Formula ya Mafanikio ya kiuchumi nchi hii ni:
TZ Economic Success = JK Economic Policies + JPM Management
Rudisha Kilimo kwanza.
Kilimo ndo uti wa mgongo wa uchumi wetu na ni njia ya uhakika ya Kulift mamilion kutoka katika umasikini. Tukihimiza viwanda kabla ya kuinua pato la mwananchi, Viwanda vingi viyakuwa vya investors na wananchi wataishia kuwa vibarua viwandani badala ya kuwa na capacity ya kuvimiliki.
Rudisha BRN
BRN ni vision, ni namna ya kuanzisha, kusimamia na kuendesha miradi kisomi na kitaalam zaidi. BRN chini ya Presidential Delivery Bureau ilisaidia katika miradi ambayo ni Landmark katika utawala wa JK, miradi kama ya umeme ilikuwa inasimamiwa chini ya BRN na ilikuwa inakwenda vizuri ( I hope bado inaenda vizuri). Kuondoa BRN ni kurudi ktk utaratibu wa zamani wa kufanya business ambao tumeshaona toka enzi za JKN, AHM, BWM kuwa siyo Optimal. Ofcourse matatizo ya BRN lazima yalikuwepo ilipaswa kuyatatua
Peleka Pesa za Serikali kwenye Mabenki ya biashara
Mabenki ni wadau wa maendeleo, wakiyumba na watu wanayumba, Serikali inao wajibu wa kuyasaidia mabenki yawe stable, kwa wenzetu wamarekani wao walikuwa wanayabail out, Sisi kwa kuwa hatuna pesa za kuyapa njia ya kuyabail out ni serikali kuweka pesa zake huko, ila inachoweza kufanya ni kukaa nayo mezani na kunegotiate nayo ili iwepo win-win, kwa mfano mathalan serikali ikitaka kukopa itakopa kwa riba ndogo sana, na pia kwa kuwa serikali imeweka mahela yake mengi huko then pindi Mabenki hayo yakikopesha hizo pesa kwa wadau wengine then serikali ipate percentage fulani nzuri ya faida. Namna hii ni nipe nikupe!. Bila serikali kufanya hivi naamini mabenki yatadorora zaidi.
Wekeza zaidi kwenye Diplomasia ya Kiuchumi.
Pambana kuleta wawekezaji, nenda duniani huko ongea na wawekezaji, tafuta miradi, tafuta masoko ya mazao ya kilimo, tangaza fursa zilizomo nchini, balozi zetu zipimwe kwa investments zinazoletwa nchini
Conclusion
Naamini, sera za kiuchumi za JK na Usimamizi madhubuti wa JPM wa kubana mianya ya rushwa, ufisadi na uzembe vinaweza kutusogeza