Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Kamanda usipaniki. Ni wakati kila mtu ajue mipaka yake. Hakuna uhuru usio na mipaka. Jifanye kutukana mamlaka halali tukusikie.

Wewe hunipangii ni jinsi gani humu nachangia
lini uliniona nikimtukana hata Kikwete?
usiongelee hisia zako za kijinga ili kujifurahisha....
ningefurahi ungeacha kuni quote
kwa sababu ufinyu wako wa kuelewa unafanya nisipende kuku reply
 
Nakumbuka watu tulikuwa na imani na kikwete na kumshangilia kwa miaka miwili, lakini huyu hata mwezi tayari tushamchokaa
Ukisikia paaa, ujue jipu lishatumbuka..pole ndugu, jifunze kutafuta vya kuchinja, no more kunyonga
 
Wewe hunipangii ni jinsi gani humu nachangia
lini uliniona nikimtukana hata Kikwete?
usiongelee hisia zako za kijinga ili kujifurahisha....
ningefurahi ungeacha kuni quote
kwa sababu ufinyu wako wa kuelewa unafanya nisipende kuku reply

Hapo kamanda umenena. Maadam umekiri huwezi kukashifu mamlaka halali acha watukutu wengine sheria iwabane. Halafu kwa vile hii ni public forum ni wazi lazima utegemee comments zako zikaririwe na kujibiwa
 
Mimi nashuhudia matamko ya mkuu yakipinga na mawaziri wake
1.Wanawake katika kipindi changu mzae kwelikweli kwa kuwa elimu bure
2.Kauli ya kutonyanyaswa kwa wamachinga mjini iliyotenguliwa na mh.simbachawene
3.Udom ni vilaza iliyofafanuliwa na ndalichako(kauli zilipingana mno)
4. Nashuhudia mkuu kutosikiliza fikra za kila mwenye haki ya kumshauri
5.Nashuhudia watanzania kupewa magwangala na dhahabu kwenda Ulaya
6.Nashuhudia ubakwaji wa demokrasia nchini
Simuungi mkono mkuu kwa haya yangu na ya kwenu pia.Tanzania ni nchi salama
Hatutaandamana ila tunahitaji haki za kiraia na utii wa sheria na katiba ya nchi yetu.
Kwa hali ilivyo sasa SITAANDAMANA NA UKUTA sep 1. NIMEJITOA NIMEKUWA MFUASI WA AMANI KWA TAIFA LANGU JAPO UKUTA HAUNA LENGO LA KUVUNJA AMANI YETU.
 
Ninashuhudia mafisadi yakisakwa; Ninashudia mafisadi yakitumia vyama vya siasa kumdhoofisha; Ninamshuhudia akipambana NATO bila kuchoka; Ninamshuhudia wazalendo wa nchi hii wakiwa nyuma yake katika mapambano ya kuijenga Tanzania mpya; Ninamshuhudia watu wa mataifa mbalimbali wakitamani angelikuwa rais wao; Ninamshuhudia akiendelea kufanywa 'SI UNIT' ya uongozi bora Africa; Ninamshuhudia, Ninamshuhudia ...!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…