Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Andiko la kikakamavu sana ! yaani umempa makavu matupu waziwazi ! hakika jf ni kiboko ! unajua nilikuwa sijaona uzi huu mpaka nilipopigiwa simu na Waziri mmoja mstaafu akiniomba niangalie jf kuna uzi wa Salary Slip kuhusu kumpa makavu mtu
 
Andiko la kikakamavu sana ! yaani umempa makavu matupu waziwazi ! hakika jf ni kiboko ! unajua nilikuwa sijaona uzi huu mpaka nilipopigiwa simu na Waziri mmoja mstaafu akiniomba niangalie jf kuna uzi wa Salary Slip kuhusu kumpa makavu mtu
Hahahaaa!!Kamanda umenifurahisha lakini pia nakushukuru.
 
Mkuu 2020 kesho tu. Mtakuja tena na maneno haya haya hadi 2025 mtakapowekewa chuma kingine tena,.

Hamjielewi. Yaani sijui mtajifunza lini?
Yaweza kuwa kweli kwa vile tukisema Time Hutu hatusikiwi mpaka tuombe msaada wa kusemea na WB au EU kisha tunaambiwa sio wazalendo.
Pia Mahakama zikisema MaDED ni makada tuwaweke pembeni mnaagiza maDAS (ambao pia ni makada) wawe returning officer's.
Huku mnahakikisha Policeccm wahapo nyuma kutumika. Sasa unapotukebehi kwa maamuzi sawia ya uchaguzi unataka nini kama sio kukinukisha?
Kina mahali mnadhani Watanzania ni waoga sana, lakini niwaambie hao mnaowaita waoga wakipata mhamasishaji wa ndani (sio fake kama Mange ambaye aliwatoa jasho kipindi cha mvua) nchi hii inaharibika Mara moja kuliko Somalia,Sudan, Malawi,Libya nk.
Hivi kina nchi ilikuwa shwari kama Ivory Coast hapo awali? Lakini ilikuja kuchafuka hadi watu kama nyie vibaraka wa watawala wakawa wanakatwa viganja. Leo kina idadi kubwa ya watu hawana viganja.
MSIYAOMBE HAYO, TUHESHIMIANE TUJENGE NCHI PAMOJA.
 
Sasa ndo tumepotea hasa, na yeye mwenyewe na wenzake wamepotezana pia...
 
Watanzania tunahitaji kubadirisha dereva, pamoja na kwamba gari ni bovu[Mifumo] lakini dereva mwerevu anapaswa alipeleke service. huyu wa sasa analiburuza tu hata kwenye makorongo anawaza kufika kabla ya wakati
 
Hali imekuwa tete upande wa pili wa shilingi, Rais John Pombe Magufuli atufai, anatupeleka kubaya, hafuati katiba na makelele mengine mengi.
Inazidi kutia shaka hasa kakundi ambako kiukweli kanaonyesha kulia kwa maumivu makali yasiyo vumilika (yaani ubatizo wa moto).
Ni kama wamebanwa katika vaisi hata wameanza kukosa pumzi, shamba la bibi limegeuka kuwa shamba la mama.
Wote tumewekwa katika mstari mabeberu na vibaraka tunawasika, wanalia. Walianza vibaraka sasa tunawasikia mabwana wenyewe ujue sinadano zimeingia mahala pake.

Jamani huu ndiyo ubatizo wa moto kama ule wa petrol, na kwa taarifa kila goti litapigwa, kila jicho litaona na kila sikio litasikia yakuwa shamba la bibi limerudishwa kwa mama mwenye watoto wake.

Kilakitu kinachofaa na kisichofaa kinasababu zake za kufaa na kuto kufaa. Sasa tuangalia Mzee Baba Mbatizaji kwa Moto kwanini hatufai.
Magu hatufai kwa haya:-
  1. Kuleta mradi mkubwa wa umeme wa Stigilazii Goji (mega watt 2100)
  2. Elimu bure
  3. Flayaova
  4. Ujenzi wa mabarabara nchi nzima, hili ni mbaya zaidi.
  5. Kurudisha nidhamu kazini.
  6. Vita harisi ya mafisa. Hili pia ndiyo hatufai kabisa.
  7. Wafanya biashara wadogo kusaidiwa
  8. Kurudisha huduma za afya.
  9. Kuzuia madawa ya kulevya kuwafikia watoto wetu.
  10. Kudhibiti utoroshwaji wa madini, hili kwa mabeberu ndiyo hatufai kabisa.
  11. Madawati nchi nzima watoto wasikae chini.
  12. Kubadilisha nchi kuwa ya viwanda
  13. ujenzi wa Treni ya umeme Dar mpaka Dom.
  14. Kununua ndege.
  15. Kuondoa vyeti feki.
  16. Kukomaa hadi kuhakikisha mradi mkubwa wa bomba la mafuta unapita Bongo na si kenya.
  17. Kuletwa kwa sera ya Utumbuaji.
  18. Ujenzi wa meli mpya kubwa katika ziwa Vikitoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.
  19. Utekelezaji wa mradi wa UMEME vijijini nchi nzima
  20. Kuwabana wapigaji.
  21. Serikari kuamia Dodoma
  22. Kuzuia safari za nje

Haya ndiyo yanayosababisha Dr. Pombe hasitufae kuwa kiongozi katika nchi hii. Mimi nasema kama sababu ni hizi atafia ofisini labda kuwe na sababu mbadala.
 
Kazuia bandarini kule watu tunashindwa kuingiza mizigo yetu ya dili. Kitu cha millioni 10 watu tulikuwa tukiingiza kwa millioni 2 tu..mfyuu
 
Kuna kitu kimekosekana kwenye thread yako
Sitaki kukitaja lakini wanaofuatia kukomenti watakisema kitakusaidia kufikia lengo la uzi huu
Asante
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…