Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We una hela??Watanzania acheni maneno ya mtandaoni
Nchi iko shwari, wapotoshaji hawajawahi kuisha
Mkuu umekumbuka shuka asubuhiKwa hali ilivyosasa,pamoja na janga hili la corona tulitakiwa kuwa na rais mwenye leadership skills,ili aweze kutuongoza vizuri watanzania na kututoa hapa kwenye mkwamo huu wa corona.
Ukiangalia kule Uganda rais museven anafanya kazi kubwa sana na matokeo yanaonekana,lakini hapa kwetu hatujui tunaenda wapi wala tunatoka wapi,kila kitu ni kimya tu hadi huzuni,ukijaribu kuongea unatishiwa kuwekwa jela.
Nafikiri kama tungemchagua hata manywele meupe mwaka 2015 labda angetuongoza vema katika kipindi hiki kigumu cha corona
Huu ni mtazamo wangu tu,sitaki matusi wala lugha za kejeri kwa mtu au kiongozi yoyote.
Mods naomba huu uzi usiupeleke kwenye jukwa la siasa au kuufuta kwani sijamkashfu kiongozi yoyote lakini nimetoa mtazamo wangu tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo hata sio la kushangaa ndio utajua akili za watazania vizuri,pamoja na madudu yote haya ila nakuambia huyu jamaa uchaguzi wa mwaka huu atapita kwa zaidi ya asilimia 80Anasema watu wasipanic wakat kashaona kakosea na amepanic matokeo yake badala ya kutulia na kujenga uya anazid kubomoa......! Kukosea si tatizo sana tatizo ni kukubali umekosea na kujirekebisha....
Ata ivyo Watz ni watu wa ajabu sana utashangaa uchaguz ujao amepita kwa kishindo!
Cha msingi jilinde ww na familia yako na uwaoendao kila mtu apambane na hali yake.....!
Sent using Jamii Forums mobile app
Tunakoelekea ni kazi tu.
Tulipoanzia ni kutumbua wafanyakazi hewa na kutengeneza afya bora kwa wafanyakazi wetu na Elimu bora .
Kwa sasa tuko na kazi ya kukusanya Kodi na kuweka taratibu sahihi wa matumizi sahihi ya Kodi .
tumekbidhi nchi washamba-ZZKwafanyakazi hewa tumewatoa, tumesave pesa,
mishahara ya wafanyakazi wa serikali hatujaongeza, tumesave pesa
Tumeongeza kodi na TRA wanakusanya kodi sana manake raisi anafuatilia kwa makini , Tumeongeza pato
Tumepunguza safari za nje, Tumesave pesa.
Tumetumbua mafisadi Tumesave pesa.
Mwaka jana mwishoni Magufuli akasema Tuna reserve ya hela haijawah kutokea toka Tanzania imeanzishwa na inaweza kutupiga tafu miez sita hata kama bila kufanya kazi,
Mwez mmoja baadae CORONA HIT THIS COUNTRY na Mambo yakawa hivi,
1. Healthy system karibia zote zimejam they are overpopulated,
2. Ventilator hazitosh.
3. Inchi haina hela na sijui zimeenda wapi
4. Watu wanakufa kama kuku.
5. Magufuli mwenyewe kwa mdomo wake anasema hatuwez kufanya lockdown watanzania ni maskin sana anasahau mwaka jana alisema Tutembee kifua mbele hii nchi watu ni matajiri sana.
6. Kakimbilia kijijin kwao huko.
NB: Ukiwa mwongo usiwe unasahau mapema, na kinachonishangaza kupunguza kote garama huko nchi bado haina hela zinaenda wapi hiz kodi zetu jaman !?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.
Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.
Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.
Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.
Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?
Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.
Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
tumekbidhi nchi washamba-ZZK
muhimu busara zaidi itumike hasa kipindi hiki haya mambo ya ujuaji mwingi utaligharibu sana taifa letu kwa kizazicha sasa na kizazi kijacho basi tu Mungu atusaidie kwa kila haliHuu ni muda Wa kumwambia ukweli kwamba hatumtaki tena.
Ana roho mbaya,mbinafsi na mjuaji sana.
Fikiria amekataa kufunga mkoa Wa dar Kwa kuona pesa ni muhimu kuliko binadamu wanao umia na wengine kufa.
Ametukimbia dar na amekwenda mafichoni huko alikokulia maana sina uhakika kama alizaliwa huko.
Huko aliko amefunga mipaka ili yeye ajilinde na corona huku wananchi Wa mikoa mingine wakiteketea.
Tokea mwanzo Wa uongozi wake hakuwahi kupenda wananchi Wa dar,amewaumiza wengi Kwa kuwabomolea huku akiwa mikoa mingine akikataza ubomoaji Kwa sababu alipewa kura na hao.
Kwa nini tuendelee kuwa na Raisi Wa namna hii?
Ni vema bunge liangalie jinsi ya kumtoa madarakani sababu amefeli sehemu kubwa sana ya uongozi wake.
Sasa wananchi wengi wasio na hatia wanateketea bila kuonyeshwa njia za kujikinga ikiwezekana walazimishwe kujikinga.
Uoga ukizidi sana mwisho wake ni mauti,hakuna Wa kumkemea so viongozi Wa dini wala so wazee waliomzidi au kumtangulia umri,wote wako ndani ya friji.
Ifike mahali tuseme Kwa pamoja HAPANA.
Sent using Jamii Forums mobile app