Jmc06, Magufuli akishinda 2020 najisaidia mafungu mafungu kutoka Mwanza hadi Dar.
Wewe ongelea hii mitano kama atatoboa!
Mlisema hivyo mwaka Jana October mpaka leo sijaona Hata mmoja wenu aliyekunya,wengi wenu mnaolalamikia utawala huu ni vijana mliozunguka mjini,asilimia 75 ya watanzania wanaishi vijijini,na wengi ni wakulima pamoja na watoto wao,Kwa wakulima wa kahawa,korosho,pamba,nyanya,Michele,miwa,matunda nk,wanapenda serikali hii kuliko serikali yoyote,maana wamepunguziwa kodi kibao na Maisha kwao yameboreshwa kuanzia ada mashuleni na madawati kila kona ya nchi na u serious kwa manesi wakienda hospitalini,unaviona ni vitu kidogo,ila Kwa makini ni Mwanga umulikao kilometa nyingi sana.,
CCM ilipata wabunge 186 na UKAWA ni 35 (bila wale wa kuteuliwa),wengi wa hawa wa CCM walitoka vijijini,CCM ina matawi kila IATA na kijiji nchi nzima,na ndo nguvu kubwa ya wapiga kura walipo,.
Mianya mingi ya uvujaji wa pesa imezibwa na madili mliyozoea hakuna tena,ndo kisa cha kushinda mnalalamika humu JF,ila kundi lenu ni dogo sanaaa,kwa mchapakazi na mkulima wa kipato halali wa miaka yote Mimi nikiwemo, hii serikali ni nzuri sanaaa,na ninaomba JPM akaze Uzi zaidi,Kwa waliozoea michongo ndo mnaendeleza kampeni 24/7 mkipeana moto kwenye mitandao mkidhani wa TZ wengi wanawasapoti kumbe ni wachache kuliko unavyodhani.
Mwisho mgombea wenu wa UKAWA mwaka Jana September aliwahi kusema upinzani usipochukua dola 2015,itawachukua miaka 50 kuchukua dola sababu alimjua mtu anayekuja JPM akishinda atarudisha nidhamu iliyopotea miaka mingi nchini,kama Lile kundi nililokwambia mwanzo wakulima nk wanasonga vizuri kuliko miaka yote ya nyuma hizi kelele za upinzani Mara dikteta haina maana kwao sanasana ni kupoteza muda tu.
Ushauri wangu vijana changamkieni fulsa,nendeni wizara ya viwanda na biashara Kuna michongo mingi sana,malalamishi humu yatawapotezea muda sanaa,mkijakushtuka too late,hayo mnaowaita mashujaa wa upinzani wapo kazi ni wanapewa ruzuku Hata wakilala rumande wanalipwa, ni hayo tu.