Hali imekuwa tete upande wa pili wa shilingi, Rais John Pombe Magufuli atufai, anatupeleka kubaya, hafuati katiba na makelele mengine mengi.
Inazidi kutia shaka hasa kakundi ambako kiukweli kanaonyesha kulia kwa maumivu makali yasiyo vumilika (yaani ubatizo wa moto).
Ni kama wamebanwa katika vaisi hata wameanza kukosa pumzi, shamba la bibi limegeuka kuwa shamba la mama.
Wote tumewekwa katika mstari mabeberu na vibaraka tunawasika, wanalia. Walianza vibaraka sasa tunawasikia mabwana wenyewe ujue sinadano zimeingia mahala pake.
Jamani huu ndiyo ubatizo wa moto kama ule wa petrol, na kwa taarifa kila goti litapigwa, kila jicho litaona na kila sikio litasikia yakuwa shamba la bibi limerudishwa kwa mama mwenye watoto wake.
Kilakitu kinachofaa na kisichofaa kinasababu zake za kufaa na kuto kufaa. Sasa tuangalia Mzee Baba Mbatizaji kwa Moto kwanini hatufai.
Magu hatufai kwa haya:-
- Kuleta mradi mkubwa wa umeme wa Stigilazii Goji (mega watt 2100)
- Elimu bure
- Flayaova
- Ujenzi wa mabarabara nchi nzima, hili ni mbaya zaidi.
- Kurudisha nidhamu kazini.
- Vita harisi ya mafisa. Hili pia ndiyo hatufai kabisa.
- Wafanya biashara wadogo kusaidiwa
- Kurudisha huduma za afya.
- Kuzuia madawa ya kulevya kuwafikia watoto wetu.
- Kudhibiti utoroshwaji wa madini, hili kwa mabeberu ndiyo hatufai kabisa.
- Madawati nchi nzima watoto wasikae chini.
- Kubadilisha nchi kuwa ya viwanda
- ujenzi wa Treni ya umeme Dar mpaka Dom.
- Kununua ndege.
- Kuondoa vyeti feki.
- Kukomaa hadi kuhakikisha mradi mkubwa wa bomba la mafuta unapita Bongo na si kenya.
- Kuletwa kwa sera ya Utumbuaji.
- Ujenzi wa meli mpya kubwa katika ziwa Vikitoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.
- Utekelezaji wa mradi wa UMEME vijijini nchi nzima
- Kuwabana wapigaji.
- Serikari kuamia Dodoma
- Kuzuia safari za nje
Haya ndiyo yanayosababisha Dr. Pombe hasitufae kuwa kiongozi katika nchi hii. Mimi nasema kama sababu ni hizi atafia ofisini labda kuwe na sababu mbadala.