Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Umesahau hili kundi la tulioumia kwa mbeba maono wetu kupigwa marisasi hadi kufikia hatua ya kuchungulia kuzimu!!
 
Sioni Magufuli akipata hata 30% ya kura. Atapata kura za akina Makonda na ndugu zake wa Chatto anaowapa uteuzi kila siku.

Wa Tanzania wote au wenyewe au ndugu zao amewaathiri kimaisha kwa maamuzi haya:-
-Kuwaondoa wanafunzi wa UDOM waliokuwa wanasoma ualimu wa sayansi
- Kufuta wafanyakazi wa vyeti feki
- Kuwatumbua wafanyakazi bila kufuata sheria
- Kutopandisha mshahara na madaraja
- Kutotoa ajira kwa wahitimu wa vyuo
- Kuvunja nyumba za Kimara na kuachia za Mwanza
- Kubagua maendeleo majimbo ya wapinzani kama Kilwa
- Kuzuia wanafunzi wenye mimba wasiendelee na masomo
- Kumtimua CAG makini kwa vile kuulizia ufisadi wa Tsh 1.5 Trilion
-Kuua wakosoaji kama BenSaa Nane na Azory Gwanda
- Kutumia vibaya fedha za Serikali kama ujenzi wa kiwanja cha Ndege Chato na mbuga ya Burigi
- Kuwaweka rumande wafanyabiashara kwa makosa ya kubambikiza kama Rugemalira
-Kuwabambikiza makosa wakosoaji kama Kabendera
- Kutunga sheria kandamizi
-Kutawala kwa kidikteta.
- Kuvuruga wafanyabiashara kama Yusuf Manji

Nimeikuta sehemu.
 

Attachments

Hii ni kumkumbusha Rais Magufuli. Nakupenda kama binadamu mwenzangu kutoka moyoni, lakini nachukia sana matendo uyafanyayo kwa wapinzani. Kwa kuwa nakupenda kama binadamu mwenzagu sitaki upate shida maishani hasa baada ya kustaafu, hivyo nakukumbusha kuwa Tanzania siyo sovereign (huru) kama matendo yako yanavyoonesha bali kuna mambo yamepandishwa juu na kuwa ya kidunia zaidi na ambayo huwezi kuyaweka chini ya himaya yako upende usipende. Mambo serikali haiwezi kuyaweka chini yake nitayaongea siku nyingine. Kwa leo nina hili pekee.

Ili upate maisha mazuri yenye heri na baraka baada ya kuachia madaraka, japokuwa umekwisha liboronga mpaka sasa, tenda haki kwa wapinzani wako kisiasa kwa muda wako uliobaki. Mbali na hapo utashitakiwa ICC - huko The Hague. Dunia inakuangalia kwa ukaribu sana, inajua ulalapo na uondokapo. Mfano wa wazi ambao unaonesha hauko huru kama unavyofikiria fungua google map utazame namna majina ya kila eneo na barabara ilivyoainishwa online, je hii ni kazi ya wataalam wako?

HAPANA. Pia kila njia unayotumia kwa mawasiliano siyo ubunifu wa Tanzania bali ni wa hao hao unaowaita mabeberu, hivyo wana kumbukumbu ya kila ulifanyalo, na uwaagizalo wasaidizi wako. Uchaguzi wa mwaka huu ni mtego kwako. Chunga sana.

Wape uhuru wapinzani kwani katiba inaruhusu wayafanyayo. Kitendo cha Sugu kukamatwa, ofisi za CHADEMA kulipuliwa na msafara wa Tundu Lissu kupigwa mawe ni doa kubwa sana kwako.

USIKU MWEMA
 
We shall overcome
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…