Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Corona tutaishinda Watanzania tuondoe taharuki Tuendelee kuchukua tahadhari zinazotolewa na viongozi wetu wa Afya kuhusu kupambana na corona
 
Kwa hali ilivyosasa,pamoja na janga hili la corona tulitakiwa kuwa na rais mwenye leadership skills,ili aweze kutuongoza vizuri watanzania na kututoa hapa kwenye mkwamo huu wa corona.

Ukiangalia kule Uganda rais museven anafanya kazi kubwa sana na matokeo yanaonekana,lakini hapa kwetu hatujui tunaenda wapi wala tunatoka wapi,kila kitu ni kimya tu hadi huzuni,ukijaribu kuongea unatishiwa kuwekwa jela.

Nafikiri kama tungemchagua hata manywele meupe mwaka 2015 labda angetuongoza vema katika kipindi hiki kigumu cha corona

Huu ni mtazamo wangu tu,sitaki matusi wala lugha za kejeri kwa mtu au kiongozi yoyote.

Mods naomba huu uzi usiupeleke kwenye jukwa la siasa au kuufuta kwani sijamkashfu kiongozi yoyote lakini nimetoa mtazamo wangu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anasema watu wasipanic wakat kashaona kakosea na amepanic matokeo yake badala ya kutulia na kujenga uya anazid kubomoa......! Kukosea si tatizo sana tatizo ni kukubali umekosea na kujirekebisha....


Ata ivyo Watz ni watu wa ajabu sana utashangaa uchaguz ujao amepita kwa kishindo!

Cha msingi jilinde ww na familia yako na uwaoendao kila mtu apambane na hali yake.....!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We mwenywe na kiherehere chako ulimchagua huyo mwenye kiburi,,, tupambane tu na hali zetu ila huyu mtu atatufikisha pahala sio
 
Mkuu umekumbuka shuka asubuhi
 
Hilo hata sio la kushangaa ndio utajua akili za watazania vizuri,pamoja na madudu yote haya ila nakuambia huyu jamaa uchaguzi wa mwaka huu atapita kwa zaidi ya asilimia 80
 
Tunakoelekea ni kazi tu.
Tulipoanzia ni kutumbua wafanyakazi hewa na kutengeneza afya bora kwa wafanyakazi wetu na Elimu bora .
Kwa sasa tuko na kazi ya kukusanya Kodi na kuweka taratibu sahihi wa matumizi sahihi ya Kodi .

wafanyakazi hewa tumewatoa, tumesave pesa,

mishahara ya wafanyakazi wa serikali hatujaongeza, tumesave pesa

Tumeongeza kodi na TRA wanakusanya kodi sana manake raisi anafuatilia kwa makini , Tumeongeza pato

Tumepunguza safari za nje, Tumesave pesa.

Tumetumbua mafisadi Tumesave pesa.

Mwaka jana mwishoni Magufuli akasema Tuna reserve ya hela haijawah kutokea toka Tanzania imeanzishwa na inaweza kutupiga tafu miez sita hata kama bila kufanya kazi,

Mwez mmoja baadae CORONA HIT THIS COUNTRY na Mambo yakawa hivi,

1. Healthy system karibia zote zimejam they are overpopulated,
2. Ventilator hazitosh.
3. Inchi haina hela na sijui zimeenda wapi
4. Watu wanakufa kama kuku.
5. Magufuli mwenyewe kwa mdomo wake anasema hatuwez kufanya lockdown watanzania ni maskin sana anasahau mwaka jana alisema Tutembee kifua mbele hii nchi watu ni matajiri sana.
6. Kakimbilia kijijin kwao huko.

NB: Ukiwa mwongo usiwe unasahau mapema, na kinachonishangaza kupunguza kote garama huko nchi bado haina hela zinaenda wapi hiz kodi zetu jaman !?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
tumekbidhi nchi washamba-ZZK
 

Wewe ndugu; Mungu akubariki kokote uliko.
 
Jamaa bado lipo mafichoni chato?
 

Attachments

  • 2368410_17353465_1346268955433008_6567779633624083107_n-1.jpg
    37.3 KB · Views: 1
Huu ni muda Wa kumwambia ukweli kwamba hatumtaki tena.
Ana roho mbaya,mbinafsi na mjuaji sana.

Fikiria amekataa kufunga mkoa Wa dar Kwa kuona pesa ni muhimu kuliko binadamu wanao umia na wengine kufa.

Ametukimbia dar na amekwenda mafichoni huko alikokulia maana sina uhakika kama alizaliwa huko.

Huko aliko amefunga mipaka ili yeye ajilinde na corona huku wananchi Wa mikoa mingine wakiteketea.

Tokea mwanzo Wa uongozi wake hakuwahi kupenda wananchi Wa dar,amewaumiza wengi Kwa kuwabomolea huku akiwa mikoa mingine akikataza ubomoaji Kwa sababu alipewa kura na hao.

Kwa nini tuendelee kuwa na Raisi Wa namna hii?
Ni vema bunge liangalie jinsi ya kumtoa madarakani sababu amefeli sehemu kubwa sana ya uongozi wake.

Sasa wananchi wengi wasio na hatia wanateketea bila kuonyeshwa njia za kujikinga ikiwezekana walazimishwe kujikinga.

Uoga ukizidi sana mwisho wake ni mauti,hakuna Wa kumkemea so viongozi Wa dini wala so wazee waliomzidi au kumtangulia umri,wote wako ndani ya friji.
Ifike mahali tuseme Kwa pamoja HAPANA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
muhimu busara zaidi itumike hasa kipindi hiki haya mambo ya ujuaji mwingi utaligharibu sana taifa letu kwa kizazicha sasa na kizazi kijacho basi tu Mungu atusaidie kwa kila hali
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…