Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Serikali ya Magufuli ilianza vizuri kwa kufuatilia rushwa, kurekebisha sheria mbaya na kuchagua watu wapya lakini sasa imeanza kufanya vitu vya kitoto. Polisi na Jeshi wakati huu wa kubana matumizi wanapoteza muda kukimbizana na viongozi wa upinzani na kutafuta wapinzani kwenye kumbi hadi za hotel, kesi zinapelekwa mahakamani kwasababu ya kumtukana raisi kwenye whatapp au facebook, maanadamano na mikutano kupigwa marufuku kwa sababu za kitoto ambazo huwezi kumdanganya hata mtoto wa darasa la saba. Raisi amekuwa na waongeaji kila kona kuanzia wakuu wa mkoa, polisi ... bila kufuata sheria yeyeote. Hii imeshusha uimara na muonekano wa Magufuli kwa wananchi wengi sana kuliko wanavyo fikiria. Hata mimi nilikuwa namuona Magufuli na jitihadi ni nzuri sasa najiuliza kama Magufuli ana busara! nasikitika sana
 
Haaaaa,, na haijulikani tena kama kweli hili zoezi la kuhamia Dodoma litafanikiwa au ilikuwa ni Siasa tu,,

Ni kweli anaongea vzr sn kwa nia ya kutukwamua hapa tulipo nasa ,, lakini hajui aanze kunasua kiungo gani ,, maana vyote kuanzia miguu ,, mikono vyote vimenasa,,

Sasa nani wa kumkumbusha ili aanze na kiungo kipi kutunasua huyo ndiye mtu mhimu sn kwa sasa,,

Ndege tunataka,, Reli ya kati tunaitaka,, nk vyote kwetu ni muhimu hata kuhamia Dodoma pia ni muhimu sn. tuanze na kipi?
 
Gene anazolazimisha mtukufu kuzipandikiza tunasubiri matokeo,hakika usipokua msukuma au mkijani namba ni ileile utaisoma tuu
 
Ni takribani mwaka sasa tangia huyu Rais aingie Ikulu ila vipaumbele vyake havigusi maisha ya Walala Hoi yeye ameamua kuanza na kununua Ndege tatu kuna mlala hoi anayepanda Ndege?
Ameamua kutumia mamilioni kuhamia Dodoma mbona hiyo haibadili chochote kwa mlala hoi, watoto wa Walala hoi mpaka leo amewanyima Pesa ya Field na walio pewa wamepewa pungufu tofauti na zamani,
Watoto wa Walala hoi wamekosa ajira kwa kisingizio cha watumishi Hewa mbona uhakiki hauishi maisha mzeee yanazidi kuwa magumu Walala hoi tumeanza kumkumbuka Baba Riz yeye maisha yalikuwa na unafuu........!!!!!
 
Kuhamia dodoma ndo mapngo mzima!
Au hujasikia madereva tax/madalali/wajenzi wanavosifia ukuaji wa kipato chao! bila kusahau jina la wanaume wa dar litaisha ss🙂
 
[emoji443] [emoji344] [emoji341] [emoji444] [emoji445] CCM ni ile ile, ni ile ile[emoji442] " mmeipenda wenyewe"[emoji445] [emoji441]
"Wacha waisome nambaaaaaaa[emoji341] [emoji344] [emoji442] [emoji450] [emoji448] [emoji449] [emoji448] [emoji447] CCM mbele kwa mbeleeeee!!!![emoji449] [emoji449] [emoji448] [emoji447]
 
Maradhi ya shinikizo la damu yataongezeka kutokana na watu kuzibwa midomo wasieleze fikra zao.
 
Sishangai huyo jamaa na Kagame asili yao ni mmoja. Kwa hiyo anajaribu kumuiga dikteta mwenzake. Ila asisahau mwenzake ni mwanajeshi.
 
Hizi danadana zinapigwa kwa ufundi wa hali ya juu sana.

Wizara moja kila mtu na tamko lake juu ya jambo moja.

Hivi mwanao akiugua malaria anazuiaje usizae mwingine mpaka huyo apone kwanza?

HEWA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom