Magufuli anatupeleka hapa:-
1. Nilikuwa nanunua mafuta ya gari 2,200 October 2015, sasa nanunua 1,782
2. Nilikuwa nafuatilia hati ya kiwanja changu Kigamboni toka 2011 nasumbuliwa, nimeenda January mwaka huu 2016, hati yangu imetoka March 2016.
3. Nilikuwa nikienda kwenye ofisi za uma kuhudumiwa ni kama vile naomba, sasa hivi nikiingia nahudumiwa kama mfalme.
4. Nilikuwa nafuatilia kuweka maji ya dawasco kwenye nyumba yangu toka 2014 nasumbuliwa, sasa hivi dawasco wamenifuata wenyewe waniwekee maji bure nitalipa kwa miezi 12 ijayo.
5. Nilikuwa nikishuhudia wafanyabiashara wakubwa wote wakikwepa kulipa kodi hapa bandarini, sasa hivi naona wote wakikimbilia TRA kulipa kodi wenyewe, na hakuna tena ki"memo" cha kutoa mzigo
6. Nimeshuhudia bajeti ya maendeleo ya Taifa ikiongezeka tofauti na miaka yote iliyopita, huku matumizi ya ndani tukiyagharimia kwa pesa zetu wenyewe.
7. Nilikuwa natumia masaa mawili toka sinza hadi mjini, sasa hivi MWENDO KASI natumia dakika 25.
8. Ninapotumia gari yangu Moroko hadi sayansi nilikuwa natumia saa nzima, sasa hivi nahisi natumia dakika 3-5 hivi
9. Wale waliokuwa wanafuja pesa na kusababisha vitu vinapanda bei, kwa kuwa wao hawabageni kwenye kununua, mfano kiwanja mtu anauza 20 million, wewe unajibana umbembeleze akuuzie 12 million, anatokea mfuja pesa zetu ananunua kwa 25 million, sasa hivi hakuna tena jeuri ya pesa zisizokuwa zako.
10. Ninashuhudia mengi ambayo nikimtafakari Magufuli, nahisi kuna haja ya kubadilisha katiba atawale miaka yote kama Mgabe.