Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.

Tatizo na barier kubwa ni elites....walizoea kuishi hayo maisha ya kifisadi sasa yanapobomolewa wanaona kuishi kwakufanya kazi inawahusu wanyonge tu....kwakua ndiyo nguvu anayoitegemea Mh. Rais ndiyo maana kila afanyalo wanali counterfeit kuonyesha ame fail badala ya kumsaidia kwakumpa options za yeye kuchagua ili aweze kuleta mabadiliko huku yakisababisha madhars madogo kwa taifa....

Niwaambie tu, dhamira njema haijawahi kushindwa; pamoja na yote Tanzania njema ni lazima apende au asipende mtu...watch and see!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Watz wakikuamulia utaomba poo.
 

Bahati mbaya kwao ni they have all to loose while we have nothing to loose.....sisi ni zaidi ya washindi...kama tuliwashinda pale walipokuwa na nguvu zote na resources zote tushindwe nyakati hizi tukiwa na nguvu hizi zote? Wata piga magoti na ndimi zao kukiri Yesu ni Bwana!
 
Ameshawashinda ndio maana wanatafuta huruma kwa wananchi alafu wakirud kwa wananchi , wanamuelewa sana Magufuli

Mtaani huku Magu ana 90%....aki establish mahakama ya mafisadi anafikisha 120% ya true voters.....Tutaelewana tu!
 
go go magufuli nyie wengine pingeni tu maana ndo kazi ya wapinzani tukutane 2020
 


Hata muungane wote bado Raisi Magufuli hamumuwezi kwa sabasbu kuu zifutazo. moja, yeye ndiye Raisi wa JMTZ na hakuna, narudia hakuna mwenye uwezo wa kuanzisha vita dhidi ya raisi wa JMTZ na akashinda hata kama Raisi angekuwa ni jiwe bado hakuna mwenye uwezo wa kulishinda, pili na siyo kwa umuhimu Watanzania tuko nyuma ya raisi Magufuli kwa maana tunaamini anachokifanya ni cha lazima kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu, tatu Raisi Magufuli ni genius wewe, Lowasa &Co. ni simple minds labda mnajua kiingereza kwa maana ndicho mlichoenda kujifunza Shuleni lkn akili ya kutatua matatizo hamna ndiyo maana kwa miaka 20 mko upinzani na hamna mlichofanikiwa kila siku mna matatizo yala yale tu , Wanasayansi wanasema na wamethibitisha kwamba ili uweze kusoma science (Fizikia, Hisabati, Kemia na msomo yote yenye ukaribu au uhusiano na haya masomo kama uchumi medicine n.k) unahitaji IQ kubwa above average na nyie wote kama akina Lowasa &Co. mliosomea Sanaa Chuo Kikuu hamuhitaji IQ kubwa kama 80-90 wkt Science unahitaji kuanzia 110, wewe na wenzako akina Mbowe, Lowasa, Msigwa, Zito kabwe wote ni mediocre minds na kamwe hamuwezi kushinda na higher IQ haijawahi kutokea Dunia hii na moja ya sifa ya mediocre minds ni maneno mengi na porojo lkn matokeo ni yale yale ...
 
Ukizungumzia suala la elimu uwe na aibu upande wenu

kwa viakili vyako unadhani magu ni rais wa ccm na ndo maana unaona kuna rais wa upande mwingine! kama raia wenyewe anaowaongoza ndo kama wewe ama kwel kaz anayo
 
kwa viakili vyako unadhani magu ni rais wa ccm na ndo maana unaona kuna rais wa upande mwingine! kama raia wenyewe anaowaongoza ndo kama wewe ama kwel kaz anayo
User name yako tu lazima ili reflect unachozungumza
 
Pamoja na demokrasia kubakwa waziwazi mwaka jana na rais wa kulazimisha kupatikana, Tanzania bado inajikuta kwenye mkwamo watangu enzi!!

Wachache kati ya watanzania waliokuwa na matumaini kidogo na huyu Magufuli sasa wanaanza kujionea wenyewe matumaini yao yanavyodidimizwa!!

Ilianza na sukari na wiki hii tumehamishia maumivu yetu kwenye mafuta ya taa!! Ugumu wa maisha kwa wanyonge bado unaendelezwa kwa kasi mno huku aliyejinadi kuwa ni sadaka kwa watanzania akikosa kabisa suluhu ya kweli ya masahibu haya!!

Ameonyesha kuwa ni Rais asiyejiamini kabisa, rais asiyeweza lolote, Rais asiyekuwa tayari kuvumilia maoni tofauti kwa kuwa anajijua HAWEZI!!

Ni masikitiko yangu kwamba inabidi tuchelewe tena kwa miaka mingine mitano zaidi ndipo tupate nafasi ya chaguzi nyingine ambayo pia ina kila mwonekano kuwa itakuwa UCHAFUZI!!

Mungu mwenye enzi yote okoa waja wako wa Tanzania!!
 
Itakuwa ni maajabu ikitokea siku moja ukapongeza lolote lililo fanyika kwenye serikali hii ya awamu ya tano nitashangaa sana.
 
Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana ! Ni hivi , uongozi mkubwa kama urais ni karama kutoka kwa Mungu , karama hii hailetwi na vifaru .

Mimi nimeshukuru sana kwa haya yanayotokea na naombea Hawa Masikini wa nchi hii waendelee kukomeshwa kwa dhiki na shida nyingi zaidi ili iwe fundisho kwa masikini wengine duniani .

Tumekuwa tukiwaelimisha kwa miaka mingi sana lakini hawaelewi , sasa Mungu kawatandika kibao cha uso waache wakome , asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu .

Adui mkubwa wa nchi hii ni ccm hakuna fukara yoyote wa nchi hii asiyelijua hili , akifuatiwa kwa mbaali na mwovu shetani , lakini wao wameendelea kumkumbatia tu , wacha wakione cha moto .
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…