Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hii ni Serikali ya Viwanda Uchwara!

Serikali ya Chama Uchwara!
Chenye Wanachama Uchwara!
Wenye mawazo uchwara!
Wakiendesha Bunge Ki-uchwara!
Chini Ya Naibu Uchwara!
Serikali ya watendaji uchwara!

Ikikandamiza Wanyonge Kwa Sababu Uchwara!
 
Serikali ya Wanyonge imeweza kumsaidia mnyonge Lugumi na maswahiba wake wanyonge wenzie kwa kuchakachua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali iliyoonyesha kwamba baada ya kulipwa shilingi bilioni 36, mnyonge Lugumi na maswahiba wake wanyonge walifunga mashine 14 tu katika vituo 108 walivyotakiwa wafunge mashine hizo.

Serikali ya wanyonge haikuona umuhimu wa kufuatilia kwanini mkataba huo haukutangazwa ili wanyonge wengine nao waweze kutuma maombi yao kuomba mkataba. Hivyo mnyonge Lugumi na maswahiba wanyonge wenzie wameshasafishwa rasmi na hawana kesi ya kujibu.
 
Wewe naona unaishi somalia wakati mapato bandarini yameshuka kwa kukimbiwa na wateja bado unaota?
 
Inabidi watanzania wajitambue hapa hakuna mnyonge anafaidi Bali in hii serikali hii ya ccm inaendelea kujitia kipato kwa sababu ni walewale
Ccm ni ileilee ooooh ni ileilee
 
serikali hii mgao wa umeme hauonekani
Serikali ya wanyonge sasa mlo kwa mnyonge ni mmoja tu baada ya kuongeza bei ya sukari na gharama za maisha kupanda tu nakula ugali saa 10 jioni tu imetoka
 
Doooh, tulishakubaliana na hali halisi asee
 
Serikali ya wanyonge kina lugumi imejahidi kuwasafisha kina lugumi sasa ni weupe kama malaika
 
Reactions: BAK
Serikali ya wanyonge imewakumbatia wanyonge wenzao watumishi wa serikali hii wanaomiliki majumba 40 hadi leo hatujui wameishia wapi
 
....... ingekuwa basi ningeshuka!
 
Mkuu huu mchezo hauhitaji hasira, mambo yote hayo yatachukuliwa hatua thabiti. Ndiyo kwanza serikali ya Rais mwenye weledi katika utendaji na uzalendo wa hali ya juu hajafikisha hata mwaka na kufanya mabadiliko makubwa ambayo yamewafanya ukawa kushikwa na butwaa! Kimsingi hofu ondoeni Jemedali Magufuli atatekeleza malalamiko yenu yote ila kwa awamu. Nasema mchezo huu hauhitaji hasira!!!
 
Mnyonge haruhusiwi kukosoa serikali bali kusifia tu!! Ukikosoa jela ni yako
 
Wewe naona unaishi somalia wakati mapato bandarini yameshuka kwa kukimbiwa na wateja bado unaota?
Swala hili halihitaji akili kubwa, walioikimbia bandari ni wateja wakwepa kodi. Ila kwa hao wachache wanaolipa kodi stahiki, hufanya makusanyo yawe sawa au kuzidi yale yakipindi kile watu wa bandari walipokuwa wanachumia matumbo! Hivi nyie ukawa leo hii nyie ndiyo mnatetea maovu!!
 
kuendelea kukaa hapa kubishana na watu wasiojua nini wanafanya bora nichukue jembe nikalime,kwanza nishukuru tu nipo kijijini huko naona umeme umeingia tayari,asante serikali japo ni wajibu wenu lakini asante kwa kutimiza huo wajibu.....
 
Bandarini sasa hivi watu wanacheza bao tu maana kazi hakuna na kenyatta ashasema nyinyi jengeni bomba la mafuta yeye anacheza na bandari tu
 
kuendelea kukaa hapa kubishana na watu wasiojua nini wanafanya bora nichukue jembe nikalime,kwanza nishukuru tu nipo kijijini huko naona umeme umeingia tayari,asante serikali japo ni wajibu wenu lakini asante kwa kutimiza huo wajibu.....
Na bili watakuja kukulipia
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…