Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Mi nimeshamaliza kuichambua! Nimeondoa mbegu zote, hapa nasubiri jua kidogo yu, ikauke nianze kufanya yangu!
 
Jumapili njema jamani,
Watz inabidi tuzielewe jitihada za JPM,Amekuta mizigo na mafuta mengi inapita bandarini inakoenda haijulikani,kaanzisha EFD ili kuipa TRA ufanisi wa ushuru lakini pia kama ni mfanya biashara usiwanyonye watz wenzio kwa kuuza bila kodi,na pia kuingiza mizigo isiyolipiwa ushuru..Hapa kwenye EFD sisi ndio tunanunua nahatuchukui risiti,kwenye visima vya kuuza mafuta baadhi wameweka kopo kukinga risiti zisimwagike.
Amekomaa na matumizi ya vitambulisho vya Taifa ili tupate fursa zilizokuwa zimebanwa na raia wa kigeni haswa wakenya,Kwa mfano mererani wajaluo na wamsai wa kenya walikuwa wengi sana sasa hivi kuingia ni tabu kwao,wameanza kuondoka.sasa ni fursa kwetu tukazichukue zinazoachwa na hao wajaluo.
Uhamiaji na idara ya kazi,nao wamepunguza kuwabeba wahindi na wakenya sehemu nyingi kuna nafasi za kazi wakiwasubiria watu wao waje wapewe kazi lakini muda unavyokwenda watakata pumzi tuwatatuajiri wenyewe,tukikomaa hizo post wataajiriwa watanzania tu.Ni wakati wa WATZ tusimame kifua mbele na tuiunge juhudi za serikali yetu.
Sasa basi tuwataje wafanyakazi wageni na kazi wanazofanya ili idara ya kazi ikahakiki ukweli wa hivyo vibali.
 
pia amekuta mishahara ya watumishi ikiongezwa kila mwaka ila yeye akapiga pin

akasaini sheria ya 15% bodi ya mikopo hata kile kidogo walichokuwa nacho nacho akanyang'anya

ngoja tuendelee kuwelewa taratibu
 
JPM kachemka mnajitahidi kumtetea kwa kusema watanzania hatumuelewi JPM ana nia nzuri. Yani miaka miwili haeleweki kitu anafanya zaidi ya vijembe na kukurupuka.

Baada ya mwaka mmoja na nusu mbele mtakosa cha kumtetea.
 
JPM kachemka mnajitahidi kumtetea kwa kusema watanzania hatumuelewi JPM ana nia nzuri. Yani miaka miwili haeleweki kitu anafanya zaidi ya vijembe na kukurupuka.

Baada ya mwaka mmoja na nusu mbele mtakosa cha kumtetea.
yani akili zote za watanzania eti tunashindwa kumwelewa mpaka tueleweshwe na watu kama jinga lao barbarosa ofisa n.k? hiki kituko
 
Hivi ukiulizwa mbowe ameleta athari gani kwa wananchi Wa Tanzania hadi unamfanya kuwa public enemy?. Sababu ni kuwa upinzani?. Je unadhani upinzani usipokuwepo ndio afya zitaimarika, maji, elimu na kazi?. Fikiria kwa making, watu hawamuoni mbowe wanatazama aliyeapishwa. Kwa hiyo msijifiche kwenye kivuli.
 
Vyama vya siasa mwiko kufanya mikutano.
Waandishi wa habari wanakamatwa na wanapangiwa nini waandike.
Wanafunzi wananyimwa mikopo na kuitwa vilaza.
Mishahara hawapandishi wamekataa.
Viongozi wa dini wakihubiri wanakamatwa na kutafutiwa uraia wa nchi za nje.
Sasa Makanisa yanataka kufutwa - TEC na KKKT na maaskofu wake kutishiwa kukamatwa

Swali huu utawala unamwongoza nani ? Ilianza na wanasiasa kuteswa, wakaja waandishi, ikaenda kwa wafanyakazi ikawafuta wafanyabisahara , ikaenda kwa wanafunzi sasa imeingia kwa makanisa makubwa na makongwe nchini - Nani anaongozwa hii serikali ipo kwa ajili ya nani ?

Hakuna mwenye amani hakuna aliyesalama hakuna mwenye uhakika wa uhai asubuhi.

Hii serikali ni ya watu gani ?????????????????????????????????????????????????????
 
Najibu kulingana na TITLE content yako sitosoma

Mh. Magufuri hii nchi anaipeleka jehanam
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…