Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Hii style ya mr. POMBE aliyokuja nayo ya kutumbua majipu kwa mtazamo wangu naiona itamgharimu sio muda mrefu. maana ilikuja kama kibwagizo cha kusherehesha mbio zake za Kuukwaa ukuu wa nchi. na ni kweli ameukwaa.

Tatizo hapa si kutumbua majipu kwa maana kwa sasa amekuwa akiimba kila siku MAJIPU...MAJIPU imefikia sasa hata kuwaambukiza watendaji wake nao wamekuwa ni wa kutumbua hata pasipokuwa na jipu wao WANAMINYAAA TU!! ili muradi wametumbua hata vidonda wakiviona wanatumbua ilhali vidonda havitumbuliwi. HII NI SHEEDAH!!

Kinachomsumbua MR. POMBE me binafsi naona kama hakioni au anapapasa tu na kuambulia MAJIPU. Lakini tumkumbushe au nimkumbushe tu kwamba majipu anayotumbua pasua ni pasua kichwa tu lkn watanzania wanaumwa kweli tena sio ugonjwa huo wa majipu anaohangaika nao kila kukicha.

Kawaida duniani hapa kila nchi majipu ni sehem ya maisha hivyo hawezi kuyamaliza na yatampotezea muda wake wa miaka mi5 aliyopimiwa na wananchi wake.

USHAURI:
Rais Magufuli nakushauri uachane na majipu sababu haya sio tatizo kuu la wananchi au linaloimaliza NCHI HII KWA UJUMLA WAKE. Naomba hayo majipu waachie vijana wako watahangaika nayo kwa kadri ya ulivyowapa maelekezo. Wakishindwa utajua nini cha kuwafanya. Najua style yako ile FUKUZA WEKA NDANI itawafaa sana hawa vijana japo haimo katika taratibu na sheria za ajira zetu.

Rais Magufuli nakushauri achana na MAJIPU tunajua yakipata dawa hata PARACETAMOL yanakauka lakini hi KANSA!! Pambana na KANSA KUU ndio inayoimaliza nchi hii na hii kansa ipo ndani ya watendaji wako na nyingine unazijua vizuri tu hizo kansa kama EPA ,ESCROW, LUGUMI, RICHMOND, KIWIRA, na nyingine nyingi tu.

Kweli sijakusikia unazigusia hata kiduchu tunasikia tu unapambana na wauza SUKARI na wakwepa kodi wa Kariakoo.

Hebu tuliza kichwa anza na kimoja kati ya hizi kansa tuonyeshe kweli unahasira nazo kama unavoonyesha hasira wakati wa kuwatumbua watendaji wako hadharani kama yule jamaa wa jiji uliyemuadhiri wakati wa ufunguzi wa daraja.
 
Mh Raisi wangu Fanya kz usisikie maneno ya watu wa pembeni,maana ck zote MTU ukifanya jema wakukupinga juhudi zako hawakosi.....tunasema hapa kazi tuuuu
 
MAJIPU.........
MAFISADI.......
MAHAKAMA YA MAFISADI..........
HAKUNA MAANDANO.......
USIVAE CHATA YA UKUTA......
HAKUNA KUONGEA.... UKIONGEA NI UCHOCHEZI.....
HAKUNA MIKUTANO/VIKAO HATA YA HARUSI......
vikao vya ndani marufuku... kwa wapinzani tu....
hebu jazeni mengine yanayofuatia...
 
Mh Raisi wangu Fanya kz usisikie maneno ya watu wa pembeni,maana ck zote MTU ukifanya jema wakukupinga juhudi zako hawakosi.....tunasema hapa kazi tuuuu
hivi we unafanya kazi kweli au ndooo waleee.....
 
Ratiba ya kukutana kimwili na mkeo ni mara 1 kwa wiki ili kubana matumizi mbegu..zisiishe
wee sasa naona talaka inakuhusu.... mbegu nilizokumiminia umipeleka wapi... ujauzito wako feki.. nakupiga kibuti... mbafffff..
 
mwisho wa siku atasema hakuna mikusanyiko makanisani na misikitini.


swissme
 
2020 sijui kampeni zitaruhusiwa au tutachagua tu kimyakimya ili tupate muda wa kufanya kazi?
 
Angalao ameruhusu kufyatua watoto maana angepiga marufuku kufyatua watoto hapo ndiyo ningeandamana
 
MAJIPU.........
MAFISADI.......
MAHAKAMA YA MAFISADI..........
HAKUNA MAANDANO.......
USIVAE CHATA YA UKUTA......
HAKUNA KUONGEA.... UKIONGEA NI UCHOCHEZI.....
HAKUNA MIKUTANO/VIKAO HATA YA HARUSI......
vikao vya ndani marufuku... kwa wapinzani tu....
hebu jazeni mengine yanayofuatia...
Majipu, Mafisadi na Mahakama ya Mafisadi haya yalipoteza pesa nyingi sana za nchi
Hakuna maandamano,Usivae chata ya UKUTA, na yote uliyotaja ni dalili za uvunjifu wa amani lazima yapigwe stop
 
TANZANIA MPYA INAKUJA

Ni Tanzania iliyo na utulivu uliojaa hofu na nidhamu ya woga.
Ni Tanzania iliyo na vyombo vya habari ambavyo vipindi vyake vingi vitakuwa ni vya burudani zaidi na sio vile vya kufikirisha/kukosoa kwa nia njema/ au kuelimisha kwa sababu visije vikatafsiriwa vinafanya uchochezi.

Ni Tanzania itayokuwa na watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ambao post zao nyingi zikiwa ni zile za mipira, udaku, na mapenzi na sio zile za ukosoaji wa kujenga.

Ni Tanzania ambayo kuanzia mashuleni mpaka vyuoni "debates" mijadala haitakuwapo kwa sababu itatafsiriwa kuwa ni Sehemu ya ufanyaji wa Siasa.
Ni Tanzania ambayo ukivaa fulana/kofia/ au kutundika bendera ya chama cha upinzani itaonekana ni kosa la jinai.

Ni Tanzania ambayo vikao vya harusi/ mikutano ya dini/mikutano ya vikao mbalimbali itakuwa inalindwa na polisi ili kusikiliza mnajadili nini, msije mkawa mnajadili uchochezi.

Ni Tanzania iliyojaa watu wenye uoga wa kudhani kila atakachokifanya ataonekana anafanya uchochezi na hivyo kupelekea kufa kwa mawazo mbadala/vipaji na maarifa mbalimbali.

Hakuna kitu hatari kama huu utulivu ambao watawala huusisitiza kila wakati kwa wanachi, utulivu si sifa, ni kitu cha hatari kuliko hata sila za maangamizi.
Duniani kote hakuna mahali utulivu ulileta maendeleo kwa binadamu zaidi ya kumfanya aishi kama jana na kama juzi.

ILI TUENDELEE NA KUIPATA TANZANIA YA VIWANDA HATUNA BUDI KUWA NA UCHOCHEZI WA KIFIKRA NA MGONGANO WA MAWAZO/KUKOSOANA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom