbo za kusifu na kushangilia ila baada ya hapo ghafla wanaanza tena kuponda....
Tena wa kiwango cha SGR mkuu.
 
Naona kila kona,kila mitandao wananchi wamechukia na wana hasira sana kiasi ambacho hakijawahi kuonekana tangu Uhuru

Je kiakili wananchi wameasi utawala wao?
Hizi ni sound za mtandaoni tu na mijini, njoo kijijini kwetu utona jinsi wananchi wanavyosia utawala madhubuti wa awamu ya tano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom