Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Uelewa wa mtanzania upo chini sana. Tatizo la pili la mtanzania ni unafiki. Tatizo letu la tatu ni woga. Hizo sifa zetu tatu ndiyo mtaji mkubwa wa Magufuli
Hizo sifa unazo ndo maana unatumia Id fake kufikisha ujumbe wako
 
Hizo data feki umezitoa wapi ,Nani kakwambia umekufa ,ili iweje umeleta Uzi kiushambenga

Uchumi wetu uko imara imara zaidi ya uimara wenyewe


..wananchi wanashindwa kutoa michango midogo-midogo kwa ajili ya elimu ya watoto.

..huo ni ushahidi kwamba wananchi nchi nzima wana hali mbaya kiuchumi, hawana uwezo wa kulipia gharama ndogo-ndogo.
 
Tuwe na subira karibuni tunaingia uchumi wa kati. Abiria wa ndege wanajua,ndege ikianza kuchukua kasi ili ipae,abiria shuruti wafunge mikanda(vyuma),kisha ikifika usawa stahiki hufungua mikanda na kujiachia(Vyuma kulegea) Tuvumilie
 
Wanaotegemea magu ajenge uchumi ni wajinga au wanafiki. Uwezo huo hana, ana uwezo wa kubomoa tu ndio maana tangu aingie madarakani kazi kubwa aliyoifanya ni kubomoabomoa kila mahali isipokuwa usukumani eti kwa sababu walimpa kura za urais!
 
Kazi ya kurekebisha uchumi mbovu ulionguka, ni kama kazi ya kurekebisha nyumba mbovu inayotaka kuanguka, kama nyufa ni ndogo ndogo tuu za kwenye kuta kama zile expansion joints, then zinazibwa tuu na nyumba inasimama, lakini kama nyufa ni kubwa na zimefika hadi kwenye msingi, huwezi kuziziba tuu, itakubidi ubomoe yote, kisha ujenge upya.

Hivyo ndio kinachoendelea sasa, tunabomoa, kisha tutajenga!.

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!.

Jee Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?- Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?.

Pascal
 
Hahaha ccm wao waliishakubaliana kumuunga mkono mtu wao hata kama ni hajui wao watamuunga mkono,mmeona wakiambizana na kulazimishana na kulazimishwa wananchi hadharani eti tumuunge mkono rais, hivyo hata kama hafanyi vizuri au hajui anafanya nini au hata sisi hatuoni matokeo tunayotaka kuyaona tunatakiwa kuunga mkono tu eti kisa ni rais aliyetokana na ccm.
Kwa wale wafia vyama mnapoona anapingwa jueni hakubaliki na hawezi jukumu hilo la urais, na mnapoona kuna maswali na mashaka kama hayo ya mtoa mada mfahamu mtu wenu ameshindwa.
Hoja ya kutaka aungwe mkono hata kama kashindwa kuongoza na kutumia rasilimali kuwanufaisha wananchi, huo ni upuuzi.
Busara ingetumika ingependeza, lakini kutumia nguvu kulazimisha failure iwe success ni upuuzi.
 
kiongozi hana vision,na wa karibu yake labda wana maono mazuri ,ila wakikutana na sentesi kama 'sipangiwi' wananywea
 
Ukitaka kujua uchumi umekufa njoo Kanda ya ziwa wavuvi wamefukuzwa kinguvunguvu ziwani eti uvuvi haramu kila kitu kime simama ni vibaka kwa kwenda mbele watu wanatupa watoto maisha magumu balaa kila mtu unaye msikia analaani serikari iliyopo madarakani
 
..wananchi wanashindwa kutoa michango midogo-midogo kwa ajili ya elimu ya watoto.

..huo ni ushahidi kwamba wananchi nchi nzima wana hali mbaya kiuchumi, hawana uwezo wa kulipia gharama ndogo-ndogo.
RAIs amekataza hiyo michango midogo midogo kwenye elimu. Ewe mhutu, njoo na data, not mere stupid words from nobody.
 
Wasomi wengi hawapendi kukosoa
 
Formula ya Mafanikio ya kiuchumi nchi hii ni:

TZ Economic Success = JK Economic Policies + JPM Management

Rudisha Kilimo kwanza.
Kilimo ndo uti wa mgongo wa uchumi wetu na ni njia ya uhakika ya Kulift mamilion kutoka katika umasikini. Tukihimiza viwanda kabla ya kuinua pato la mwananchi, Viwanda vingi viyakuwa vya investors na wananchi wataishia kuwa vibarua viwandani badala ya kuwa na capacity ya kuvimiliki.

Rudisha BRN
BRN ni vision, ni namna ya kuanzisha, kusimamia na kuendesha miradi kisomi na kitaalam zaidi. BRN chini ya Presidential Delivery Bureau ilisaidia katika miradi ambayo ni Landmark katika utawala wa JK, miradi kama ya umeme ilikuwa inasimamiwa chini ya BRN na ilikuwa inakwenda vizuri ( I hope bado inaenda vizuri). Kuondoa BRN ni kurudi ktk utaratibu wa zamani wa kufanya business ambao tumeshaona toka enzi za JKN, AHM, BWM kuwa siyo Optimal. Ofcourse matatizo ya BRN lazima yalikuwepo ilipaswa kuyatatua

Peleka Pesa za Serikali kwenye Mabenki ya biashara

Mabenki ni wadau wa maendeleo, wakiyumba na watu wanayumba, Serikali inao wajibu wa kuyasaidia mabenki yawe stable, kwa wenzetu wamarekani wao walikuwa wanayabail out, Sisi kwa kuwa hatuna pesa za kuyapa njia ya kuyabail out ni serikali kuweka pesa zake huko, ila inachoweza kufanya ni kukaa nayo mezani na kunegotiate nayo ili iwepo win-win, kwa mfano mathalan serikali ikitaka kukopa itakopa kwa riba ndogo sana, na pia kwa kuwa serikali imeweka mahela yake mengi huko then pindi Mabenki hayo yakikopesha hizo pesa kwa wadau wengine then serikali ipate percentage fulani nzuri ya faida. Namna hii ni nipe nikupe!. Bila serikali kufanya hivi naamini mabenki yatadorora zaidi.

Wekeza zaidi kwenye Diplomasia ya Kiuchumi.
Pambana kuleta wawekezaji, nenda duniani huko ongea na wawekezaji, tafuta miradi, tafuta masoko ya mazao ya kilimo, tangaza fursa zilizomo nchini, balozi zetu zipimwe kwa investments zinazoletwa nchini

Conclusion
Naamini, sera za kiuchumi za JK na Usimamizi madhubuti wa JPM wa kubana mianya ya rushwa, ufisadi na uzembe vinaweza kutusogeza
 
Unaongelea uchumi wakati wewe ni mganga wa tiba mbadala, wapi na wapi!,
Hata ukitaka kuiboresha nyumba yako ya zamani iwe ya kisasa lazima baadhi ya maeneo yabomolewe.
Mlizoea vya mtelemko, hapa kazi tu
Kwang mganga wa kienyeji hatafuti chakula?
 
Kama bado mnategemea serikali ya CCM ije itatue umasikini poleni.
Miaka 56 madarakani wanaopanda kiuchumi ni viongozi wa serikali tu

Ndiyo sababu hawataki kuretire,ukiona ameretire anakimbilia Ubunge ili awe Waziri,ni wale wale waliokuwa watendaji wakirudi wanakuwa Mawaziri.
 
kiongozi hana vision,na wa karibu yake labda wana maono mazuri ,ila wakikutana na sentesi kama 'sipangiwi' wananywea

Na aliwaambia kwenye Mkutano Mkuu hapokei ushauri,mtu wa aina hii hafai kuwa Kiongozi wa Taifa kubwa kama letu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…